4/27/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | 9. Katikati ya Maafa Niliona Ulinzi wa Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu | 9. Katikati ya Maafa Niliona Ulinzi wa Mungu

Zhang Min, Beijing
Agosti 6, Mwaka wa 2012
Mnamo Julai 21, mwaka wa 2012, mvua ilianza kunyesha sana asubuhi. Kufikia wakati wa adhuhuri wakati nilipaswa kwenda kwa mkutano, niliona mvua ilikuwa nzito sana kiasi kwamba sikutaka kwenda. Lakini ulikuwa mara moja tu kwa wiki, kama singeenda singekuwa na njia yoyote ya kufanya kazi yangu ya kanisa. Chochote kilichokuwako kikiendelea nje, bado ilinipasa nishiriki nao. Nilipofikiria hayo, niliharakisha kwenda kwa mkutano. Baada ya saa kumi alasiri hiyo, yule ndugu wa kiume wa mahali pa kukutana alikimbia akarudi nyumbani akisema: "Bado mnafanya mkutano, endeni nyumbani, kuna maji mengi yanayoteremka pale." Nilikwenda na kuangalia na kulikuwa na maji mengi sana yaliyokuwa yakiteremka, mto huo ulikuwa umefurika na ukipanda juu sana.

4/26/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Ufafanuzi wa Tamko la Kumi na Moja

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Ufafanuzi wa Tamko la Kumi na Moja

Kwa macho ya mwanadamu, inaonekana hakuna badiliko katika matamshi ya Mungu wakati wa kipindi hiki, ambalo ni kwa sababu watu hawawezi kuelewa sheria ambazo kwazo Mungu hunena, na hawafahamu muktadha wa maneno Yake. Baada ya kusoma maneno ya Mungu, watu hawaamini kwamba kuna mafumbo yoyote mapya katika maneno haya; hivyo, hawawezi kuishi maisha yaliyo mapya kiajabu, na badala yake huishi maisha yaliyokwama na yasiyokuwa na uhai. Lakini katika matamshi ya Mungu, tunaona kwamba kuna kiwango cha kina cha maana, kile kisichofahamika na pia kisichofikika na mwanadamu.

Swahili Christian Song "Ni Furaha Kuu kuwa Mtu Mwaminifu" | Mbinguni ni mahali pa mtu mwaminifu




🎉🎉****************🎻🎻**************🎙️🎙️*******************🎼🎼
😇😇*******************💓💓****************🎧🎧****************🌺🌺🌺
Kuelewa ukweli huiachilia huru roho ya mtu 
na kumfanya mtu kuwa mwenye furaha.
Nimejazwa na imani katika neno la Mungu na sina shaka.
Mimi niko bila uhasi wowote, 
sirudi nyuma, na kamwe sikati tamaa.
Ninauunga mkono wajibu wangu 
kwa moyo wangu wote na mawazo, na siujali moyo.
Ingawa ubora wa tabia yangu ni wa chini, 
nina moyo wa uaminifu.
Nimejitolea kikamilifu katika kila kitu 
ili kuyaridhisha mapenzi ya Mungu.

4/25/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Una Mtazamo Upi Kuhusu Nyaraka Kumi na Tatu

 Kanisa la Mwenyezi Mungu | Una Mtazamo Upi Kuhusu Nyaraka Kumi na Tatu

Mwenyezi Mungu alisema, Agano Jipya la Biblia lina nyaraka kumi na tatu za Paulo. Barua hizi kumi na tatu ziliandikwa na Paulo kwa makanisa yaliyomwamini Yesu Kristo wakati wa kazi yake. Yaani, aliziandika barua baada ya Yesu kupaa mbinguni na alifufuliwa. Barua zake ni ushuhuda wa ufufuo wa Bwana Yesu na kupaa mbinguni baada ya kifo Chake, na zinahubiri njia ya watu kutubu na kuubeba msalaba. Kwa kweli, njia hizi na shuhuda zote zilikuwa za kuwafundisha ndugu na dada katika sehemu mbalimbali za Uyahudi wakati huo, kwa sababu wakati huo Paulo alikuwa mtumishi wa Bwana Yesu, na alikuwa ameinuliwa kutoa ushuhuda kwa Bwana Yesu. Watu tofauti huinuliwa kutekeleza kazi Yake tofauti wakati wa kila kipindi cha kazi ya Roho Mtakatifu, yaani, kufanya kazi ya mitume ili kuendeleza kazi ambayo Mungu anakamilisha Mwenyewe.

