1/31/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 6

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu, Sura ya 6

    Binadamu wanapigwa bumbuazi kwa sababu ya matamshi ya Mungu wanapotambua kwamba Mungu amefanya kitendo kikubwa katika ulimwengu wa kiroho, kitu ambacho mwanadamu hawezi na ambacho Mungu Mwenyewe pekee ndiye Anaweza kufanikisha. Kwa sababu hii, Mungu mara tena anawasilisha maneno ya huruma kwa wanadamu. Mioyo ya watu inapojaa ukinzani, ikishangaa: “Mungu ni Mungu asiye na huruma au upendo, lakini badala yake Mungu aliyejitolea kuwaangusha binadamu; kwa hiyo mbona Atuonyeshe huruma? Yawezekana kwamba Mungu kwa mara nyingine amehamia kwa utaratibu?”

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Onyo kwa Wale Wasioweka Ukweli katika Vitendo

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,siku za mwisho

Matamshi ya Mwenyezi Mungu, Onyo kwa Wale Wasioweka Ukweli Katika Vitendo

Wale miongoni mwa ndugu na dada ambao daima hueneza ubaya wao ni vibaraka wa Shetani na hulivuruga kanisa. Watu hawa lazima siku moja wafukuzwe na kuondolewa. Katika Imani yao kwa Mungu, ikiwa watu hawana moyo wa kumcha Mungu ndani yao, ikiwa hawana moyo ambao ni mtiifu kwa Mungu, basi hawatashindwa tu kufanya kazi yoyote ya Mungu, lakini kinyume na hayo watakuwa watu wanaovuruga kazi ya Mungu na wanaomuasi Mungu. Wakati mtu anayeamini Mungu hamtii Mungu ama kumcha Mungu lakini badala yake anamwasi Yeye, basi hii ndiyo aibu kuu zaidi kwa muumini. Ikiwa usemi na mwenendo wa muumini daima havina mpango na bila kizuizi kama asiyeamini, basi huyu muumini ni mwovu zaidi kumpiku asiyeamini;

1/30/2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu, Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)

Kwa kipindi hiki chote, tumezungumza juu ya mambo mengi yanayohusiana na kumjua Mungu na hivi karibuni tulizungumza kuhusu kitu fulani muhimu sana juu ya mada hii: Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote. Wakati uliopita tulizungumza juu ya vipengele vichache vya mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu aliyatengeneza kwa ajili ya binadamu, vilevile Mungu kuandaa kila aina ya riziki ya lazima kwa ajili ya watu katika maisha yao. Kwa kweli, kile ambacho Mungu anafanya si tu kuandaa mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa watu wala si tu kuandaa riziki yao ya kila siku, bali ni kuandaa vipengele mbalimbali vya kazi kubwa ya ajabu na ya lazima kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa watu na kwa ajili ya maisha ya binadamu. Haya yote ni matendo ya Mungu.

Sura ya 88. Kulipa Gharama ili Kupata Ukweli ni Muhimu Sana

   Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kanisa
    Mwenyezi Mungu alisema, Sio rahisi kwa vijana kuendeleza kazi; wengi wao hawadumishi mwendo. Ni lazima moyo wako uwe mtulivu, lazima uweze kudumisha mwendo na uwe tayari kutumia muda kwake. Wengine hujiburudisha au kuwachezea wengine, lakini wewe unasema, "Siwezi, sina wakati. Biashara yangu ina shughuli sana. Nendeni mkajiburudishe. Ni lazima niipange biashara yangu.” Unaweza tu kufaulu kwa kushughulika na kujitolea kwa biashara yako. Kwa kweli, hukosi nguvu sasa, wala hukosi ujuzi wa kitaalamu. Ili kuboresha hali yako ya kitaaluma, unaweza kufanya baadhi ya utafiti na ujifunze. Ni yapi zaidi, una msingi huu, akili hii, ujuzi huu maalum; unachokosa kwa kweli ni kutumia wakati na nguvu.

