1/14/2018

Kwa Furaha Ukaribishe Ujio wa Mungu! | Kwaya ya Injili ya Kichina Onyesho la 19” | Haleluya

Jinsi Bwana Anavyowasili

Umeme wa Mashariki,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Injili



Katika mwili wa kiroho, au katika mwili wa kawaida? "Nanyi jiwekeni tayari, kwa kuwa saa msiyodhani ndipo atakapokuja Mwana wa Adamu"(Luka 12:40). “Kwa maana kama umeme utokavyo mashariki, na kumulika hata magharibi; hivyo ndivyo ujio wake Mwana wa Adamu utakavyokuwa” (Mathayo 24: 27). “Wakati huu, Mungu haji kufanya kazi kwa mwili wa kiroho ila kwa ule wa kawaida sana. Sio tu mwili wa kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya pili, lakini pia mwili ambao Mungu anarudia.”(Neno Laonekana katika Mwili).

1/13/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | 32 Ni Watu wa Aina Gani Watakaoadhibiwa

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,hukumu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | 32  Ni Watu wa Aina Gani Watakaoadhibiwa

   Kukufuru na kashfa   Kukufuru na kashfa dhidi ya Mungu ni dhambi ambayo haitasamehewa kwa enzi hii na enzi ijayo na wale wanaofanya dhambi hii hawatazaliwa upya kamwe. Hili linamaanisha kwamba tabia ya Mungu haiwezi kuvumilia kosa la wanadamu. Watu wengine wanaweza kusema maneno yasiyofaa au maneno mabaya wakati hawaelewi, au wanapodanganywa, kuwekewa vikwazo, kudhibitiwa, au kukandamizwa na wengine. Lakini wanapokubali njia ya ukweli katika siku zijazo watajawa na majuto. Halafu wao hufanya matendo mazuri ya kutosha na wanaweza kupata mabadiliko na kufikia ufahamu, na kwa njia hii kosa lao la awali halitakumbukwa tena.

1/12/2018

Karibu Kurudi kwa Bwana Yesu | Drama yenye Muziki ya Sifa za Ufalme–Enzi Mpya Imeanza!


Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kanisa
Chini ya mbingu ya usiku yenye nyota, tulivu na kimya, kundi la Wakristo wanasubiri kwa ari kurudi kwa Mwokozi wakiimba na kucheza kwa muziki mchangamfu.Wanaposikia habari za furaha "Mungu amerejea" na "Mungu ametamka maneno mapya", wanashangaa na kusisimka. Wanafikiri: "Mungu ameonekana? Tayari ametokea?" Kwa udadisi na kutokuwa na uhakika, mmoja baada ya mwingine, wanaingia katika safari ya kuyatafuta maneno mapya ya Mungu. .Katika kutamafuta kwao kugumu, baadhi ya watu wanauliza maswali hali wengine wanalikubali tu.baadhi ya watu wanaangalia bila kutoa maoni, wakati wengine wanafanya mapendekezo na kutafuta majibu katika Biblia–wanaangalia lakini mwishowe kuangalia huku hakuzai matunda.Wakati tu wanapokata tamaa, shahidi mmoja anawaletea nakala ya Biblia ya Enzi ya Ufalme, na wanavutiwa kwa kina na maneno yaliyomo katika kitabu. Hiki ni kitabu cha aina gani kweli? Je, kwa kweli wamepata maneno mapya ambayo Mungu ameyanena katika kitabu hiki? Je, wamekaribisha kwa furaha kuonekana kwa Mungu?

1/11/2018

12 Mapenzi ya Mungu ni Kuwaokoa Watu kwa Kiwango Kikubwa Sana Kinachowezekana

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu
Yesu Kristo,Kuonekana kwa Mungu

1. Usijishughulishe na Ikiwa Umejaaliwa na Mungu, bali Ujishughulishe na Ufuatiliaji Wako

Mwenyezi Mungu alisema, Watu wengi hawaelewi mapenzi ya Mungu; wanafikiri kuwa kila mtu ambaye ameamuliwa na Mungu ataokolewa bila kuepuka na wanafikiri kuwa kila mtu asiyeamuliwa na Mungu hataokolewa hata wakiyafanya mambo vyema zaidi. Wanafikiri kwamba Mungu hataamua matokeo ya watu kulingana na utendaji na tabia yao. Iwapo unafikiri hivi, basi unamwelewa Mungu visivyo kabisa. Iwapo Mungu angefanya hili kweli, basi Mungu angekuwa mwenye haki? Mungu huamua matokeo ya watu kulingana na kanuni: Mwishowe matokeo ya watu yataamuliwa kulingana na utendaji wao wa kibinafsi na tabia. Huoni tabia ya Mungu yenye haki, na daima unamwelewa Mungu visivyo na kugeuza nia Zake, ambayo hukufanya daima uwe bila rajua na kupoteza matumaini.

