9/04/2019

Mungu Mwenye Mwili Awaongoza Binadamu Kuingia Katika Enzi Mpya

Mungu Mwenye Mwili Awaongoza Binadamu Kuingia Katika Enzi Mpya

I

Mungu mwenye mwili, Anaitamatisha enzi
wakati tu mgongo wa Yehova ulionekana.
Pia Anahitimisha enzi ya imani
ambapo kutokuwa yakini kwa Mungu kulifikiriwa.
Kazi ya Mungu wa mwisho mwenye mwili
humleta mwanadamu katika enzi ya utendaji zaidi.
Kazi Anayofanya huwaleta binadamu wote
kwa wakati wa kupendeza na wa kweli zaidi.
Anatamatisha enzi ya udhahania,
Anatamatisha enzi ambapo mwanadamu
alitamani kuutafuta uso wa Mungu lakini hakuweza wakati huo.
Anatamatisha huduma ya mwanadamu kwa Shetani, mwanadamu anaongozwa hadi katika enzi mpya.
Yote haya yanafanikishwa na kazi ya Mungu katika mwili,
badala ya Roho wa Mungu pekee.

9/03/2019

Neno la Mungu "Je, Kazi ya Mungu ni Rahisi Jinsi Mwanadamu Anavyodhania?" (Official Video)



Maneno ya Mungu "Je, Kazi ya Mungu ni Rahisi Jinsi Mwanadamu Anavyodhania?"(Official Video)


Mwenyezi Mungu anasema, "Unapaswa kuona kuwa mapenzi Yake na kazi Yake si rahisi kama ilivyokuwa katika kuumba mbingu na nchi na vyote vilivyomo. Kwa sababu kazi ya leo ni kubadilisha wale waliopotoshwa, wale waliokufa ganzi, na kutakasa walioumbwa kisha kushughulikiwa na Shetani, si kuumba Adamu na Hawa, ama hata kuumba mwanga, ama aina yote ya mimea na wanyama. Kazi Yake sasa ni kutakasa wote waliopotoshwa na Shetani ili kwamba wamrejelee, wawe miliki Yake na wawe utukufu wake. Kazi kama ile si rahisi jinsi mwanadamu anavyofikiria kuhusu kuumbwa kwa mbingu na nchi na vilivyomo, wala si sawa na kumkemea Shetani aende katika shimo lisilo na mwisho, kama anayvodhania mwanadamu. Bali, ni kumbadilisha mtu, kubadili kilicho hasi kuwa chanya na kufanya kuwa miliki Yake ambacho si chake."

Iliyotazamwa Mara Nyingi: Umuhimu wa Kazi ya Mungu ya Maneno

9/02/2019

Latest Swahili Gospel Movie "Siri ya Utauwa: Mfuatano" | God is the Way, the Truth, and the Life




Lin Bo'en ni mhubiri mzee ambaye amemwani Bwana kwa miongo mingi. Tangu alipomkubali Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho, alihukumiwa, akatengwa, na akafukuzwa kutoka kwa jumuiya ya kidini na wachungaji na wazee wa kanisa, nguvu zinazompinga Kristo. Lakini ingawa Lin Bo’en alishambuliwa, akahukumiwa na kusingiziwa, hakusita kwa woga. Badala yake, imani yake ikawa thabiti zaidi kuliko ilivyowahi kuwa, na hili lilimwongoza kufahamu hatimaye kwamba wachungaji na wazee wa kanisa wa ulimwengu wa dini walikuwa wakiigiza kwa udanganyifu sura adilifu. 

9/01/2019

Best Christian Worship Songs Swahili | Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho



Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho


Mungu ndiye Mwanzo, Mungu ndiye Mwanzo, Mungu ndiye Mwanzo, na tena Mwisho, na tena Mwisho, na tena Mwisho. Mungu ndiye Mpanzi, Mungu ndiye Mpanzi, Mungu ndiye Mpanzi, na Mvunaji (Mvunaji). Mungu ndiye Mwanzo na Mwisho; Mungu ndiye Mpanzi na Mvunaji. Mungu ndiye Mwanzo na Mwisho; Mungu ndiye Mpanzi na Mvunaji. Mungu ndiye Mwanzo na Mwisho; Mungu ndiye Mpanzi na Mvunaji. Mungu Anakuwa mwili hasa kwa ajili ya kuikaribisha enzi mpya, na, kwa hakika, Anapoikaribisha enzi mpya, Atakuwa Ameikamilisha enzi ya kale wakati uo huo. 

