Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Neno-la-Mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Neno-la-Mungu. Onyesha machapisho yote

9/14/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko la Thelathini na Tisa

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko la Thelathini na Tisa

Kila siku Natembea juu ya ulimwengu, Nikiangalia kwa makini vitu vyote vilivyoumbwa kwa mkono Wangu. Juu ya mbingu ni mahali Pangu pa pumziko, na chini yake ni nchi ambayo Natembea. Natawala kila kitu miongoni mwa vyote vilivyoko, Naamuru kila kitu miongoni mwa vitu vyote, Nikisababisha vyote vilivyoko kufuata hali halisi ya maisha na kutii amri ya asili.

9/10/2018

Imani Katika Mungu Haipasi Kuwa kwa ajili ya Kutafuta Amani na Baraka Pekee

Sura ya 7 Vipengele Vingine vya Ukweli Ambavyo Unafaa Kueleweka Katika Imani Yako kwa Mungu

5. Imani Katika Mungu Haipasi Kuwa kwa ajili ya Kutafuta Amani na Baraka Pekee

Maneno Husika ya Mungu:
Ni kitu gani ambacho mwanadamu amepokea tangu alipomwamini Mungu mara ya kwanza? Umejua kitu gani kumhusu Mungu? Umebadilika kiasi gani kwa sababu ya imani yako kwa Mungu? Sasa mnajua nyote ya kwamba imani ya mwanadamu katika Mungu si kwa ajili ya wokovu wa roho na ustawi wa mwili tu, wala si kuimarisha maisha yake kwa njia ya upendo wa Mungu, na kadhalika. Kama ilivyo sasa, kama unampenda Mungu kwa ajili ya ustawi wa mwili au furaha ya muda, basi hata kama, mwishoni, upendo wako kwa Mungu utafikia kilele chake na wewe hutaulizia kitu chochote, upendo huu unaoutafuta ni upendo mchafu na haumpendezi Mungu. 

7/31/2018

Unahitaji Kusadiki Vipi Mungu Ili Kuweza Kuokolewa na Kufanywa Kuwa Mtimilifu?

Sura ya 4 Ukweli wa Kazi ya Mungu ya Siku za Mwisho

5. Unahitaji Kusadiki Vipi Mungu Ili Kuweza Kuokolewa na Kufanywa Kuwa Mtimilifu?

Maneno Husika ya Mungu:
Kufanya muhtasari wa kuishika njia ya Petro katika kumwamini Mungu, ni kuishika njia ya kufuatilia ukweli, ambayo pia ni njia ya kujijua na kubadilisha tabia ya mtu. Ni kwa kuishika tu njia ya Petro ndio mtu atakuwa anashika njia ya kukamilishwa na Mungu. Mtu lazima aelewe hasa jinsi ya kuishika njia ya Petro na jinsi ya kuiweka katika vitendo. Kwanza, mtu lazima aweke kando madhumuni yake mwenyewe, shughuli zisizofaa, na hata familia yake na vitu vyote vya mwili wake. Lazima ajitolee kwa moyo wote, yaani, ajitolee kabisa kwa neno la Mungu, azingatie kula na kunywa neno la Mungu, azingatie kutafuta ukweli, utafutaji wa nia ya Mungu katika maneno Yake, na ajaribu kufahamu mapenzi ya Mungu katika kila kitu.

7/20/2018

Nilijifunza Kufanya Kazi na Wengine

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Wakristo
Liu Heng    Mkoa wa Jiangxi
Kupitia neema na kuinuliwa kwa Mungu, nilichukua jukumu la kuwa kiongozi wa kanisa. Wakati huo, nilikuwa na shauku mno na niliweka azimio mbele ya Mungu: Bila kujali kinachonikabili, sitayatelekeza majukumu yangu. Nitafanya kazi vizuri na yule dada mwingine na nitakuwa mtu anayetafuta ukweli. Lakini nilikuwa nimeamua tu, na sikujua jinsi ya kuingia katika uhalisi wa uhusiano wa kufanya kazi kwa mpangilio wa kuridhisha.

7/19/2018

Filosofia ya Shetani Inanasa na Kuharibu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, kanisa
Wu You    Mji wa Hechi, Mkoa wa Guangxi
Wakati fulani uliopita, kanisa lilinipangia kuishi na familia mwenyeji kwa sababu za kazi. Wakati nilipofanya ushirika kwanza na ndugu wa kiume na wa kike wa familia hii mwenyeji, walisema, "Tunaogopa sana kuomba katika ushirika. Tunajua cha kusema tunaposali peke yetu, lakini linapokuja suala la kuomba wakati wa ushirika, hatujui hasa cha kusema."