1/10/2018

Sura ya 10. Wale Wanaopenda Ukweli Wana Njia ya Kufuata

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,kanisa

1. Kama hali ya Watu Ni Ya Kawaida Inategemea na Kama Wanapenda Ukweli au La

Mwenyezi Mungu alisema, Watu wengi wameibua suala lifuatalo: Baada ya ushirika wa juu, wanahisi wazi kabisa, wanakuwa na nguvu zaidi, na hawana hisia hasi—lakini hali kama hiyo inabaki tu kwa karibu siku kumi, ambapo baadaye hawawezi kudumisha hali ya kawaida. Suala ni nini? Je mmewahi kujiuliza kinachosababisha hili? Mbona hali zenu ni nzuri sana katika siku hizo takriban kumi za kwanza? Wengine wanasema kuwa hili ni tokeo la kutolenga ukweli. Lakini hivyo ungeweza vipi kufikia kiwango hiki cha kawaida baada ya kusikia ushirika? Mbona ulikuwa na furaha sana baada ya kuusikia ukweli? Wengine wanasema ni kwa sababu ya kazi ya Roho Mtakatifu.

1/09/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu, Maoni Wanayopaswa Kushikilia Waumini

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Biblia
neno la mungu,biblia

Matamshi ya Mwenyezi Mungu, Maoni Wanayopaswa Kushikilia Waumini 

Ni kitu gani ambacho mwanadamu amepokea tangu alipomwamini Mungu mara ya kwanza? Umejua kitu gani kumhusu Mungu? Umebadilika kiasi gani kwa sababu ya imani yako kwa Mungu? Sasa mnajua nyote ya kwamba imani ya mwanadamu katika Mungu si kwa ajili ya wokovu wa roho na ustawi wa mwili tu, wala si kuimarisha maisha yake kwa njia ya upendo wa Mungu, na kadhalika. Kama ilivyo sasa, kama unampenda Mungu kwa ajili ya ustawi wa mwili au furaha ya muda, basi hata kama, mwishoni, upendo wako kwa Mungu utafikia kilele chake na wewe hutaulizia kitu chochote, upendo huu unaoutafuta ni upendo mchafu na haumpendezi Mungu.

1/07/2018

Karibu Kurudi kwa Bwana Yesu | Drama ya Muziki “ Kwaya ya Injili ya Kichina Onyesho la 19” | Haleluya

Chini ya mbingu ya usiku yenye nyota, tulivu na kimya, kundi la Wakristo wanasubiri kwa ari kurudi kwa Mwokozi wakiimba na kucheza kwa muziki mchangamfu.Wanaposikia habari za furaha "Mungu amerejea" na "Mungu ametamka maneno mapya", wanashangaa na kusisimka. Wanafikiri: "Mungu ameonekana? Tayari ametokea?" Kwa udadisi na kutokuwa na uhakika, mmoja baada ya mwingine, wanaingia katika safari ya kuyatafuta maneno mapya ya Mungu. Katika kutafuta kwao kugumu, baadhi ya watu wanauliza maswali hali wengine wanalikubali tu. baadhi ya watu wanaangalia bila kutoa maoni, wakati wengine wanafanya mapendekezo na kutafuta majibu katika Biblia–wanaangalia lakini mwishowe kuangalia huku hakuzai matunda ....

1/06/2018

Umeme wa Mashariki | 13 Maana ya Utendaji wa Watu Kuamua Matokeo Yao

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,kanisa
hukumu,ukweli
neno la Mwenyezi Mungu13.Maana ya Utendaji wa Watu Kuamua Matokeo Yao
Kwa sasa, utendaji wa watu unaamua matokeo yao, lakini huu utendaji ni upi? Je, unaujua? Nyinyi mnaweza kufikiri kwamba hili linarejelea tabia ya watu iliyopotoka ikijionyesha kazini mwao, lakini halimaanishi lile. Utendaji huu unanena kuhusu ikiwa unaweza kuweka ukweli kwenye vitendo au la na ikiwa unaweza kusalia mwaminifu na kujizatiti unapotenda wajibu wako au la, na vilevile mtazamo wako wa kumwamini Mungu, msimamo wako kwa Mungu, uamuzi wako wa kuteseka kwa ajili ya ugumu, mtazamo wako kwa kukubali hukumu na kupogolewa, kiwango chako cha mabadiliko na idadi ya dhambi kubwa. Haya yote yanachangia katika utendaji wako.