Sauti ya Mungu | Sura ya 110

Kila kitu kitakapofichuliwa utakuwa wakati ambapo Nitapumzika, na hata zaidi, utakuwa wakati ambapo kila kitu kitakuwa sawa. Mimi hufanya kazi Yangu binafsi; Mimi hupanga kila kitu na kusafidi kila kitu Mwenyewe. Nitakapotoka Sayuni na Nitakaporejea, wazaliwa Wangu wa kwanza watakapokuwa wamekamilishwa na Mimi, Nitakuwa Nimemaliza kazi Yangu kubwa. Katika mawazo ya watu kitu ambacho kinafanywa ni sharti kiweze kuonekana na kuguswa, lakini jinsi Ninavyoona, kila kitu ni kikamilifu wakati ambapo Ninafanya mpango Wangu.

8/31/2019

Neno la Mungu | Sura ya 115


Neno la Mungu | Sura ya 115

Moyo Wangu utakufurahia mno, Nitacheza kwa furaha juu yako, na Nitakupa baraka zisizo na mwisho, kwa kuwa kabla ya uumbaji, ulitoka Kwangu, na leo lazima urejee upande Wangu, kwa kuwa wewe si wa dunia ama ulimwengu bali, badala yake, wewe ni Wangu. Nitakupenda milele, Nitakubariki milele na Nitakulinda milele. Ni wale tu ambao wametoka Kwangu wanaoyajua mapenzi Yangu, na ni wao tu wataudhukuru mzigo Wangu na kufanya kile ambacho Ninataka kukifanya.

8/30/2019

Wimbo wa Kuabudu | Ishara ya Tabia ya Mungu

Wimbo wa Kuabudu | Ishara ya Tabia ya Mungu

I
Tabia ya Mungu inajumuisha upendo Wake na faraja Yake kwa binadamu,
Tabia ya Mungu,
tabia ya Mungu ni kitu ambacho Mtawala wa viumbe vyote vinavyoishi
au kile ambacho Bwana wa uumbaji wote anacho.

8/29/2019

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | "Unapaswa Kushughulikiaje Wito Wako wa Mustakabali?"



Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | "Unapaswa Kushughulikiaje Wito Wako wa Mustakabali?"


Mwenyezi Mungu anasema, "Hata ingawa wamenusurika mpaka siku hii, ni nani angefikiri kuwa wamepewa sumu na yule mwovu kwa muda mrefu? Je, umesahau kuwa wewe ni mmoja wa waathiriwa? Kwa ajili ya upendo wako kwa Mungu, una nia ya kufanya kila uwezalo kuwaokoa walionusurika? Je, huna nia , ya kutumia nguvu zako zote kulipiza Mungu anayempenda binadamu kama nyama na damu Yake Mwenyewe? Unaitafsiri vipi hali ya kutumiwa na Mungu kuishi maisha yako yasiyo ya kawaida? Je, unao kweli uamuzi na matumaini ya kuishi kwa kudhihirisha maisha ya maana ya mtu mcha Mungu anayemtumikia Mungu?"

Dondoo Nyingine ya Filamu: 1. Ni jinsi gani mtu anafaa kuitambua sauti ya Mungu? Je, mtu anawezaje kuthibitisha kwamba Mwenyezi Mungu kweli ni Bwana Yesu aliyerudi?


8/28/2019

10. Kwa nini ni kwa kupitia na kuitii kazi ya Mungu mwenye mwili pekee ndipo mtu anaweza kumjua Mungu?

I. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Kupata Mwili kwa Mungu

10. Kwa nini ni kwa kupitia na kuitii kazi ya Mungu mwenye mwili pekee ndipo mtu anaweza kumjua Mungu?

Aya za Biblia za Kurejelea:
“Na Neno alifanywa kuwa mwili, na akakaa kati yetu, (nasi tukautazama utukufu wake, utukufu kama ule wa Mwana wa pekee aliyezaliwa na Baba,) aliyejawa neema na ukweli” (Yohana 1:14).

