1/22/2018

30 Kumtumikia Mungu Mtu Anapaswa Kutembea Njia ya Petro

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Yesu
Kumtumikia Mungu Mtu Anapaswa Kutembea Njia ya Petro
Mwenyezi Mungu alisema, Watu wengi hawawezi kuainisha ni watu gani wana ukweli, watu gani hawana ukweli na watu gani husema mambo yaliyo na ukweli. Unapoulizwa kueleza ni nini maana ya "ukweli," huwezi kueleza kwa wazi. Lakini mara tu mtu anaposema kitu, unasema: “Mtazamo wake ni wa kweli. Maneno ayasemayo yanaonyesha ufahamu wa utendaji uliopatikana kupitia kwa uzoefu.” Unaelewa mara tu unapowasikia wakizungumza. Kwa ninyi hapa mlio wapya, Nikiwauliza ni nini maana ya 'uhalisi,' hamtaweza tu kunijibu, lakini pia hamtaweza kueleza tofauti kati ya mtu anayezungumza uhalisi na mtu anayezungumza mafundisho ya dini.

Kanisa la Mwenyezi Mungu | 003 Zingatia Majaliwa ya Binadamu



Kanisa la Mwenyezi Mungu | Wimbo wa Maneno ya Mungu | Zingatia Majaliwa ya Binadamu

I
Mungu awahimiza makabila yote, mataifa na nyanja zote:
Sikizeni sauti Yake, muione kazi Yake;
mzingatie hatima ya wanadamu;
mfanye Mungu Mtakatifu na Mheshimiwakl, Mkuu na wa pekee wakuabudiwa,
ulimwengu wote, na wanadamu, waishi chini ya baraka Yake Mungu,
kama vizazi vya Ibrahimu, walivyoishi na ahadi ya Yehova,
kama viumbe vya Mungu, Adamu na Hawa, walivyoishi bustani Edeni.
Kazi ya Mungu ni kama mawimbi yavumayo hakuna wa kumzuia au kumsimamisha.

1/21/2018

Ni Tofauti Gani Iliyopo Kati Ya Ukristo na Kanisa la Mwenyezi Mungu?

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Ukristo

Ni Tofauti Gani Iliyopo Kati Ya Ukristo na Kanisa la Mwenyezi Mungu? 

Ukristo na Kanisa la Mwenyezi Mungu huamini katika Mungu huyo huyo. Watu wanaoelewa historia ya dini wanajua kwamba Uyahudi wa Israeli ulizaliwa na kazi ambayo Yehova Mungu alifanya wakati wa Enzi ya Sheria. Ukristo, Ukatoliki, na Othodoksi ya Mashariki yote yalikuwa makanisa yaliyoibuka baada ya Bwana Yesu mwenye mwili kufanya kazi ya ukombozi. Kanisa la Mwenyezi Mungu lilikuja kuwepo wakati Mungu alipopata mwili wakati wa siku za mwisho kufanya kazi ya hukumu.

Kumpenda Mungu Tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli

 Mwenyezi Mungu ,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki
Matamshi ya Mwenyezi MunguMnapotaka kumpenda na kumjua Mungu leo, kwa upande mmoja ni lazima mstahimili mateso, usafishaji, na kwa ule upande mwingine, ni lazima mgharamike. Hakuna funzo lililo kubwa kuliko lile la kumpenda Mungu, na inaweza kusemwa kuwa funzo ambalo watu hujifunza katika maisha yao yote ya imani ni jinsi ya kumpenda Mungu. Hii ni kusema, kama unamwamini Mungu ni lazima umpende Mungu. Ikiwa unamwamini tu Mungu lakini humpendi, hujapata ufahamu wa Mungu, na hujawahi kumpenda Mungu kwa upendo wa kweli utokao moyoni mwako, basi imani yako kwa Mungu ni bure; kama katika imani yako kwa Mungu humpendi Mungu, basi unaishi bure, na maisha yako yote ndiyo ya duni zaidi kwa maisha yote.

1/20/2018

Fuata Nyayo za Mwanakondoo |“ Kwaya ya Injili ya Kichina Onyesho la 19” | Haleluya

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,Wakristo

Fuata Nyayo za Mwanakondoo

Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Fuata Nyayo za Mungu! “Hawandio wanaomfuata Mwanakondoo kokote aendako” (Revelation 14:4). Kwa kuwa tunaamini katika Bwana, kufuata nyayo za Mwanakondoo ni muhimu zaidi!

Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Uaminifu
Mwenyezi Mungu alisema, Alipokuwa akiadibiwa na Mungu, Petro aliomba, "Ee Mungu! Mwili wangu ni mkaidi, na unaniadibu na kunihukumu mimi. Nafurahi katika adabu Yako na hukumu, na hata kama Hunitaki mimi, katika hukumu Yako mimi ninaona tabia Yako takatifu na tabia Yako ya haki. Unaponihukumu, ili wengine wapate kuiona hali Yako ya haki katika hukumu Yako, ninaridhika. Iwapo hukumu Yako itaonyesha tabia Yako, na kuruhusu tabia Yako ya haki kuonekana na viumbe wote, na iwapo inaweza kufanya upendo wangu Kwako uwe safi zaidi, ili niweze kufikia mfano wa mwenye haki, basi hukumu Yako ni nzuri, kwa maana hivyo ndivyo mapenzi Yako ya neema yalivyo. Najua kwamba bado kuna mengi ndani yangu yaliyo ya uasi, na kwamba mimi bado sifai kuja mbele Yako.

