11/09/2017

Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mungu
Umeme wa Mashariki | Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu

Umeme wa Mashariki | Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu

Mwenyezi Mungu  alisema, Kazi ya kumsimamia mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu, na ina maana kuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu. Hatua hizi tatu hazihusishi kazi ya kuuumba ulimwengu, ila ni hatua tatu za kazi ya Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Kazi ya kuiumba dunia ilikuwa kazi ya kusababisha uwepo wa wanadamu wote. Haikuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu, na haina uhusiano na kazi ya kumwokoa mwanadamu, kwa kuwa dunia ilipoumbwa mwanadamu hakuwa amepotoshwa na Shetani, na hivyo hakukuwa na haja ya kutekeleza kazi ya kumwokoa mwanadamu.

11/08/2017

Umeme wa Mashariki | Sura ya 23

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu,

 Umeme wa Mashariki | Sura ya 23

 Ninapopaza sauti Yangu, macho Yangu yanapofyatua moto, Ninaitazama kwa uangalifu dunia nzima, Ninatazama kwa uangalifu ulimwengu mzima. Wanadamu wote wananiomba Mimi, wameinua macho yao kuelekea Kwangu, wakiomba Nipunguze hasira, na kuapa kutoniasi tena. Lakini haya siyo yaliyopita; bali yaliyopo kwa sasa. Ni nani anayeweza kubadilisha mapenzi Yangu? Kwa kweli sio sala katika moyo wa mwanadamu, wala maneno yanayotoka midomoni mwao? Ni nani ambaye ameweza kuishi hadi wakati huu, isipokuwa ni kwa nguvu Zangu? Ni nani anayeishi ila kwa maneno ya kinywa Changu? Ni nani asiyekaa chini ya uangalifu wa macho Yangu?

11/07/2017

Umeme wa Mashariki | Dhambi Zitampeleka Mwanadamu Jahanamu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,maombi
Umeme wa Mashariki | Dhambi Zitampeleka Mwanadamu Jahanamu
Mwenyezi Mungu alisema, Nimewapa maonyo mengi na kutawaza juu yenu kweli nyingi ili kuwashinda. Leo mnajihisi kustawishwa zaidi kuliko mlivyokuwa hapo zamani, kuelewa kanuni nyingi za jinsi mtu anapaswa awe, na kumiliki kiasi kikubwa cha maarifa ya kawaida ambayo watu waaminifu wanapaswa kuwa nayo. Hiki ndicho mmepata baada ya miaka mingi sasa. Mimi sikani mafanikio yenu, lakini lazima Niseme wazi kuwa Mimi pia sikani kutotii kwenu kwingi na uasi dhidi Yangu hii miaka mingi, kwa sababu hakuna hata mtakatifu mmoja kati yenu, bila yeyote kuachwa nyuma nyinyi ni watu mliopotoshwa na Shetani, na maadui wa Kristo. Dhambi zenu na kutotii kwenu hadi sasa havihesabiki, hivyo si ajabu kwamba Mimi daima Hujirudia mbele yenu. Sitaki kuishi hivi na nyinyi, lakini kwa ajili ya siku zenu za baadaye, kwa ajili ya hatima zenu, Mimi hapa Nitarudia Niliyoyasema mara nyingine tena.

11/06/2017

Kuwa Mzingatifu wa Mapenzi ya Mungu ili Upate Utimilifu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mungu,Umeme wa Mashariki
Umeme wa Mashariki | Kuwa Mzingatifu wa Mapenzi ya Mungu ili Upate Utimilifu
Mwenyezi Mungu alisema, Kadiri unavyozingatia mapenzi ya Mungu, ndivyo unavyokuwa na mzigo zaidi; kadiri unavyokuwa na mzigo, ndivyo uzoefu wako utakuwa mwingi zaidi. Unapokuwa mzingatifu wa mapenzi ya Mungu, Mungu atakupa mzigo huu, na Mungu atakupa nuru ya mambo ambayo amekuaminia. Baada ya Mungu kukupa mzigo huu, utaangalia ukweli wa kipengele hiki unapokula na kunywa maneno ya Mungu. Kama una mzigo unaohusiana na hali ya maisha ya ndugu, huu ni mzigo ulioaminiwa kwako na Mungu, na sala zako za kila siku daima zitaubeba mzigo huu. Kile ambacho Mungu hufanya kimeaminiwa kwako, uko radhi kutekeleza kile ambacho Mungu anataka kufanya, na hivi ndivyo inavyomaanisha kuuchukua mzigo wa Mungu kama wako. Wakati huu, kula na kunywa kwako maneno ya Mungu kutalenga masuala katika vipengele hivi, na utafikiri, nitayatatuaje masuala haya? Nitawaruhusu vipi ndugu kufunguliwa, wawe na furaha katika nafsi zao?