7/09/2018

Zawadi ya Kupendeza Zaidi Ambayo Mungu Amenipa

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kanisa
Yixin    Jiji la Shijiazhuang, Mkoa wa Hebei
Kabla, ningewasikia mara kwa mara ndugu zangu wa kiume na wa kike wakisema, "Kila kitu ambacho Mungu hufanya ni kwa ajili ya matokeo mazuri; ndiyo yote wanayohitaji watu." Nilikubali hili na kukubaliana nalo, lakini sikuwa na ufahamu wowote kupitia uzoefu wangu mwenyewe. Baadaye nilipata ufahamu kiasi kwa njia ya mazingira ambayo Mungu aliniumbia.

7/07/2018

Nilipitia Wokovu wa Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, wakristo
Cheng Hao    Mji wa Yongzhou, Mkoa wa Hunan
Kwa neema ya Mungu, mimi na mke wangu tulipandishwa vyeo hadi kwa timu ya injili ya pili ili kutimiza wajibu wetu. Muda mfupi uliopita, mke wangu alipandishwa cheo kuwa mkurugenzi wa timu, huku mimi, kutokana na kiburi changu mwenyewe na utukutu wangu, nilipoteza kazi ya Roho Mtakatifu na kupelekwa nyumbani kutafakari juu ya matendo yangu.

7/06/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Siri Zilizofichwa Nyuma ya Ukimbizaji

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Ushuhuda

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Siri Zilizofichwa Nyuma ya Ukimbizaji

📖📖~~~*******~~~🌻🌻🌻~~~******~~~😘😘
Li Li     Mji wa Dezhou, Mkoa wa Shandong
Sio muda mrefu uliopita, nilitiwa moyo na Mungu na kupandiswa cheo kuwa mfanyakazi wa eneo. Siku moja, nilipokuwa nimekusanyika na wafanyakazi wenzangu, sikuweza kujizuia kufikiria mwenyewe: ni lazima nifanye vyema. Ningetimiza wajibu wangu vibaya, viongozi wangu na wafanyakazi wenzangu wangenionaje? Matokeo yake yalikuwa, tulipozungumzia mada fulani pamoja, almradi nilikuwa na ufahamu kidogo wa mada hiyo, basi ningejaribu kuwa wa kwanza kusema kitu, hata hivyo wakati sikuwa na ufahamu wa mada iliyojadiliwa na sikuweza kusema chochote, nilijipata nikiwa na wasiwasi.

6/27/2018

Matamshi ya Mungu | Maisha Ya Kawaida ya Kiroho Huwaongoza Watu Kwenye Njia Sahihi

Mwenyezi Mungu alisema, Mmetembea tu sehemu ndogo sana ya njia ya muumini katika Mungu, na bado hamjaingia kwenye njia sahihi, kwa hiyo bado mko mbali na kutimiza kiwango cha Mungu. Hivi sasa, kimo chenu hakitoshi kuyakidhi mahitaji Yake. Kwa sababu ya ubora wenu wa tabia na vilevile asili yenu ya maumbile ya upotovu, nyinyi daima huichukulia kazi ya Mungu kwa uzembe na hamuichukulii kwa uzito. Hii ni dosari yenu kubwa zaidi.

6/17/2018

Meupe na Safi ni Maji yaliyo Kando ya Kiti cha Enzi cha Mungu

Maji yaliyo kando ya kiti cha enzi cha Mungu, safi na meupe, yanatulisha sisi.
Neno la Mungu, maji ya uzima, mtiririko unaostawisha mioyo yetu.
Mwenyezi Mungu, tunakusifu Wewe. Shukrani ziwe Kwako na mwanga Wako!
Kutoka kwa upotovu Ulituokoa, hivyo sasa tunaishi katika mwanga Wako!
Sasa tunaishi katika mwanga Wako!

