11/29/2017

Kuuweka tu Ukweli Katika Matendo Ni Kuwa na Uhalisi


Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,ndugu na dada
watu wa Mungu ,kumwabudu Mungu

Kuuweka tu Ukweli Katika Matendo Ni Kuwa na Uhalisi

Mwenyezi Mungu alisema, Kuwa na uwezo wa kuyaeleza maneno ya Mungu kiwazi haimaanishi kwamba wewe unaumiliki uhalisi. Mambo si rahisi kama ulivyofikiria. Ikiwa unaumiliki uhalisi au la haina msingi kwa kile unachokisema, badala yake inatokana na kile unachoishi kwa kudhihirisha. Wakati maneno ya Mungu yanakuwa maisha yako na kujionyesha kwako kwa asili, hapo ndipo unapoumiliki uhalisi, hapo ndipo umeupata uelewa na kimo cha kweli.

Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu katika Mwili na Wajibu wa Mwanadamu

Umeme wa Mashariki,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu

Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu katika Mwili na Wajibu wa Mwanadamu

Mwenyezi Mungu alisema, Ni lazima myafahamu maono ya kazi ya Mungu na mpate mwelekeo wa kazi Yake. Huku ni kuingia kwa njia nzuri. Punde mnapong’amua ukweli wa maono kwa usahihi, kuingia wako utakuwa salama; bila kujali kazi Yake hubadilika kiasi gani, utaendelea kuwa imara moyoni mwako, utakuwa wazi kuhusu maono, na utakuwa na lengo la kuingia na kazi yako. Kwa njia hiyo, tajriba na ufahamu ulio ndani yako utakua kwa kina na kutakaswa zaidi. Punde unapong’amua ukweli wote, hutapoteza kitu maishani na hutapotea.Kama hutazijua hatua hizi za kazi, utapata hasara kwa kila mojawapo. Huwezi kugeuka baada ya siku chache tu na hutaweza kuipata njia mwafaka hata katika majuma machache.

11/27/2017

Umeme wa Mashariki | Waovu Lazima Waadhibiwe

Umeme wa Mashariki  Waovu Lazima Waadhibiwe 
    Mwenyezi Mungu alisema, Kukagua kama unatenda uhaki katika kila jambo unalotenda, na iwapo matendo yako yanachunguzwa na Mungu, ni tabia za kanuni za wale wanaomwamini Mungu. Utaitwa mwenye haki kwa sababu una uwezo wa kukidhi matakwa ya Mungu, na kwa sababu umekubali utunzaji na ulinzi wa Mungu. Machoni pa Mungu, wote wanaokubali utunzaji, ulinzi na ukamilishaji Wake na wale waliopatwa Naye, ni wenye haki na hutazamwa kwa upendo sana Mungu. Zaidi ya unavyokubali neno la Mungu wakati huu, ndivyo unavyoweza kupokea na kuelewa mapenzi ya Mungu zaidi, na hivyo ndivyo unavyoweza kuishi kwa kudhihirisha neno la Mungu na kukidhi mahitaji Yake. Haya ndiyo maagizo ya Mungu kwako na kile unapaswa kufikia.

11/26/2017

Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,uaminifu
Umeme wa Mashariki | Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu

Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu

    Mwenyezi Mungu alisema, Kazi ya Mungu katika mwili inajumuisha sehemu mbili. Mara ya kwanza Alipofanyika kuwa mwili, watu hawakumwamini au kumfahamu na kumsulubisha Yesu msalabani. Mara ya pili, pia, watu pia hawakuamini ndani Yake, wala kumfahamu, na kwa mara nyingine wakamsulubisha Kristo msalabani. Je, si mwanadamu ni adui wa Mungu? Kama mwanadamu hamjui Yeye, mwanadamu anawezaje kuwa mwandani wa Mungu? Na anawezaje kuwa amehitimu kumshuhudia Mungu? Kumpenda Mungu, kumtumikia Mungu, kumtukuza Mungu—je, huu si udanganyifu?

11/25/2017

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha Kwa ajili ya Hatima Yako

Umeme wa Mashariki | Kanisa la Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha Kwa ajili ya Hatima Yako

   
      Nimefanya kazi nyingi miongoni mwenu na, bila shaka, Nimetamka mengi pia. Hata hivyo, Nahisi kwamba maneno na kazi Yangu havijatimiza lengo la kazi Yangu ya siku za mwisho kikamilifu. Maana, katika siku za mwisho, kazi Yangu si kwa ajili ya mtu au watu fulani, bali ni kwa manufaa ya kufafanua tabia Yangu asilia. Hata hivyo, kutokana na sababu nyingi—pengine ukosefu wa muda au shughuli nyingi za kazi—tabia Yangu haijamwezesha binadamu kunijua hata kidogo. Kwa hivyo, Ninasonga mbele katika mpango Wangu mpya, katika kazi Yangu ya mwisho, kufungua ukurasa mpya katika kazi Yangu ili wale ambao wanaoniona watajipiga kifuani na kuulilia na kuombolezea uwepo Wangu bila kukoma.