11/05/2017

Unapaswaje Kuitembea Hatua ya Mwisho ya Njia?

Umeme wa Mashariki | Unapaswaje Kuitembea Hatua ya Mwisho ya Njia?
Sasa mko kwenye hatua ya mwisho ya njia, na hii ni sehemu muhimu. Labda umevumilia mateso mengi kabisa, umefanya kazi nyingi, umetembea barabara nyingi, na umesikiliza mahubiri mengi, na haijakuwa rahisi kufika hadi sasa. Ikiwa huwezi kuvumilia mateso yaliyo mbele yako na kama unaendelea kama ulivyofanya zamani, basi huwezi kufanywa mkamilifu. Hii si ili kukutisha—huu ni ukweli. Baada ya Petro kupitia kazi ya Mungu kiasi fulani, alipata umaizi na ufahamu mwingi. Pia alielewa kiasi fulani cha kanuni ya huduma, na baadaye aliweza kujitolea kikamilifu kwa kile ambacho Yesu alimwaminia. Usafishaji mkubwa alioupokea mara nyingi ulikuwa kwa sababu katika mambo aliyoyafanya, alihisi kwamba alikuwa na deni kubwa kwa Mungu na kwamba hangeweza kamwe kumfidia, na aligundua kuwa wanadamu wamepotoka sana, kwa hivyo alikuwa na dhamiri yenye hatia. Yesu alikuwa amemwambia mambo mengi na wakati huo alikuwa na ufahamu mdogo tu.

Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Fuata Nyayo za Mungu

Umeme wa Mashariki  Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Fuata Nyayo za Mungu
Mwenyezi Mungu alisema, Sasa, mnatakiwa kufuatilia kugeuka kuwa watu wa Mungu, na mtaanza kuingia kote katika njia sahihi. Kuwa watu wa Mungu kuna maana ya kuingia katika Enzi ya Ufalme. Leo, mnaanza kwa urasimu kuingia katika mafunzo ya ufalme, na maisha yenu ya baadaye yatakoma kuwa goigoi na hobelahobela kama yalivyokuwa awali; maisha hayo ni yasiyoweza kufikia viwango vinayotakiwa na Mungu. Kama huhisi umuhimu wowote, basi hili huonyesha kwamba huna hamu ya kujiendeleza mwenyewe, kwamba ukimbizaji wako umekanganywa na kuchanganywa, na wewe ni usiyeweza kutimiza mapenzi ya Mungu.

11/03/2017

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Maneno kwa Vijana na Wazee

Umeme wa Mashariki,Wakristo,Roho Mtakatifu
Umeme wa Mashariki | Maneno kwa Vijana na Wazee

Mwenyezi Mungu alisema , Nimetekeleza kazi nyingi sana duniani na Nimetembea kati ya wanadamu kwa miaka mingi sana. Ilhali watu kwa nadra sana huwa na ufahamu wa sura Yangu na tabia Yangu, na watu wachache wanaweza kuelezea kikamilifu kazi Ninayofanya. Watu wanakosa mengi sana, daima wanakosa ufahamu wa kile Ninachokifanya, na mioyo yao daima iko tayari kana kwamba wanaogopa sana Nitawaleta katika hali nyingine na kisha kuwapuuza. Kwa hivyo, mtazamo wa watu Kwangu daima ni vuvuwaa pamoja na tahadhari kubwa sana. Hili ni kwa sababu watu wamekuja kwa wakati wa sasa bila kuelewa kazi Ninayofanya, na wao hasa hukanganywa na maneno ambayo Ninawaambia. Wao huyabeba maneno Yangu mikononi mwao, wasijue kama wanapaswa kujitahidi kuamini au kama wanapaswa kuyasahau kwa shaka. Hawajui kama wanapaswa kuyatia katika vitendo, au kama wanapaswa kungoja kuona. Hawajui kama wanapaswa kuachana na kila kitu na kisha kufuata kwa ujasiri, au kama wanapaswa kuendelea kuwa wa kirafiki na ulimwengu kama hapo awali. Ulimwengu wa ndani wa watu ni wenye utata sana, na wao ni wajanja sana.

