Umeme wa Mashariki | Tamko la Thelathini na Tatu
Mwenyezi Mungu alisema, Katika nyumba Yangu, kulikuwapo wakati mmoja wale waliolisifu jina Langu takatifu, ambao walifanya kazi bila kuchoka ili utukufu Wangu duniani ungejaza anga. Kwa sababu ya hili, Nilifurahi sana, moyo Wangu ulijawa na furaha—lakini nani angeweza kufanya kazi badala Yangu, akiacha usingizi usiku na mchana? Azimio la mwanadamu mbele Yangu hunipa raha, lakini uasi wake huchochea hasira Yangu, na hivyo, kwa sababu mwanadamu hawezi kamwe kuzingatia wajibu wake, huzuni Yangu kwa ajili yake inakua kubwa zaidi.