6/14/2018

Kutumia Neno la Mungu Kama Kioo

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kanisa
Wu Xia    Mji wa Linyi , Mkoa wa Shandong
Baada ya kuikubali kazi hii na kula na kunywa neno la Mungu, ilikuwa dhahiri kwangu kwamba ni muhimu sana kwamba mimi nijifahamu. Kwa hiyo, nilipokuwa nikila na kunywa neno la Mungu, nilihakikisha nimejithibitisha tena dhidi ya neno ambalo Mungu humfichua mwanadamu. Katika hali nyingi, niliweza kutambua kasoro zangu na upungufu. Nilihisi kwamba ningekuja kujifahamu kweli. Hata hivyo, ilikuwa ni kwa njia ya ufunuo kutoka kwa Mungu tu nilipoweza kuona kwamba kwa hakika sikujifahamu kulingana na neno la Mungu.

5/22/2018

Swahili Gospel Song "Sala ya Watu wa Mungu" | Kuishi katika Upendo wa Mungu


Watu wa Mungu wanainuliwa mbele ya kiti Chake cha Enzi,  
maombi mengi mioyoni mwao. 
Mungu huwabariki wote wanaorejea Kwake; 
wote wanaishi katika mwanga.
Omba Roho Mtakatifu alipe nuru neno la Mungu 
ili kwamba tujue kikamilifu mapenzi ya Mungu.
Tunaomba watu wote walitunze sana neno la Mungu 
na waje kutafuta kumjua Mungu.

5/14/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Asili na Utambulisho wa Mwanadamu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Asili na Utambulisho wa Mwanadamu

Kwa kweli, hawajasikitika, na wamekuwa wakitazama kile ambacho kimefanywa kwa miaka elfu sita iliyopita mpaka leo, kwa kuwa Sikuwaacha. Badala yake, kwa sababu mababu zao walikula tunda kutoka kwa mti wa ujuzi wa mema na maovu lililotolewa na yule mwovu, waliniacha kwa ajili ya dhambi. Mema ni Yangu, wakati maovu ni ya yule mwovu ambaye hunihadaa kwa ajili ya dhambi. Mimi Siwalaumu mwanadamu, wala Siwaangamizi kwa ukatili au kuwatolea kuadibu kusiko na huruma, kwani uovu haukuwa wa wanadamu kiasili.

4/26/2018

Swahili Christian Song "Ni Furaha Kuu kuwa Mtu Mwaminifu" | Mbinguni ni mahali pa mtu mwaminifu




🎉🎉****************🎻🎻**************🎙️🎙️*******************🎼🎼
😇😇*******************💓💓****************🎧🎧****************🌺🌺🌺
Kuelewa ukweli huiachilia huru roho ya mtu 
na kumfanya mtu kuwa mwenye furaha.
Nimejazwa na imani katika neno la Mungu na sina shaka.
Mimi niko bila uhasi wowote, 
sirudi nyuma, na kamwe sikati tamaa.
Ninauunga mkono wajibu wangu 
kwa moyo wangu wote na mawazo, na siujali moyo.
Ingawa ubora wa tabia yangu ni wa chini, 
nina moyo wa uaminifu.
Nimejitolea kikamilifu katika kila kitu 
ili kuyaridhisha mapenzi ya Mungu.

4/23/2018

Sura ya 42. Kwa Kutafuta Ukweli Tu Ndio Unaweza Kupata Mabadiliko Katika Tabia Yako

Mwenyezi Mungu alisema, Kwa kutafuta ukweli tu ndipo utapata mabadiliko katika tabia yako: Hili ni jambo unalofaa kulielewa na kulielewa vizuri kabisa. Usipoelewa ukweli vya kutosha, utateleza kwa urahisi na kupotoka. Kutafuta kukua katika maisha lazima utafute ukweli katika kila kitu. Haijalishi suala gani laweza kutokea, lazima utafute kukumbana nalo katika njia inayopatana na ukweli, kwa sababu ukikumbana nayo kwa njia isiyo safi kabisa, basi unaenda kinyume na ukweli. Chochote ufanyacho, lazima kila wakati ufikirie thamani yake. Unaweza kufanya yale mambo yaliyo na maana na lazima usifanye mambo yasiyo na maana.

3/13/2018

🧡💖🌱53. Kukubali Ukweli kwa Hakika Ni Nini?

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kanisa

Xiaohe Mji wa Puyang, Mkoa wa Henan
Hapo awali, kila wakati niliposoma maneno yaliyofichuliwa na Mungu kuhusu jinsi watu hawakubali ukweli, sikuamini kwamba maneno hayo yangetumika kwangu. Nilifurahia kula na kunywa neno la Mungu na kuwasiliana kuhusu neno la Mungu, na niliweza kukubali na kukiri kila kitu ambacho Mungu amesema kuwa ukweli—bila kujali jinsi kilivyoumiza moyo wangu au jinsi hakikuambatana na mawazo yangu. Aidha, bila kujali kiwango cha dosari kaka na dada zangu wangeonyesha, ningekikiri na kukikubali. Sikutafuta kujitetea mwenyewe, hivyo nilidhani kwamba nilikuwa mtu ambaye kwa hakika alikubali ukweli.