Umeme wa Mashariki | Asili na Utambulisho wa Mwanadamu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Wakristo
Umeme wa Mashariki | Asili na Utambulisho wa Mwanadamu
Kwa kweli, hawajasikitika, na wamekuwa wakitazama kile ambacho kimefanywa kwa miaka elfu sita iliyopita mpaka leo, kwa kuwa Sikuwaacha. Badala yake, kwa sababu mababu zao walikula tunda kutoka kwa mti wa ujuzi wa mema na maovu lililotolewa na yule mwovu, waliniacha kwa ajili ya dhambi. Mema ni Yangu, wakati maovu ni ya yule mwovu ambaye hunihadaa kwa ajili ya dhambi. Mimi Siwalaumu mwanadamu, wala Siwaangamizi kwa ukatili au kuwatolea kuadibu kusiko na huruma, kwani uovu haukuwa wa wanadamu kiasili. Kwa hivyo ingawa wale Waisraeli walinipigilia misumari msalabani hadharani, wao, ambao wamekuwa wanamngoja Masiha na Yehova na kumtamani sana Mwokozi Yesu, hawajasahau ahadi Yangu.

Umeme wa Mashariki | Juu ya Hatima

Umeme wa Mashariki,Kristo,Wakristo
Umeme wa Mashariki | Juu ya Hatima

Mwenyezi MunguWakati wowote hatima inatajwa, muichukulie kwa uzito maalumu; nyinyi nyote ni mahususi hasa kuhusu jambo hili. Baadhi ya watu hawawezi kusubiri kumsujudia Mungu ili hatimaye kuwa na hatima nzuri. Naweza jishirikisha na hamu yenu, ambayo haihitaji kuonyeshwa katika maneno. Kabisa hamtaki miili yenu ianguke katika maafa, na hata zaidi, hamtaki kushuka katika adhabu ya muda mrefu hapo baadaye. Mnatarajia tu kuishi kwa uhuru zaidi na kwa urahisi. Hivyo mnahisi wasiwasi hasa wakati wowote hatima inatajwa, mkihofia kwa undani kwamba msipokuwa waangalifu vya kutosha, mnaweza kosea Mungu na kuwa chini ya adhabu inayostahili. Hamjasita kufanya maafikiano kwa ajili ya hatima zenu, na wengi wenu ambao wakati mmoja walikuwa wa kuzunguka na wapuuzi hata kwa ghafla wamegeuka hususa wapole na wa dhati; unyofu wenu hata una mzizimo. Pasipo kutilia maanani, nyinyi nyote mna mioyo minyoofu, na kutoka mwanzo hadi mwisho mmejifungua wazi Kwangu bila kuficha siri zozote katika mioyo yenu, yawe lawama, udanganyifu, au ibada. Kwa jumla, "mmekiri" kwa uwazi Kwangu yale mambo muhimu katika pahali pa siri yenye kina kwenu. Mambo kama yalivyo, Sijawahi kuepuka aidha ya mambo kama haya, kwa sababu yamekuwa ya kawaida Kwangu. 

Kuijua Kazi ya Mungu Leo

Mwenyezi Mungu alisema, Kuijua kazi ya Mungu katika nyakati hizi, kwa sehemu kubwa, ni kumjua Mungu katika mwili wa siku za mwisho, kile ambacho ni huduma Yake kuu, na kile ambacho Amekuja kufanya duniani. Hapo mwanzoni Nimesema katika maneno Yangu kwamba Mungu Amekuja duniani (wakati wa siku za mwisho) ili kuweka mfano kabla Hajaondoka. Ni kwa jinsi gani Mungu Ameuweka mfano huu? Kwa kuzungumza maneno, kwa kufanya kazi na kuzungumza katika nchi nzima. Hii ni kazi ya Mungu wakati wa siku za mwisho; Anazungumza tu ili dunia iwe ulimwengu wa maneno, ili kila mtu awe amepewa na kutiwa nuru maneno Yake, na ili roho ya mwanadamu iamshwe na aweze kuona vizuri kuhusu maono yake.