11/24/2017

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV

Umeme wa Mashariki | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV

Utakatifu wa Mungu (I)

Mwenyezi Mungu alisema, Tumekuwa na ushirika wa ziada wa mamlaka ya Mungu leo, na hatutazungumza kuhusu haki ya Mungu sasa hivi. Leo tutazungumza kuhusu mada nzima mpya—utakatifu wa Mungu. Utakatifu wa Mungu pia ni kipengele kingine cha kiini cha kipekee cha Mungu, hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kushiriki mada hii hapa. Hiki kipengele cha kiini cha Mungu ambacho Nitashiriki, pamoja na vile vipengele viwili tulivyoshiriki mbeleni, tabia ya haki ya Mungu na mamlaka ya Mungu—yote ni ya kipekee? (Ndiyo.) Utakatifu wa Mungu pia ni wa kipekee, basi msingi wa upekee huu, mzizi wa upekee huu, ni maudhui ya ushirika wetu wa leo.Mnaelewa? Rudieni nyuma Yangu: kiini cha kipekee cha Mungu—utakatifu wa Mungu.

11/23/2017

Kumjua Mungu Ndiyo Njia ya Kumcha Mungu na Kuepuka Maovu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu
Umeme wa Mashariki | Kumjua Mungu Ndiyo Njia ya Kumcha Mungu na Kuepuka Maovu
Mwenyezi Mungu alisema, Kila mmoja anapaswa kuchunguza maisha yake upya ya kumwamini Mungu ili kuona iwapo, katika kumtafuta Mungu, ameelewa kwa dhati, amefahamukwa dhati, na kuja kumjua Mungukwa dhati, iwapo anajua kweli ni mawazo gani Mungu Anayo kwa aina tofauti za binadamu, na iwapo kweli anaelewa kile ambacho Mungu Anafanya juu yake na jinsi Mungu Anaeleza kila tendo lake. Huyu Mungu, Ambaye yuko kando yako, Akiongoza mwelekeo wa kuendelea kwako, Akiamuru hatima yako, na kukupa mahitaji yako—ni kiasi gani ambacho, katika uchambuzi wako, unaelewa nani kiasi gani ambacho kweli unajua kumhusu Yeye?

11/22/2017

Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki
Umeme wa Mashariki | Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu
Mwenyezi Mungu alisema, Kunayo mambo mengi ambayo Ninatumai mtaweza kufikia. Hata hivyo, matendo yenu na maisha yenu yote hayawezi kutimiza kwa ujumla mahitaji Yangu, kwa hiyo lazima Nilenge suala moja kwa moja na kuwafafanulia moyo na akili Zangu. Tukichukulia kwamba uwezo wenu wa utambuzi na ufahamu wenu vyote ni duni sana, karibu mmekosa kabisa kujua tabia na dutu Yangu, na hivyo ni suala la dharura kwangu Mimi kuwafahamisha kuhusu haya. Haijalishi hapo awali ulielewa kiwango kipi au kama uko radhi kuelewa masuala haya, lazima bado Niyaelezee kwenu kwa undani.Suala hili si lile ambalo ni geni sana kwenu, lakini inaonekana kwamba hamwelewi au hamjazoea maana iliyomo kwenye suala hili.

Umeme wa Mashariki | Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Yesu
Mwenyezi Mungu alisema, Mpango Wangu mzima wa usimamizi, ambao una urefu wa miaka elfu sita, unashirikisha awamu tatu, au enzi tatu: Kwanza, Enzi ya Sheria; pili, Enzi ya Neema (ambayo pia ni enzi ya Ukombozi); na mwisho, Enzi ya Ufalme. Kazi Yangu katika enzi hizi tatu hutofautiana katika maudhui kulingana na asili ya kila enzi, lakini katika kila hatua huambatana na mahitaji ya mwanadamu—au, sahihi zaidi, inafanywa kulingana na ujanja ambao Shetani anatumia katika vita Vyangu dhidi yake. Madhumuni ya Kazi Yangu ni kumshinda Shetani, ili kutoa wazi hekima Yangu na kudura, kufichua ujanja wote wa Shetani na hivyo kuokoa wanadamu wote, wanaoishi chini ya miliki yake.