3/11/2018

Sura ya 53. Kuelewa Visawe na Tofauti katika Asili ya Binadamu

Umeme wa Mashariki | Sura ya 53. Kuelewa Visawe na Tofauti katika Asili ya Binadamu

Je, mnaona kwa dhahiri njia ya imani yenu kwa Mungu na njia yenu ya kufuata ukweli? Imani katika Mungu kweli ni nini? Je, mmetosheka baada ya kupitia shida kidogo? Watu wengine hufikiri kwamba baada ya kupitia hukumu na kuadibiwa, kupogolewa na ushughulikiwaji au baada ya kufichua hali yao ya kweli, wamemaliza na matokeo yao yameonekana. Wengi wa watu hawawezi kuona suala hili kwa dhahiri, na wao wote husimamishwa hapo, bila kujua jinsi ya kuitembea njia iliyo mbele. Kwa ujumla, wasipopitia ushughulikiwaji na upogolewaji au hawana vikwazo vyovyote, watahisi kama kutafuta ukweli wakati wakiamini katika Mungu, na watahisi kwamba wanapaswa kuyatosheleza mapenzi ya Mungu.

3/04/2018

Umeme wa Mashariki | 62. Sababu ya Kweli ya Kazi Isiyofaa

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kanisa

Umeme wa Mashariki | 62. Sababu ya Kweli ya Kazi Isiyofaa
Xinyi Mji wa Xi’an, Mkoa wa Shaanxi
Katika ziara zangu za karibuni kwa makanisa, mara nyingi niliwasikia viongozi na wafanyakazi wakisema kwamba watu wengine, baada ya kuhudhuria ushirika na mimi, waligeuka hasi, wanyonge na walikosa motisha ya kuendelea kutafuta. Wengine walisema ilikuwa vigumu sana kumwamini Mungu na walimwelewa Mungu visivyo. Wengine walisema kwamba hali zao zilikuwa nzuri kabla ya wao kukutana na mimi, lakini punde tu waliponiona, walihisi shinikizo kubwa mno na wasio na raha.

2/16/2018

17 Ufahamu wa Kupata Mwili

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki, Kupata Mwili
Bwana-Yesu, Kupata Mwili
Mwenyezi Mungu alisema, Kumjua Mungu kunapaswa kufanywa kupitia kwa kusoma neno la Mungu na kulielewa neno la Mungu. Watu wengine husema: "Sijamwona Mungu mwenye mwili, hivyo nitawezaje kumjua Mungu?" Neno la Mungu kwa kweli ni maonyesho ya tabia ya Mungu. Kutoka kwa neno la Mungu unaweza kuuona upendo wa Mungu kwa wanadamu, wokovu Wake wa wanadamu, na jinsi Anavyowaokoa ... kwa sababu neno la Mungu linaonyeshwa na Mungu ikilinganishwa na Mungu kumtumia mwanadamu kuliandika.

2/14/2018

Neno la Mwenyezi Mungu | Sura ya 37. Kanuni Kuu za Jinsi Wafanyakazi Hufanya Kazi

 Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Biblia

Neno la Mwenyezi Mungu | Sura ya 37. Kanuni Kuu za Jinsi Wafanyakazi Hufanya Kazi

    Katika kazi yao, wafanyakazi wanapaswa kuzingatia mambo mawili: Moja ni kufanya kazi kabisa kulingana na kanuni zilizowekwa masharti na mipangilio ya kazi. Wafanyakazi hawapaswi kukiuka kanuni hizi, wasifanye kazi kulingana na mawazo yao wenyewe, na siyo kulingana na mapenzi yao. Wanapaswa kuonyesha uhusiano kwa kazi ya familia ya Mungu, na kuweka maslahi ya familia ya Mungu kwanza katika kila kitu wakifanyacho. Jambo jingine pia ni muhimu, na ni kwamba, katika kila kitu wakifanyacho, kuzingatia kufuata mwongozo wa Roho Mtakatifu, na kufanya kila kitu kwa ukali kulingana na neno la Mungu.