3/04/2019

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | "Enzi ya Ufalme Ndiyo Enzi ya Neno" (Official Video)


Mwenyezi Mungu anasema, "Katika Enzi ya Ufalme, Mungu anatumia neno ili kukaribisha enzi mpya, ili kubadilisha mbinu za kazi Yake, na kuweza kufanya kazi katika enzi nzima. Hii ndiyo kanuni ambayo Mungu hufanyia kazi katika Enzi ya Neno. Alikuwa mwili ili kuweza kuzungumza kutoka mitazamo tofauti, kumwezesha binadamu kumwona Mungu kwa kweli, ambaye ni Neno linaloonekana katika mwili, na hekima Yake na maajabu. Kazi kama hiyo inafanywa ili kwa njia bora zaidi kutimiza shabaha za kumshinda binadamu, kumfanya binadamu kuwa mtimilifu, na kumwondoa binadamu. Hii ndiyo maana ya kweli ya kutumia neno ili kufanya kazi katika Enzi ya Neno."

      Kujua zaidi: Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu

3/03/2019

Matamshi ya Kriso—Sura ya 6

Mwenyezi Mungu, Mkuu wa vitu vyote, hushika madaraka Yake ya kifalme kutoka kwa kiti Chake cha enzi. Yeye hutawala ulimwengu na vitu vyote Naye Anatuongoza katika dunia yote. Mara kwa mara tutakuwa karibu Naye, na kuja mbele Zake kwa utulivu; kamwe hatutakosa wakati mmoja, na kuna mambo ya kujifunza wakati wote. Mazingira yanayotuzunguka pamoja na watu, mambo na vitu, yote yameruhusiwa na kiti Chake cha enzi. Usiwe na moyo wa kunung’unika, au Mungu hatatupa neema Yake juu yako.

3/02/2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 5



Milima na mito huenda ikibadilika, vijito hutiririka mbele, na maisha ya mwanadamu ni yenye uvumilivu mdogo kuliko ardhi na anga.
Mwenyezi Mungu pekee ndiye maisha ya milele yaliyofufuka milele, katika vizazi hai milele! Vitu vyote na matukio viko katika mikono Yake, Shetani yuko chini ya miguu Yake.
Leo hii ni kwa sababu ya uteuzi wa Mungu ulioamuliwa kabla kwamba Ametuokoa kutoka kukamatwa na Shetani.

3/01/2019

Wimbo Mpya wa Dini | "Kazi ya Mungu Inaendelea Kuboreshwa" | Have You Followed God's Footsteps?


Kazi ya Mungu inaendelea kuwa bora;
ingawa kusudi linabaki bila kubadilika,
mbinu ya kazi Yake inabadilika daima,
na hivyo pia wale wanaomfuata.
Kadiri ambavyo Mungu anafanya kazi zaidi,
ndivyo anavyozidi mwanadamu kumjua, kikamilifu,
ndivyo tabia ya mwanadamu inavyozidi kubadilika
pamoja na kazi Yake ifaavyo.

2/28/2019

Neno la Mwenyezi Mungu | Sura ya 4

Neno la Mwenyezi Mungu  | Sura ya 4

Daima tutakuwa tukiangalia na kusubiri, kuwa na utulivu katika roho na kutafuta kwa moyo safi. Chochote kitakachotufikia, tusishiriki kwa upofu. Twahitajika tu kuwa kimya mbele ya Mungu na daima kushiriki naye, na kisha nia Yake itafichuliwa kwetu. Roho zetu sharti daima ziwe tayari kutofautisha na sharti ziwe na bidii na zisiokubali kushindwa. Ni lazima tuteka kutoka kwa maji ya uhai mbele ya Mungu, maji ambayo huondoa kiu kutoka kwa roho zetu zilizokauka.

2/27/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 2

Kanisa la Filadelfia limechukua umbo, na hili limesababishwa kabisa na neema na rehema za Mungu. Watakatifu wameleta upendo wao wa Mungu mbele na kamwe hawakuyumbayumba kutoka kwa njia yao ya kiroho. Kuwa imara katika imani kwamba Mungu mmoja wa kweli Amekuwa mwili, ya kwamba Yeye ndiye Mkuu wa ulimwengu Ambaye hutawala vitu vyote—hii imethibitishwa na Roho Mtakatifu na ni ushahidi thabiti! Kamwe hauwezi kubadilika!
Eh, Mwenyezi Mungu! Leo Umefungua macho yetu ya kiroho, kuwaruhusu vipofu kuona, viwete kutembea, wenye ukoma kuponywa.