1/29/2018

Christian Music Video Swahili “Hadithi ya Xiaozhen”(2): Kupigania Dhahabu



Christian Music Video Swahili “Hadithi ya Xiaozhen”(2): Kupigania Dhahabu

Xiaozhen alipopata kipande kikubwa cha dhahabu, aliwaita marafiki wake ili wagawane. Kile ambacho hakutambua ni kwamba mara tu watu wanapoona dhahabu, asili nzuri na mbaya ya mwanadamu hujiweka wazi …

     Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji.

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko la Thelathini na Moja

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Matamshi ya Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu, Tamko la Thelathini na Moja

Sijawahi kuwa na nafasi ndani ya mioyo ya watu. Ninapowatafuta watu kweli, wao hufunga na kubana macho yao na kupuuza matendo Yangu, kana kwamba yote Nifanyayo ni jaribio la kuwafurahisha, kutokana na hilo wao daima huchukizwa na matendo Yangu. Ni kana kwamba Nakosa kujitambua kokote: Mimi kila mara hujiringa mbele ya mwanadamu, kusababisha kughadhibishwa ndani ya mwanadamu, ambaye ni "mwadilifu na mwenye haki." Lakini chini ya hali mbaya kama hizo, Mimi huvumilia, na kuendeleza kazi Yangu.

1/28/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | 73. Kwa Nini Nimetembea Njia ya Mafarisayo?

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Wakristo
Wakristo,Ushahidi
Kanisa la Mwenyezi Mungu | 73. Kwa Nini Nimetembea Njia ya Mafarisayo?
Suxing Mkoa wa Shanxi
Mimi ni mtu mwenye kiburi na majivuno, na cheo kimekuwa udhaifu wangu. Kwa miaka mingi, nimefungwa na sifa na cheo na sijaweza kujiweka huru kutoka kwazo. Mara kwa mara nimepandishwa cheo na kubadilishwa na mtu mwingine; nimekuwa na vizuizi vingi katika cheo changu na nimekumbwa na matuta mengi njiani. Baada ya miaka mingi ya kushughulikiwa na kusafishwa, nilihisi kwamba sikuwa nachukulia cheo changu kwa uzito. Sikutaka kuwa kama nilivyokuwa katika nyakati zilizopita nikifikiri kwamba mradi nilikuwa kiongozi ningeweza kukamilishwa na Mungu na kwamba iwapo sikuwa kiongozi, basi sikuwa na matumaini.

Sura ya 31. Jinsi ya Kufahamu Uenyezi na Utendaji wa Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu
Mwenyezi Mungu alisema, Kitu hiki kinachoitwa mwanadamu kina uwezo wa kumsaliti Mungu, kwa hivyo unaweza kujua nini kutoka kwa hili? Baadhi ya watu huuliza: "Mungu alimuumba mwanadamu kwa hivyo Mungu hawezi kumzuia mwanadamu kumsaliti Yeye? Ni kwa nini mwanadamu bado ana uwezo wa kumsaliti Mungu? Je, Mungu si mwenyezi?" Hili ni tatizo, sio? Ni tatizo gani unaloweza kuona hapa katika suala hili? Mungu ana upande wa vitendo, lakini pia Ana upande wa uenyezi. Mwanadamu asingekuwa amepotoshwa na Shetani, bado tu angeweza kumsaliti Mungu. Kitu hiki kinachoitwa mwanadamu hakina hiari ya nafsi yake mwenyewe: Jinsi wanatakiwa kumwabudu Mungu, jinsi wanapaswa kumkana Shetani, kutoshirikiana na uovu wake. Wanapaswa kumtii Mungu, Mungu ana ukweli, uzima na njia, na Mungu hakosewi. Mambo haya hayako ndani ya wanadamu, wala wanadamu hawamiliki mambo hayo ambayo yangefahamu asili ya Shetani.

1/27/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu, Kusudi la Kuwasimamia Binadamu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,Injili

Matamshi ya Mwenyezi Mungu, Kusudi la Kuwasimamia Binadamu

    Ikiwa watu wanaweza kweli kuielewa kikamilifu njia sahihi ya maisha ya binadamu na vilevile kusudi la usimamizi wa Mungu wa binadamu, wasingeshikilia mategemeo yao ya baadaye na majaliwa yao binafsi kama hazina mioyoni mwao. Wasingetamani tena kuwatumikia wazazi wao ambao ni wabaya zaidi kuliko nguruwe na mbwa. Je, mategemeo ya baadaye na majaliwa ya mwanadamu si kabisa kile kinachoitwa nyakati za sasa "wazazi" wa Petro? Yamekuwa kama tu mwili na damu ya mwanadamu.