1/19/2018

Umeme wa Mashariki | Njia… (1)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki, injili
uhalisia,ushindi,Kanisa

  Umeme wa Mashariki | Njia… (1)

  Katika maisha yake, hakuna mtu anayejua ni aina gani ya vipingamizi ataenda kukutana navyo, wala hajui ni aina gani ya kusafishwa ambayo atapata mara kwa mara. Kwa wengine ni katika kazi yao, kwa wengine ni katika matazamio yao ya siku za baadaye, kwa wengine ni katika familia yao ya asili, na kwa wengine ni katika ndoa yao. Lakini kilicho tofauti nayo ni kwamba leo sisi, kundi hili la watu, tunateseka kwa ajili ya neno la Mungu. Yaani, kama mtu anayemtumikia Mungu, amekutana na vipingamizi katika njia ya kuamini katika Yeye, na hii ni njia ambayo waumini wote hufuata na ni njia iliyo chini ya miguu yetu yote.Ni kutoka katika kipengele hiki ndipo tunaanza rasmi mwendo wetu wa kuamini katika Mungu, kuanza maisha yetu kama binadamu, na kuingia katika njia sahihi ya maisha.

Fungua Mlango na Kumkaribisha Bwana-Kwaya ya Injili ya Kichina Onyesho la 19

Ni Mungu Anayezungumza!

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kanisa
Maneno Yake yenye ari ya onyo kwa wanadamu ni mapole na ya amani. Maneno Yake ambayo huhukumu na kufichua dutu potovu ya watu yana utukufu na ghadhabu. Maneno Yake yamejaa mamlaka, nguvu, na yamejaa hekima. Yote ni ukweli, na uzima! Tumetambua sauti Yake na maneno Yake, tumeona kuonekana Kwake!

1/18/2018

Kazi ya Roho Mtakatifu na Kazi ya Shetani

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki, ndugu na dada
makanisa ya nyumbani
Mwenyezi Mungu alisema, Unaelewa vipi umaalum katika roho? Roho Mtakatifu hufanya vipi kazi ndani ya mwanadamu? Shetani hufanya vipi kazi ndani ya mwanadamu? Roho waovu hufanya vipi kazi ndani ya mwanadamu? Na maonyesho ya kazi hii ni yapi? Wakati kitu kinakufanyikia, je, kinakuja kutoka kwa Roho Mtakatifu, na je, unapaswa kukiheshimu, au kukikataa? Utendaji halisi wa watu huibua mengi ambayo ni ya mapenzi ya kibinadamu ilhali ambayo watu daima huamini kutoka kwa Roho Mtakatifu.

Matamshi ya Mwenyezi Mungu, Tamko La Kumi

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki ,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu, Tamko La Kumi

     Enzi ya Ufalme ni, hata hivyo, tofauti na nyakati za kale. Haihusu kile anachofanya mwanadamu. Badala yake, Mimi binafsi Natekeleza kazi Yangu baada ya kushuka duniani—kazi ambayo wanadamu hawawezi kuelewa wala kufanikisha. Tangu kuumbwa kwa ulimwengu mpaka leo, miaka hii yote daima imehusu kujenga kanisa, lakini hakuna mtu anayesikia kamwea kuhusu kujenga ufalme.

1/17/2018

Mungu ni Mungu | "Zingatia Majaliwa ya Binadamu" | Swahili Christian Song


Zingatia Majaliwa ya Binadamu

Mungu awahimiza makabila yote, mataifa na nyanja zote:
Sikizeni sauti Yake, muione kazi Yake; 
mzingatie hatima ya wanadamu;
mfanye Mungu Mtakatifu na Mheshimiwa, Mkuu na wa pekee wakuabudiwa,

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,nyimbo

1/16/2018

Je, Mwenyezi Mungu na Bwana Yesu ni Mungu Mmoja?

Je, Mwenyezi Mungu na Bwana Yesu ni Mungu Mmoja?

Wanadamu walipopotoshwa na Shetani, Mungu alianza mpango Wake wa usimamizi kwa ajili ya wokovu wa wanadamu. Mungu ametekeleza hatua tatu za kazi kwa ajili ya wokovu wa wanadamu. Wakati wa Enzi ya Sheria, Yehova Mungu alitoa sheria na kuyaongoza maisha ya wanadamu, Akiwafanya watu kujua kwamba wanapaswa kumwabudu Mungu, na kuwafanya wajue dhambi ni nini. Lakini kutokana na ujio wa hatua za mwisho za Enzi ya Sheria, upotovu wa wanadamu ukawa hata wa kina zaidi, na watu mara nyingi walikiuka sheria na kutenda dhambi dhidi ya Yehova.

Umeme wa Mashariki | 45. Kanuni Zangu za Maisha Ziliniacha Nikiwa Nimeharibika

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,Wakristo
Wakristo wa China 

Umeme wa Mashariki | 45. Kanuni Zangu za Maisha Ziliniacha Nikiwa 

NimeharibikaChangkai Mji wa Benxi, mkoa wa Liaoning
Maneno ya kawaida "Watu wazuri humaliza wakiwa wa mwisho" ni ambayo mimi binafsi ninayafahamu sana. Mimi na mume wangu sote tulikuwa hasa watu wasio na hatia: Wakati wa masuala yaliyohusisha faida au hasara yetu binafsi, hatukuwa aina ya watu wa kubishana na kusumbuana na wengine. Pale ambapo tuliweza kuwa wavumilivu tulikuwa wavumilivu, pale ambapo tungeweza kuwa na fadhila tulifanya tulivyoweza kuwa na fadhila. Kama matokeo yake, mara nyingi tulijipata tukiwa tumedanganywa na kudhulumiwa na wengine.