Hadithi ya 2. Mlima Mkubwa, Kijito Kidogo, Upepo Mkali, na Wimbi Kubwa | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII

Kijito Kidogo,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Hadithi ya 2. Mlima Mkubwa, Kijito Kidogo, Upepo Mkali, na Wimbi Kubwa

Mwenyezi Mungu alisema, Kulikuwa na kijito kidogo kilichotiririka kwa kuzungukazunguka, hatimaye kikawasili chini ya mlima mkubwa. Mlima ulikuwa unazuia njia ya kijito hiki, hivyo kijito kikauomba mlima kwa sauti yake dhaifu na ndogo, "Tafadhali noamba kupita, umesimama kwenye njia yangu na umenizibia njia yangu kuendelea mbele." Basi mlima ukauliza, "Unakwenda wapi?" Swali ambalo kijito kililijibu, "Ninatafuta makazi yangu." Mlima ukasema, "Sawa, endelea na tiririkia juu yangu!" Lakini kwa sababu kijito kilikuwa dhaifu sana na kichanga sana, hakukuwa na namna kwake kutiririka juu ya mlima mkubwa hivyo, hivyo hakikuwa na uchaguzi bali kuendelea kutiririka chini ya mlima...
Upepo mkali ukavuma, ukiwa umekusanya mchanga na vumbi kuelekea ambapo milma ulikuwa umesimama. Upepo ukauungurumia mlima, "Hebu nipite!" Mlima ukauliza, "Unakwenda wapi?" Upepo ukavuma kwa kujibu, "Ninataka kwenda upande ule wa mlima." Mlima ukasema, "Sawa, kama unaweza kupenya katikati yangu, basi unaweza kwenda!"

Baada ya Kupoteza Hadhi Yangu …

 Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Wakristo

Umeme wa Mashariki | 3. Baada ya Kupoteza Hadhi Yangu …

Huimin Mji wa Jiaozuo, Mkoa wa Henan
Kila wakati nilipoona au kusikia kuhusu mtu aliyekuwa amebadilishwa naye kujisikia mwenye huzuni, dhaifu au mnunaji, na kutotaka kufuata tena, basi niliwaangalia kwa dharau. Nilidhani haikuwa kitu zaidi ya watu tofauti waliokuwa na majukumu tofauti ndani ya kanisa, kwamba hakukuwa na tofauti kati ya juu au chini, kwamba sote tulikuwa uumbaji wa Mungu na hakukuwa na sababu ya kuhuzunikia. Kwa hiyo kama nilikuwa nikiwatunza waumini wapya au kuongoza wilaya, sikuwahi kufikiri kuwa nilizingatia sana hadhi yangu, kwamba nilikuwa mtu wa aina hiyo. Singeweza kamwe kufikiri hata katika miaka milioni moja kwamba ningeonyesha tabia ya aibu kama hiyo wakati mimi mwenyewe nilipobadilishwa ...

4/24/2018

Umeme wa Mashariki | Ni Lazima Wale Wanaofaa Kukamilishwa Wapitie Usafishaji

Umeme wa Mashariki | Ni Lazima Wale Wanaofaa Kukamilishwa Wapitie Usafishaji

    Mwenyezi Mungu alisema, Kama unamwamini Mungu, ni lazima umtii Mungu, uweke ukweli katika vitendo na utimize wajibu wako wote. Zaidi ya hayo, ni lazima uelewe mambo unayopaswa kupitia. Ikiwa unapitia tu kushughulikiwa, kufundishwa nidhamu na hukumu, kama wewe unaweza tu kumfurahia Mungu, lakini huwezi kuhisi wakati Mungu anakufundisha nidhamu au kukushughulikia, hili halikubaliki. Labda katika wakati huu wa usafishaji unaweza kushikilia msimamo wako. Hii bado haitoshi; ni lazima uendelee mbele.

Umeme wa Mashariki | Ufafanuzi wa Tamko la Thelathini na Mbili

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Umeme wa Mashariki | Ufafanuzi wa Tamko la Thelathini na Mbili

Maneno ya Mungu huwaacha watu wakikuna vichwa vyao; ni kana kwamba, Anapozungumza, Mungu anaepukana na mwanadamu na kuzungumza na hewa, kana kwamba Hafikirii hata kidogo kuzingatia zaidi matendo ya mwanadamu, na Hatilii maanani kabisa kimo cha mwanadamu, kana kwamba maneno Anayozungumza hayaelekezwi kwa dhana za watu, lakini kuepukana na mwanadamu, kama lilivyokuwa kusudi la Mungu la asili. Kwa sababu nyingi sana, maneno ya Mungu hayaeleweki na mwanadamu hawezi kuyapenya. Hili halishangazi. Lengo la asili la maneno yote ya Mungu si kwa watu kupata ujuzi au ustadi kwayo; badala yake, ni njia moja kati ya zile Mungu ametumia kufanya kazi kutoka mwanzo hadi leo.

