Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Mwendelezo-wa-Neno-Laonekana-katika-Mwili. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Mwendelezo-wa-Neno-Laonekana-katika-Mwili. Onyesha machapisho yote

3/23/2018

Umeme wa Mashariki | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IIπŸ“–πŸ“š

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Wokovu

  Umeme wa Mashariki | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II

  (II) Ubinadamu Hupata Kibali cha Huruma na Uvumilivu wa Mungu Kupitia kwa Toba ya dhati

🌼🌼🌼🌼🌼*************🌻🌻🌻🌻*************🌺🌺🌺🌺🌺
      Kinachofuata ni hadithi ya biblia ya “Wokovu wa Mungu kwa Ninawi.”

    (Yona 1:1-2) Basi neno la BWANA lilimjia Yona mwana wa Amitai, likisema, Inuka, uende Ninawi, mji ule mkubwa, upige kelele juu yake; kwa maana uovu wao umepanda juu mbele zangu.
    (Yona 3) Neno la BWANA likamjia Yona mara ya pili, likisema, Inuka, uende Ninawi, mji ule mkubwa, uhubiri habari Ninayokuamuru.Basi Yona akainuka, akaenda Ninawi, kulingana na amri ya BWANA.

3/22/2018

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu
    Mwenyezi Mungu alisema, Kwenye mkutano wetu wa mwisho tuliweza kuzungumzia mada muhimu sana. Je, wakumbuka mada hiyo ilikuwa kuhusu nini? Hebu Niirudie. Mada ya ushirika wetu wa mwisho ilikuwa: Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe. Je, mada hii ni muhimu kwako? Ni sehemu gani katika mada hii ni muhimu kwako? Kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, au Mungu Mwenyewe? Ni sehemu ipi inakuvutia zaidi? Ni sehemu ipi unayotaka kusikiliza kuhusu zaidi? Najua ni vigumu kwako wewe kulijibu swali hilo, kwa sababu tabia ya Mungu inaweza kuonekana katika kila kipengele cha kazi Yake, na tabia Yake inafichuliwa katika kazi Yake siku zote na pahali pote, na, kutokana na hayo, inawakilisha Mungu Mwenyewe; kwenye mpango wa usimamizi wa ujumla wa Mungu, kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe vyote hivi haviwezi kutenganishwa.

3/12/2018

πŸ“–πŸ“–Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Tabia ya Haki ya Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Kwa vile sasa mumesikiliza kikao cha ushirika uliopita kuhusu mamlaka ya Mungu, Ninao ujasiri kwamba mumejihami vilivyo na mseto wa maneno kuhusu suala hili. Kiwango unachoweza kukubali, kushika, na kuelewa vyote hivi vinategemea na jitihada zipi utakazotumia. Ni tumaini Langu kwamba utaweza kutazamia suala hili kwa dhati; kwa vyovyote vile hufai kulishughulikia shingo-upande! Sasa, je, kujua mamlaka ya Mungu ni sawa na kujua Mungu kwa uzima wake? Mtu anaweza kusema kwamba kujua mamlaka ya Mungu ndiyo mwanzo wa kumjua Mungu mwenyewe kwa upekee wake, na mtu anaweza kusema pia kwamba kuyajua mamlaka ya Mungu kunamaanisha kwamba mtu tayari ameingia kwenye lango kuu la kujua hali halisi ya ule upekee wa Mungu Mwenyewe.

3/11/2018

Sura ya 53. Kuelewa Visawe na Tofauti katika Asili ya Binadamu

Umeme wa Mashariki | Sura ya 53. Kuelewa Visawe na Tofauti katika Asili ya Binadamu

Je, mnaona kwa dhahiri njia ya imani yenu kwa Mungu na njia yenu ya kufuata ukweli? Imani katika Mungu kweli ni nini? Je, mmetosheka baada ya kupitia shida kidogo? Watu wengine hufikiri kwamba baada ya kupitia hukumu na kuadibiwa, kupogolewa na ushughulikiwaji au baada ya kufichua hali yao ya kweli, wamemaliza na matokeo yao yameonekana. Wengi wa watu hawawezi kuona suala hili kwa dhahiri, na wao wote husimamishwa hapo, bila kujua jinsi ya kuitembea njia iliyo mbele. Kwa ujumla, wasipopitia ushughulikiwaji na upogolewaji au hawana vikwazo vyovyote, watahisi kama kutafuta ukweli wakati wakiamini katika Mungu, na watahisi kwamba wanapaswa kuyatosheleza mapenzi ya Mungu.

