1. Ni jinsi gani mtu anafaa kuitambua sauti ya Mungu? Je, mtu anawezaje kuthibitisha kwamba Mwenyezi Mungu kweli ni Bwana Yesu aliyerudi?
“Kondoo wangu huisikia sauti yangu, na mimi Ninawajua, nao hunifuata” (Yohana 10:27).
“Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana hatazungumza juu yake mwenyewe; bali chochote atakachosikia, atakinena: na atawaonyesha mambo yajayo” (Yohana 16:12-13).
“Yeye aliye na sikio, na alisikie neno ambalo Roho aliyaambia makanisa” (Ufunuo 2:7).
“Tazama, Simba wa kabila ya Yuda, Shina lake Daudi, ameweza kukifungua hicho kitabu, na kuzitoa muhiri saba zilizoko” (Ufunuo 5:5).