4/23/2018

Jinsi Upendo wa Mungu kwa Mwanadamu Ulivyo Muhimu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Upendo kwa Mungu

Umeme wa Mashariki | Wimbo wa Maneno ya Mungu

I
Mandhari iliyochorwa katika Biblia "Amri ya Mungu kwa Adamu"
ni ya kugusa na yenye kutia moyo.
Ingawa hiyo picha ina Mungu na mtu tu,
uhusiano kati ya hao wawili ni wa ndani sana
tunaanza kuhisi mshangao, mshangao na uvutiwaji.
II
Upendo wa Mungu unaofurika umepewa mwanadamu bure,
upendo wa Mungu umemzunguka.

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 1

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 1

Kama tu Mungu alivyosema, "Hakuna anayeweza kuelewa mzizi wa maneno Yangu, wala kusudi la maneno haya." Kama Isingekuwa uongozi wa Roho wa Mungu, kama isingekuwa kwa majilio ya maneno Yake, wote wangeangamia chini ya kuadibu Kwake. Ni kwa nini Mungu humjaribu mwanadamu kwa muda mrefu hivyo? Na kwa muda mrefu kama miezi mitano? Hili ndilo wazo la kulenga la ushirika wetu na vilevile wazo kuu katika hekima ya Mungu. Tunaweza kuchukulia kwamba: Isingekuwa jaribio hili, na bila Mungu kushambulia, kuua, na kuwatema binadamu wapotovu, ikiwa ujenzi wa kanisa ungeendelea mpaka leo, basi hilo lingefanikisha nini?

Sura ya 42. Kwa Kutafuta Ukweli Tu Ndio Unaweza Kupata Mabadiliko Katika Tabia Yako

Mwenyezi Mungu alisema, Kwa kutafuta ukweli tu ndipo utapata mabadiliko katika tabia yako: Hili ni jambo unalofaa kulielewa na kulielewa vizuri kabisa. Usipoelewa ukweli vya kutosha, utateleza kwa urahisi na kupotoka. Kutafuta kukua katika maisha lazima utafute ukweli katika kila kitu. Haijalishi suala gani laweza kutokea, lazima utafute kukumbana nalo katika njia inayopatana na ukweli, kwa sababu ukikumbana nayo kwa njia isiyo safi kabisa, basi unaenda kinyume na ukweli. Chochote ufanyacho, lazima kila wakati ufikirie thamani yake. Unaweza kufanya yale mambo yaliyo na maana na lazima usifanye mambo yasiyo na maana.

4/22/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kuhusu Maisha ya Petro

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kuhusu Maisha ya Petro

    Mwenyezi Mungu alisema, Petro ni mfano ambao Mungu aliutambulisha kwa wanadamu, na yeye ni mtu mashuhuri anayejulikana vizuri. Kwa nini mtu mnyonge kama huyo aliwekwa mahala kama mfano na Mungu na amesifiwa na vizazi vya baadaye? Bila shaka, ni wazi kwamba hili halitenganishwi na maonyesho yake na azimio lake la upendo kwa Mungu. Kuhusu wapi ambapo moyo wa Petro wa upendo kwa Mungu ulionyeshwa na kile ambacho uzoefu wake wa maishani ulivyokuwa kwa kweli, lazima turudi kwa Enzi ya Neema kutazama tena desturi za wakati huo, ili kumwona Petro wa enzi hiyo.
Petro alizaliwa katika nyumba ya kawaida ya wakulima wa Kiyahudi. Wazazi wake waliikimu familia yote kwa kufanya ukulima, naye alikuwa mzaliwa wa kwanza kati ya watoto wote; alikuwa na ndugu wanne.

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko la Ishirini na Nane

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

 Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko la Ishirini na Nane

Nilipokuja kutoka Zayuni, vitu vyote vilikuwa vimenisubiri, na Niliporudi Zayuni, Nilisalimiwa na wanadamu wote. Nilipokuja na kwenda, hatua Zangu hazikuwahi zuiliwa na vitu vilivyokuwa na uadui Kwangu, na kwa hivyo kazi Yangu iliendelea kwa utaratibu. Leo, Ninapokuja miongoni mwa viumbe vyote, vitu vyote vinanisalimu kwa kimya, kwa uoga mkuu kuwa Nitaondoka tena na Niondoe usaidizi kwao. Vitu vyote vinafuata uongozi Wangu, na vyote vinaangalia upande ulioashiriwa na mkono Wangu. Maneno ya kinywa Changu yamefanya kamili viumbe vingi na kuwaadibu wana wengi wa uasi Kwa hivyo, wanadamu wote wanaangalia maneno Yangu kwa makini, na kusikiza kwa karibu maneno ya kinywa Changu, na wanaogopa sana kupitwa na fursa hii nzuri.