1/05/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu, Tamko La Kwanza

Matamshi ya Mwenyezi Mungu, Tamko La Kwanza

Je, wale wanaoshuhudia maneno Yangu huyakubali kwa kweli? Je, mnanijua kwa kweli? Mmejifunza utiifu kweli? Ninyi hutumia rasilimali kwa ajili Yangu kwa uaminifu? Mmekuwa na ushuhuda thabiti, usiokubali kushindwa Kwangu mlipokabiliwa na joka kuu jekundu? Je, moyo wenu wa ibada hulifedhehesha kweli joka kuu jekundu? Ni kupitia tu kwa jaribio la maneno Yangu ndipo Naweza kutimiza lengo Langu la kulitakasa kanisa na kuwachagua wale wanaonipenda Mimi kweli. Ni jinsi gani tena ambayo mtu yeyote angenielewa Mimi? Ni nani anaweza kuelewa uadhama Wangu, ghadhabu Yangu, na hekima Yangu kupitia kwa maneno Yangu? Nitakamilisha Nilichoanza, lakini bado ni Mimi nipimaye mioyo ya wanadamu. Kwa kweli, hakuna mwanadamu anayenielewa Mimi kwa ukamilifu, kwa hiyo Ninamwongoza kwa maneno, na kumwongoza katika mwongo mpya kwa njia hii.

1/03/2018

Wimbo wa Uzoefu wa Maisha | Nitampenda Mungu Milele

Nyimbo, Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki


Wimbo wa Uzoefu wa Maisha | Nitampenda Mungu Milele

  I
 Ee Mungu! Maneno Yako yameniongoza kurudi Kwako.
Nakubali mafunzo katika ufalme Wako mchana na usiku.
Majaribio mengi na maumivu, mateso mengi sana.
Mara nyingi nilimwaga machozi na kuhisi huzuni,
na mara nyingi nimeanguka katika mtego wa Shetani.Lakini Hujawahi kuniacha.

1/02/2018

Kwa nini Mungu Huchukua Jina la Mwenyezi Mungu Katika Enzi ya Ufalme?

Kwa nini Mungu Huchukua Jina la Mwenyezi Mungu Katika Enzi ya Ufalme?

Watu wengi hawaelewi ni kwa nini, kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni kurudi kwa Bwana Yesu katika siku za mwisho, Bwana Yesu anaitwa Mwenyezi Mungu wakati Anapokuja kufanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho. Kwa nini haendelei kuitwa Bwana Yesu? Kwa kweli, Mungu ana jina jipya kila wakati Anapofanya hatua moja ya kazi Yake. Jina hili jipya linachukuliwa na Mungu Mwenyewe kama inavyofaa kazi hii–siyo kitu ambacho watu humuita Yeye kama wanavyotaka.

1/01/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Maana ya Kuwa Mwanaadamu Halisi

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Maana ya Kuwa Mwanaadamu Halisi

Kumsimamia mwanadamu ndio Kazi Yangu, na ushindi Wangu dhidi yake ulikuwa hata umeshaamuliwa kabla zaidi Nilipoiumba dunia. Watu hawajui kwamba Nitashinda kabisa katika siku za mwisho, na pia hawajui kwamba ushahidi Wangu kumshinda Shetani ni kuwashinda walio waasi miongoni mwa binadamu. Lakini Nilikuwa Nimeshamwambia adui Yangu lilipokuwa linapambana na Mimi kwamba Nitakuwa mshindi wa wale waliokuwa wamechukuliwa na Shetani na kwa muda mrefu walikuwa watoto wa Shetani, na watumishi wake waaminifu wanaoangalia nyumba yake.

12/31/2017

Umeme wa Mashariki | Kuhusu Biblia (4)

Umeme wa Mashariki,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Biblia
maandiko ya Biblia,neno la mungu

                           Umeme wa Mashariki | Kuhusu Biblia (4)

Biblia inaandika masuala ya Israeli na matendo ya watu wake wateule wakati huo. Kwa maneno mengine, ni maelezo ya masuala ya Yehova, ambayo kwayo Roho Mtakatifu hatoi lawama. Ingawa kulikuwa na uteuzi wa sehemu za kujumuisha au kuondolewa, ingawa Roho Mtakatifu hathibitishi, bado Hatoi lawama. Biblia si kitu chochote zaidi ya historia ya Israeli na kazi ya Mungu. Watu, masuala, na mambo inayoyarekodi yote yalikuwa ya kweli, na hakuna kitu kuhusu hayo kilikuwa ni ishara ya maisha ya baadaye—mbali na unabii wa Isaya na Danieli, au kitabu cha Yohana cha maono. Watu wa awali wa Israeli walikuwa wenye maarifa na watu wenye utamaduni wa hali ya juu, na maarifa yao ya kale na utamaduni ulikuwa wa kiwango cha juu, na hivyo kile walichoandika kilikuwa cha kiwango cha juu kuliko watu wa leo.