8/27/2019

Mama wa "Vijijini" Akutana na Binti Mkwe wa "Mjini"

Liu Jie, Hunan
Mama wa "Vijijini" Akutana na Binti Mkwe wa "Mjini"
Maoni Tofauti, Migongano Ya Siku Zote
Mimi ni mke wa kawaida, mke mzuri na mama mwenye upendo, mimi huwatunza vizuri mume wangu na watoto wangu, mimi hufanya kazi kwa bidii na mwekevu katika kuendesha nyumba yangu, na sijawahi kamwe kutumia fedha zangu bila hadhari. Lakini kitu kisichofikirika kilinifika. Mwanangu alimuoa msichana wa kisasa ambaye kwa kweli alipenda kujifurahisha na kuvaa na kufuata mitindo ya ulimwengu. Alifuatilia na kununua chochote kilichopendwa ulimwenguni, alipoteza pesa nyingi mno, na kiasi cha pesa alichopata kila mwezi ndicho kiasi alichotumia.

8/26/2019

“Kupita Katika Mtego” – Mtu Anaweza Kuokolewa kwa Kumwamini Bwana Katika Dini? | Filamu za Injili (Movie Clip 4/7)



“Kupita Katika Mtego” – Mtu Anaweza Kuokolewa kwa Kumwamini Bwana Katika Dini? | Filamu za Injili (Movie Clip 4/7)


Ndani ya dini, kuna watu wengi ambao wanaamini kwamba, ingawa wachungaji na wazee wanashikilia mamlaka katika ulimwengu wa dini na kutembea njia ya Mafarisayo wafiki, ingawa wanakubali na kuwafuata wachungaji na wazee, wanaamini katika Bwana Yesu, si katika wachungaji na wazee, hivyo basi inawezaje kusemwa kuwa njia wanayoyotembea pia ni ile ya Mafarisayo? Je, mtu kweli hawezi kuokolewa kwa kumwamini Mungu ndani ya dini?

Soma Zaidi: Kuna tofauti ipi kati ya maisha ya kanisa katika Enzi ya neema na maisha ya kanisa katika Enzi ya Ufalme?

8/25/2019

“Kupita Katika Mtego” – Jinsi Mungu Anavyomwokoa Mwanadamu Kutoka kwa Ushawishi wa Shetani | Filamu za Injili (Movie Clip 5/7)



“Kupita Katika Mtego” – Jinsi Mungu Anavyomwokoa Mwanadamu Kutoka kwa Ushawishi wa Shetani | Filamu za Injili (Movie Clip 5/7)


Biblia inasema, "Kwa maana muda umekuja ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu..." (1 Petro 4:17). Katika siku za mwisho, Mwenyezi Mungu anaonyesha ukweli wote unaomtakasa na kumwokoa mwanadamu na Anatuonyesha tabia Yake yenye haki, uadhama na isiyokosewa. Kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho imefanywa kumwokoa mwanadamu ili aweze kujinasua kutoka kwa ushawishi wa Shetani na kurudi kwa Mungu. 

8/24/2019

“Kupita Katika Mtego” – Kwa nini Chama cha Kikomunisti cha China Kinalitesa Kanisa la Mwenyezi Mungu | Filamu za Injili (Movie Clip 6/7)



“Kupita Katika Mtego” – Kwa nini Chama cha Kikomunisti cha China Kinalitesa Kanisa la Mwenyezi Mungu | Filamu za Injili (Movie Clip 6/7)


Chama cha Kikomunisti cha China ni serikali ya kishetani ambayo huchukia ukweli na Mungu. Kinajua kwamba Mwenyezi Mungu peke Yake katika ulimwengu ndiye Anayeweza kuonyesha ukweli. Mwenyezi Mungu yuko katika mchakato wa kufanya kazi ya wokovu wa siku za mwisho. Neno la Mwenyezi Mungu likienezwa kati ya watu, wale wote wanaopenda ukweli watarejea kwa Mwenyezi Mungu. Uso wa kishetani wa Chama cha Kikomunisti cha China, uso wake wa kweli, ambao huchukia ukweli na kumpinga Mungu utafunuliwa.