11/20/2017

Video za Kikristo | Kuelezea Wazi Uhusiano Kati ya Biblia na Mungu | "Biblia na Mungu" (Swahili Subtitles)


Video za Kikristo | Kuelezea Wazi Uhusiano Kati ya Biblia na Mungu | "Biblia na Mungu" (Swahili Subtitles)

Liu Zhizhong ni mzee katika kanisa moja la mtaani la nyumba nchini China. Amekuwa muumini kwa zaidi ya miaka 30, na amesisitiza bila kukoma kwamba “Biblia ni ufunuo wa Mungu,” “Biblia inamwakilisha Mungu, kuamini katika Mungu ni kuamini katika Biblia, kuamini katika Biblia ni kuamini katika Mungu.” Moyoni mwake, Biblia ni kuu. Kwa sababu ya upendo na imani yake pofu katika Biblia, hajawahi kutafuta au kuitazama kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho. Hadi siku moja, alipowazuia waumini kusoma maneno ya Mwenyezi Mungu mtandaoni, akawa na fursa ya kukutana na wahubiri kutoka katika Kanisa la Mwenyezi Mungu.

11/19/2017

Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani


Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mungu
Umeme wa Mashariki | Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani
Mwenyezi Mungu alisemai ,Nyinyi nyote mna furaha kupokea tuzo mbele ya Mungu na kutambuliwa na Mungu. Haya ni matakwa ya kila mtu baada ya yeye kuanza kuwa na imani kwa Mungu, kwani mwanadamu kwa moyo wake wote hutafuta mambo yaliyo juu na hakuna aliye tayari kubaki nyuma ya wengine. Hii ndiyo njia ya mwanadamu. Kwa sababu hii, wengi kati yenu wanajaribu daima kupata neema ya Mungu mbinguni, lakini kwa kweli, uaminifu wenu na uwazi kwa Mungu ni wa kiasi kidogo sana ukilinganishwa na uaminifu na uwazi wenu kwenu wenyewe.Mbona Nasema hivi? Kwa sababu Sikiri uaminifu wenu kwa Mungu kabisa, na zaidi Nakana kuwepo kwa Mungu ndani ya mioyo yenu.

Kujadili Maisha ya Kanisa na Maisha Halisi

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kanisa
Umeme wa Mashariki | Kujadili Maisha ya Kanisa na Maisha Halisi
Mwenyezi Mungu alisema, Watu huhisi kuwa wao wanaweza tu kubadilika katika maisha yao ya kanisani, na kuwa iwapo hawaishi ndani ya kanisa, mbadiliko hauwezekani, kuwa hawawezi kutimiza mbadiliko katika maisha yao halisi. Mwaweza kutambua suala hili ni lipi? Nimeongea juu ya kumleta Mungu katika maisha halisi, na hii ndiyo njia kwa wale wanaomwamini Mungu kuingia katika uhalisi wa maneno ya Mungu. Kwa kweli, maisha ya kanisa ni njia ndogo tu ya kuwakamilisha watu. Mazingira ya msingi ya kuwakamilisha wanadamu bado ni maisha halisi. Hiki ndicho kitendo halisi na mafunzo halisi Niliyozungumzia, yanayowaruhusu wanadamu kutimiza maisha ya ubinadamu wa kawaida na kuishi kwa kudhihirisha mfano wa mtu wa kweli katika maisha ya kila siku. Kipengele kimoja ni kwamba mtu lazima aelimike ili kuinua kiwango chake mwenyewe cha elimu, aweze kuelewa maneno ya Mungu, na kutimiza uwezo wa kuelewa.

11/18/2017

Tofauti Muhimu Kati ya Mungu Aliyepata Mwili na Wanadamu Wanaotumiwa na Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki


Kwa miaka mingi Roho wa Mungu Amekuwa Akifanya kazi kwa kutafuta duniani. Kwa enzi nyingi Mungu Ametumia wanadamu wengi kufanya kazi Yake. Hata hivyo Roho wa Mungu bado hana mahali pazuri pa kupumzika. Kwa hivyo Mungu hupitia wanadamu mbalimbali kufanya kazi Yake na kwa kiasi kikubwa hutumia wanadamu kufanya hivyo. Yaani, katika miaka hii yote mingi, kazi ya Mungu haijawahi kusimama. Inaendelezwa mbele kupitia mwanadamu, bila kikomo mpaka siku ya leo. Ingawa Mungu Amesema na Ametenda mengi, mwanadamu bado hamjui Mungu, hii ni kwa sababu Mungu hajawahi kuonekana na mwanadamu na Yeye Hana umbo.