3/10/2018

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe IπŸ“–πŸ˜ŠπŸ˜‡

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Leo tunawasiliana kuhusu mada muhimu. Hii ni mada ambayo imezungumziwa tangu kuanza kwa kazi ya Mungu mpaka sasa, na inayo umuhimu mkuu kwa kila mtu. Kwa maneno mengine, hili ni suala ambalo kila mmoja atakutana nalo kwenye mchakato wote wa kusadiki kwake katika Mungu na suala ambalo lazima lizungumziwe. Ni suala muhimu, lisiloepukika ambalo mwanadamu hawezi kujitenganisha nalo. Tukizungumzia umuhimu, ni nini kitu muhimu zaidi kwa kila muumini katika Mungu? Baadhi ya watu wanafikiri kwamba kitu muhimu zaidi ni kuyaelewa mapenzi ya Mungu; baadhi wanasadiki ni muhimu zaidi kula na kunywa maneno ya Mungu; baadhi wanahisi kitu muhimu zaidi ni kujijua wenyewe;

3/08/2018

🀲😊Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VπŸ“–πŸ‘πŸ˜‡

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Neno la Mwenyezi Mungu, Utakatifu wa Mungu (II)

Habari za jioni kila mtu! (Habari ya jioni Mwenyezi Mungu!) Leo, kaka na dada, hebu tuimbe wimbo. Tafuta mmoja ambao mnapenda na ambao mmeimba mara nyingi kabla. (Tungependa kuimba wimbo wa neno la Mungu “Upendo Safi Bila dosari.”)
Kiitikio: “Upendo” unarejelea hisia safi bila dosari, ambapo mnatumia mioyo yenu kupenda, kuhisi, na kuwa wa kufikiri. Katika upendo hakuna masharti, hakuna vizuizi, na hakuna umbali. Katika upendo hakuna tuhuma, hakuna udanganyifu, hakuna mpango, na hakuna ujanja. Katika upendo hakuna chaguo na hakuna chochote kichafu.

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII

Kumjua-Mungu, Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki
(II)Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote
Leo Nitashiriki nawe mada mpya. Mada itakuwa ni nini? Kichwa cha mada kitakuwa "Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote." Je, hii siyo mada kubwa kidogo kuweza kuijadili? Je, inaonekana kama kitu ambacho kidogo hakiwezi kufikika? Mungu kuwa chanzo cha uhai kwa vitu vyote inaweza kuonekana ni mada ambayo watu wanahisi kutohusika nayo, lakini wote wanaomfuata Mungu wanapaswa kuielewa. Hii ni kwa sababu mada hii haihusiani kwa kuchanganulika na kila mtu anayemjua Mungu, kuweza kumridhisha na kumheshimu. Hivyo, mada hii inapaswa kuwasilishwa. Baadhi ya watu wanaweza kuwa na uelewa wa msingi wa mada hii, au pengine baadhi ya watu wanaitambua.

3/05/2018

πŸ“–πŸ“–Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe IIIπŸ‘πŸ˜‡

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,Injili
9. Yesu Atenda Miujiza.
1) Yesu Awalisha Watu Elfu Tano.
(Yohana 6:8-13) Mmoja wa wanafunzi wake, Andrea, nduguye Simoni Petro, akamwambia, Yupo mvulana hapa, aliye na mikate mitano ya shayiri na samaki wawili: lakini hivi ni nini kwa watu wengi kama hawa? Naye Yesu akasema, Wafanye watu hawa waketi chini. Na mahali pale palikuwa na majani mengi. Basi wale wanaume wakaketi, wapatao elfu tano kwa jumla. Kisha Yesu akaichukua ile mikate; na baada ya kutoa shukrani, akawagawia wafuasi wake, nao wafuasi wake wakawagawia walioketi; na vile vile wale samaki kwa kiasi walichoweza. Waliposhiba, aliwaambia wanafunzi wake, Kusanyeni vipande vilivyobaki, ili chochote kisipotee. Basi wakavikusanya, wakajaza vikapu kumi na viwili kwa vipande vya mikate mitano ya shayiri vilivyobaki baada ya wale watu kula.

2/27/2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II)

Mwenyezi Mungu alisema, Tuendelee na mada ya mawasiliano ya wakati uliopita. Je, mnaweza kukumbuka ni mada gani tuliwasiliana wakati uliopita? (Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote.) Je, “Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote” ni mada mnayohisi ikiwa mbali sana nanyi? Mtu fulani anaweza kuniambia wazo kuu la mada hii tuliyowasiliana wakati uliopita? (Kupitia kwa uumbaji wa Mungu wa vitu vyote, ninaona kwamba Mungu hulea vitu vyote na hulea wanadamu. Katika siku zilizopita, kila mara nilifikiria kwamba Mungu anapompa mwanadamu, Anawapa tu watu Wake waliochaguliwa neno Lake, lakini kamwe sikuona, kupitia kwa sheria za vitu vyote, kwamba Mungu anawalea wanadamu.

2/18/2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Neema

2. Mungu anaweka Uwiano Kati ya Vitu Vyote ili Kumpatia Binadamu Mazingira Imara kwa ajili ya Kuendelea Kuishi

Tumemaliza kusema juu ya jinsi ambavyo Mungu anatawala sheria za vitu vyote vilevile jinsi ambavyo Anawakimu na kuwalea binadamu wote kupitia sheria Zake kwa ajili ya viumbe vyote ndani ya sheria hizo. Hiki ni kipengele kimoja. Kinachofuata, tutazungumza juu ya kipengele kingine, ambacho ni njia moja ambayo Mungu ana udhibiti wa kila kitu. Hivi ndivyo, baada ya kuumba vitu vyote, Akaweka uwiano wa uhusiano kati yao. Hii pia ni mada kubwa sana kwenu. Kuweka uwiano wa uhusiano kati ya vitu vyote—je, hiki ni kitu ambacho watu wanaweza kufanya? Binadamu wenyewe hawawezi. Watu wanaweza tu kuharibu.