11/02/2017

Umeme wa Mashariki | Hakuna Aliye wa Mwili Anayeweza Kuepuka Siku Ya Ghadhabu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mungu
Umeme wa Mashariki | Hakuna Aliye wa Mwili Anayeweza Kuepuka Siku Ya Ghadhabu
Leo, Nawaonya hivi kwa ajili ya kusalimika kwenu wenyewe, ili kazi Yangu iendelee vizuri, na ili kazi Yangu ya uzinduzi kote ulimwenguni iweze kufanyika kwa njia inayofaa na kikamilifu, ikifichua maneno Yangu, mamlaka, adhama na hukumu kwa watu wa nchi zote na mataifa. Kazi Ninayoifanya miongoni mwenu ni mwanzo wa kazi Yangu katika ulimwengu wote. Ingawa sasa ni siku za mwisho tayari, jua kwamba "siku za mwisho" ni jina tu la enzi: Kama tu vile Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema, linaashiria enzi, na linaashiria enzi nzima, badala ya mwisho wa miaka au miezi michache. Hata hivyo siku za mwisho ni tofauti kabisa na Enzi ya Neema na Enzi ya Sheria. Kazi ya siku za mwisho haifanyiki katika taifa la Israeli, lakini kati ya mataifa; ni ushindi mbele ya kiti Changu cha enzi cha watu kutoka mataifa yote na makabila yote nje ya Israeli, ili utukufu Wangu katika ulimwengu wote uweze kujaza dunia nzima.

11/01/2017

Swahili Christian Movie | Nyendo za Mateso ya Kidini | "Saa ya Giza Kabla ya Mapambazuko"



    Tangu kilipokuja mamlakani katika China Bara mnamo mwaka wa 1949, Chama Cha Kikomunisti cha China kimekuwa hakikomi katika mateso yake kwa imani ya kidini. Kwa wayowayo kimewashika na kuwaua Wakristo, kuwafukuza na kuwadhulumu wamishonari wanaofanya kazi nchini China, wakachukua ngawira na kuchoma nakala nyingi za Biblia, wakafunga kabisa na kubomoa majengo ya kanisa, na bila mafanikio wakajaribu kukomesha makanisa yote ya nyumbani. Filamu hii ya hali halisi inaelezea uzoefu wa kweli wa Mkristo Mchina, Yang Huizhia, ambaye alikamatwa na serikali CCP, akateswa, na kufa kutokana na kuteswa kwake kwa sababu ya imani yake kwa Mungu. Baada ya Yang Huizhi kufa, serikali ya CCP kwa uongo ilidai kuwa kifo chake kilikuwa kimetokana na mshtuko wa moyo. Familia yake ilitaka kutafuta haki kwa ajili yake, lakini hatimaye walishtuka hadi kutulia kwa sababu ya vitisho vya CCP.

Umeme wa Mashariki | Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Kristo,Roho Mtakatifu
Umeme wa Mashariki | Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Kwa nini unamwamini Mungu? Watu wengi wanafadhaishwa na swali hili. Siku zote wana mitazamo tofauti kuhusu Mungu wa vitendo na Mungu wa mbinguni, jambo linaloonyesha kwamba wanamwamini Mungu sio ili wamtii, bali kupata manufaa fulani, au kuepuka mateso ya janga. Wakati huo tu ndipo wanakuwa watii kwa kiasi fulani, lakini utii wao ni wa masharti, ni kwa ajili ya matarajio yao wenyewe, na kushinikiziwa. Hivyo: kwa nini unamwamini Mungu? Ikiwa ni kwa ajili ya matarajio yako tu, na majaliwa yako, basi ni bora zaidi usingeamini. Imani kama hii ni kujidanganya, kujihakikishia, na kujishukuru. Kama imani yako haijajengwa katika msingi wa utii kwa Mungu, basi hatimaye utaadhibiwa kwa kumpinga Mungu. Wale wote ambao hawatafuti utii kwa Mungu kwa imani yao wanampinga Mungu. Mungu anaomba kwamba watu watafute ukweli, kwamba wawe na kiu cha neno la Mungu, na wanakula na kunywa maneno ya Mungu, na kuyaweka katika matendo, ili waweze kupata utii kwa Mungu.