Fumbo la Kupata Mwili (1)

 Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu
Mwenyezi Mungu alisema, Katika Enzi ya Neema, Yohana alimwandalia Yesu njia. Hangeweza kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe ila alitimiza tu kazi ya mwanadamu. Ingawa Yohana alikuwa mtangulizi wa Bwana; hangeweza kumwakilisha Mungu; alikuwa tu binadamu aliyetumiwa na Roho Mtakatifu. Kufuatia ubatizo wa Yesu, “Roho Mtakatifu alimshukia Yeye kwa mfano wa njiwa.” Kisha Akaanza kazi Yake, hivyo, Alianza kufanya huduma ya Kristo. Hiyo ndiyo maana Alichukua utambulisho wa Mungu, kwa sababu Alitoka Kwa Mungu. Haijalishi aina ya imani Yake kabla ya hii—labda wakati mwingine ilikuwa dhaifu, au wakati mwingine ilikuwa na nguvu—hayo ndiyo yalikuwa maisha Yake ya kawaida ya binadamu kabla Afanye huduma Yake.

1/26/2018

007 Papa hapa, Hivi Sasa, Tuungane Pamoja | Umeme wa Mashariki

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,nyimbo

Umeme wa Mashariki | Wimbo wa Uzoefu wa Maisha

Papa hapa, Hivi Sasa, Tuungane Pamoja


I
Kwa kupendana, sisi ni familia. Ah … ah …
Papa hapa, hivi sasa, tunaungana;
kusanyiko la watu wampendao Mungu.
Bila upendeleo, tukishikizwa kwa karibu,
furaha na utamu vikijaza nyoyo zetu.
Jana tuliacha majuto na hatia; leo tunaelewana,
tunaishi katika upendo wa Mungu.

1/25/2018

Sura ya 28. Bila Ukweli Ni Rahisi Kumkosea Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Wakristo
Mwenyezi Mungu alisema,Kutoa kwenu "muhtasari kuhusu ukweli" hakufanywi ili kuwawezesha watu kupata maisha au kupata mabadiliko katika tabia zao kutoka kwa ukweli. Badala yake, kunafanywa ili watu waweze kuwa weledi wa maarifa na mafundisho fulani kutoka kwa ukweli. Wao huonekana kana kwamba wanaelewa lengo lililokusudiwa katika kazi ya Mungu, wakati kwa kweli wamekuwa weledi wa baadhi ya maneno ya mafundisho tu. Hawaelewi maana iliyokusudiwa ya ukweli, na si tofauti na kusomea theolojia au kusoma Biblia.

Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu
    Mwenyezi Mungu alisema, Watu wote wanahitaji kuelewa kusudio la kazi Yangu ulimwenguni, yaani, lengo la mwisho la kazi Yangu na ni kiwango kipi ambacho lazima Nitimize katika kazi hii kabla inaweza kukamilika. Kama watu, wanaotembea na Mimi hadi leo, hawaelewi kazi Yangu inahusu nini, basi hawajakuwa wakitembea na Mimi bure? Watu wanaonifuata Mimi wanafaa kujua mapenzi Yangu. Nimekuwa nikifanya kazi ulimwenguni kwa maelfu ya miaka, na ningali nafanya hivyo sasa. Ingawaje kunavyo vipengele vingi hasa vilivyojumuishwa katika kazi Yangu, kusudio lake linabakia lilelile. Kwa mfano, ingawaje nimejazwa na hukumu na adabu kwake binadamu, bado ni kwa ajili ya kumwokoa binadamu, ili niweze kueneza kwa njia bora zaidi injili Yangu na kupanua zaidi kazi Yangu miongoni mwa Mataifa baada ya binadamu kufanywa kuwa kamili.