2/11/2018

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Yesu
    Mwenyezi Mungu alisema, Vikao hivi kadhaa vya ushirika vimekuwa na athari kubwa katika kila mmoja wa watu. Kwa sasa, watu wanaweza hatimaye kuhisi uwepo wa kweli wa Mungu na kwamba Mungu kwa hakika yuko karibu sana na wao. Ingawa watu wameamini katika Mungu kwa miaka mingi, hawajawahi kuelewa kwa kweli mawazo na fikira Zake kama wanavyozielewa sasa, wala hawajawahi kupata kwa kweli uzoefu wa matendo Yake halisi kama walio nao kwa sasa.
Kama ni maarifa au matendo halisi, wengi wamejifunza kitu kipya na kutimiza ufahamu wa juu zaidi, na wametambua kosa lililopo kwenye ufuatiliaji wao wa kale, wametambua hali yao waliyopitia ya juujuu na kwamba mambo mengi sana hayaambatani na mapenzi ya Mungu, na wametambua kwamba kile ambacho binadamu amepungukiwa nacho zaidi ni maarifa ya tabia ya Mungu.

2/06/2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kumjua Mungu,
Mamlaka ya Mungu (I)

Kwenye Siku ya Nne, Misimu, Siku, na Miaka ya Mwanadamu Iliumbika Huku Mungu Akionyesha Mamlaka Yake kwa Mara Nyingine Tena

Mwenyezi Mungu alisema, Muumba alitumia matamshi Yake kutimiza mpango Wake, na kwa njia hii Alipitisha siku tatu zake za kwanza kwenye mpango Wake. Kwenye siku hizi tatu, Mungu hakuonekana kushughulika kila pahali, au kujichosha Yeye Mwenyewe; kinyume cha mambo ni kwamba, Alikuwa na siku tatu za kwanza nzuri katika mpango Wake na Alitimiza utekelezaji mkubwa wa mabadiliko makubwa ya ulimwengu. Ulimwengu mpya kabisa ulijitokeza mbele ya macho Yake, na, kipande kwa kipande, picha nzuri na ya kupendeza ambayo ilikuwa imefichwa ndani ya fikira Zake ilikuwa tayari imefichuliwa kwa matamshi ya Mungu.

1/30/2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu, Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)

Kwa kipindi hiki chote, tumezungumza juu ya mambo mengi yanayohusiana na kumjua Mungu na hivi karibuni tulizungumza kuhusu kitu fulani muhimu sana juu ya mada hii: Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote. Wakati uliopita tulizungumza juu ya vipengele vichache vya mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu aliyatengeneza kwa ajili ya binadamu, vilevile Mungu kuandaa kila aina ya riziki ya lazima kwa ajili ya watu katika maisha yao. Kwa kweli, kile ambacho Mungu anafanya si tu kuandaa mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa watu wala si tu kuandaa riziki yao ya kila siku, bali ni kuandaa vipengele mbalimbali vya kazi kubwa ya ajabu na ya lazima kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa watu na kwa ajili ya maisha ya binadamu. Haya yote ni matendo ya Mungu.

1/24/2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

 Matamshi ya Mwenyezi Mungu,Mamlaka ya Mungu (I)

Vikao vyangu mbalimbali vya ushirika vilivyopita vilikuwa vinahusu kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe. Baada ya kuvisikiliza vikao hivi vya ushirika, je, unahisi kuwa umefaidi na kupata ufahamu na maarifa kuhusu tabia ya Mungu? Ufahamu wako na maarifa ni mkubwa kiwango gani? Je, unaweza kuweka nambari katika kiwango hicho? Je, vikao hivi vya ushirika vilikupa ufahamu wa kina kuhusu Mungu? Inaweza kusemwa ufahamu huu ni maarifa ya kweli ya Mungu? Inaweza kusemwa kwamba maarifa na ufahamu huu wa Mungu ni maarifa ya hali halisi nzima ya Mungu, na kila kitu Anacho na alicho? La, bila shaka haiwezi kusemwa hivyo!

12/28/2017

Matamshi ya Mwenyezi Mungu,Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki
maneno ya Mungu,Kazi ya Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu,Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV

3. Mazungumzo kati ya Shetani na Yehova Mungu
(Ayu 1:6-11) Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za BWANA, Shetani naye akaenda kati yao. BWANA akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu BWANA, na kusema, Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo. Kisha BWANA akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu. Ndipo Shetani akamjibu BWANA, na kusema, Je! Huyo Ayubu yuamcha BWANA bure? Wewe hukumzingira kwa ukigo pande zote, pamoja na nyumba yake, na vitu vyote alivyo navyo? Kazi za mikono yake umezibarikia, nayo mali yake imeongezeka katika nchi.