2/26/2019

Ushuhuda wa Mkristo: Jinsi Alivyoshinda Majaribu ya Kuwa na Mpenzi wa Siri (Sehemu ya 2)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Wakristo
 
Na Xiyue, Mkoa wa Henan
Katika siku chache zilizofuata, ingawa Jingru hakuwa ameanguka katika majaribu ya Shetani na alijua kwamba hangeweza kuwa mwenzi wa Wang Wei kamwe, mkutano wake na Wang Wei jioni hiyo na ungamo lake la kweli vilirudiwa akilini mwake tena na tena kama onyesho katika filamu …
Wang Wei alipompigia simu tena, moyo wa Jingru ulishtuka kidogo, naye akajiambia: “Sote wawili hatuwezi kuwa kitu kimoja, lakini bado tunaweza kuwa marafiki wa kawaida.

2/25/2019

Wimbo wa Maneno ya Mungu | Kiini cha Kristo Ni Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,nyimbo
I
 Mungu anayekuwa mwili anaitwa Kristo, na hivyo Kristo anayeweza kuwapa watu ukweli anaitwa Mungu. Si kupita kiasi kusema hivyo, kwani Ana kiini cha Mungu. Ana tabia ya Mungu na hekima katika kazi Yake, ambayo haifikiwi na mwanadamu. Wale wanaojiita Kristo wenyewe ilhali hawawezi kufanya kazi ya Mungu ni wadanganyifu. Wanaojifanya kuwa Kristo hatimaye wataanguka, ingawaje wanadai kuwa Kristo, hawana kiini chochote cha Kristo.

2/24/2019

Ushuhuda wa Mkristo: Jinsi Alivyoshinda Majaribu ya Kuwa na Mpenzi wa Siri (Sehemu ya 1)

 
Na Xiyue, Mkoa wa Henan
Jioni moja, Jingru alikuwa akinadhifisha kwake.
“Krr, krr.” Simu ilianza kulia. Aliijibu na sauti ngeni lakini bado inayojulikana ililia sikioni mwake: “Halo! Ni Wang Wei. Uko nyumbani!”
“Wang Wei?” Jingru kwa namna fulani alistaajabu: Kwa nini alikuwa akimpigia simu sasa baada ya miaka mingi sana?
“Ndiyo … niko nyumbani. Kuna nini?” aliuliza Jingru kwa mshangao.

2/23/2019

Ni kwa Kufanya Kazi Katika Mwili Pekee Ndiyo Mungu Anaweza Kumpata Binadamu

I
Kupitia katika neno la Mungu wa utendaji,
unyonge wa mwanadamu na uasi yanahukumiwa na kufichuliwa.
Kisha wanadamu wanapokea kile wanachohitaji.
Wanaona kuwa Mungu amekuja katika ulimwengu huu wa binadamu.
Kazi ya Mungu wa utendaji ina nia ya kumwokoa kila mmoja kutoka kwa ushawishi wa Shetani,
kuwaokoa wait kutoka kwa uchafu na tabia iliyopotoshwa na Shetani.

2/22/2019

Matamshi ya Mungu—Sura ya 86

Watu husema kuwa Mimi ni Mungu mwenye huruma na wao husema kwamba Nitaoa wokovu kwa kila kitu Nilichokiumba—mambo haya yote yanasemwa kulingana na fikira za binadamu. Kunitaja Mimi kama Mungu mwenye huruma kunaelekezewa wazaliwa Wangu wa kwanza na kuletea Kwangu wokovu kunaelekezewa wazaliwa Wangu wa kwanza na watu Wangu. Kwa sababu Mimi ni Mungu mwenye hekima, ni wazi katika mawazo Yangu ni nani Ninaowapenda na ni nani Ninaowachukia.

2/21/2019

Swahili Christian Video | Nyendo za Mateso ya Kidini Nchini China


Tangu kilipokuja mamlakani katika China Bara mnamo mwaka wa 1949, Chama Cha Kikomunisti cha China kimekuwa hakikomi katika mateso yake kwa imani ya kidini. Kwa wayowayo kimewashika na kuwaua Wakristo, kuwafukuza na kuwadhulumu wamishonari wanaofanya kazi nchini China, wakachukua ngawira na kuchoma nakala nyingi za Biblia, wakafunga kabisa na kubomoa majengo ya kanisa, na bila mafanikio wakajaribu kukomesha makanisa yote ya nyumbani.

2/20/2019

Wimbo Injili | Kutafuta Wandani

I
Umefanya kazi katika bustani kwa muda mrefu na Umepanda upendo Wako ndani sana.
Umelipa kila gharama, Ukitamani kuwapata watu ambao wana moyo mmoja na Wewe.
Umetafuta kwa muda mrefu—ni nani anayeweza kuelewa dhiki Yako?
Umewekeza upendo mwingi sana wa kweli, lakini ni vigumu Kwako kupata faraja katika maumivu Yako.