8/31/2019

Neno la Mungu | Sura ya 115


Neno la Mungu | Sura ya 115

Moyo Wangu utakufurahia mno, Nitacheza kwa furaha juu yako, na Nitakupa baraka zisizo na mwisho, kwa kuwa kabla ya uumbaji, ulitoka Kwangu, na leo lazima urejee upande Wangu, kwa kuwa wewe si wa dunia ama ulimwengu bali, badala yake, wewe ni Wangu. Nitakupenda milele, Nitakubariki milele na Nitakulinda milele. Ni wale tu ambao wametoka Kwangu wanaoyajua mapenzi Yangu, na ni wao tu wataudhukuru mzigo Wangu na kufanya kile ambacho Ninataka kukifanya.

8/30/2019

Wimbo wa Kuabudu | Ishara ya Tabia ya Mungu

Wimbo wa Kuabudu | Ishara ya Tabia ya Mungu

I
Tabia ya Mungu inajumuisha upendo Wake na faraja Yake kwa binadamu,
Tabia ya Mungu,
tabia ya Mungu ni kitu ambacho Mtawala wa viumbe vyote vinavyoishi
au kile ambacho Bwana wa uumbaji wote anacho.

8/29/2019

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | "Unapaswa Kushughulikiaje Wito Wako wa Mustakabali?"



Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | "Unapaswa Kushughulikiaje Wito Wako wa Mustakabali?"


Mwenyezi Mungu anasema, "Hata ingawa wamenusurika mpaka siku hii, ni nani angefikiri kuwa wamepewa sumu na yule mwovu kwa muda mrefu? Je, umesahau kuwa wewe ni mmoja wa waathiriwa? Kwa ajili ya upendo wako kwa Mungu, una nia ya kufanya kila uwezalo kuwaokoa walionusurika? Je, huna nia , ya kutumia nguvu zako zote kulipiza Mungu anayempenda binadamu kama nyama na damu Yake Mwenyewe? Unaitafsiri vipi hali ya kutumiwa na Mungu kuishi maisha yako yasiyo ya kawaida? Je, unao kweli uamuzi na matumaini ya kuishi kwa kudhihirisha maisha ya maana ya mtu mcha Mungu anayemtumikia Mungu?"

Dondoo Nyingine ya Filamu: 1. Ni jinsi gani mtu anafaa kuitambua sauti ya Mungu? Je, mtu anawezaje kuthibitisha kwamba Mwenyezi Mungu kweli ni Bwana Yesu aliyerudi?


8/28/2019

10. Kwa nini ni kwa kupitia na kuitii kazi ya Mungu mwenye mwili pekee ndipo mtu anaweza kumjua Mungu?

I. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Kupata Mwili kwa Mungu

10. Kwa nini ni kwa kupitia na kuitii kazi ya Mungu mwenye mwili pekee ndipo mtu anaweza kumjua Mungu?

Aya za Biblia za Kurejelea:
“Na Neno alifanywa kuwa mwili, na akakaa kati yetu, (nasi tukautazama utukufu wake, utukufu kama ule wa Mwana wa pekee aliyezaliwa na Baba,) aliyejawa neema na ukweli” (Yohana 1:14).

8/27/2019

Mama wa "Vijijini" Akutana na Binti Mkwe wa "Mjini"

Liu Jie, Hunan
Mama wa "Vijijini" Akutana na Binti Mkwe wa "Mjini"
Maoni Tofauti, Migongano Ya Siku Zote
Mimi ni mke wa kawaida, mke mzuri na mama mwenye upendo, mimi huwatunza vizuri mume wangu na watoto wangu, mimi hufanya kazi kwa bidii na mwekevu katika kuendesha nyumba yangu, na sijawahi kamwe kutumia fedha zangu bila hadhari. Lakini kitu kisichofikirika kilinifika. Mwanangu alimuoa msichana wa kisasa ambaye kwa kweli alipenda kujifurahisha na kuvaa na kufuata mitindo ya ulimwengu. Alifuatilia na kununua chochote kilichopendwa ulimwenguni, alipoteza pesa nyingi mno, na kiasi cha pesa alichopata kila mwezi ndicho kiasi alichotumia.

8/26/2019

“Kupita Katika Mtego” – Mtu Anaweza Kuokolewa kwa Kumwamini Bwana Katika Dini? | Filamu za Injili (Movie Clip 4/7)



“Kupita Katika Mtego” – Mtu Anaweza Kuokolewa kwa Kumwamini Bwana Katika Dini? | Filamu za Injili (Movie Clip 4/7)


Ndani ya dini, kuna watu wengi ambao wanaamini kwamba, ingawa wachungaji na wazee wanashikilia mamlaka katika ulimwengu wa dini na kutembea njia ya Mafarisayo wafiki, ingawa wanakubali na kuwafuata wachungaji na wazee, wanaamini katika Bwana Yesu, si katika wachungaji na wazee, hivyo basi inawezaje kusemwa kuwa njia wanayoyotembea pia ni ile ya Mafarisayo? Je, mtu kweli hawezi kuokolewa kwa kumwamini Mungu ndani ya dini?

Soma Zaidi: Kuna tofauti ipi kati ya maisha ya kanisa katika Enzi ya neema na maisha ya kanisa katika Enzi ya Ufalme?

8/25/2019

“Kupita Katika Mtego” – Jinsi Mungu Anavyomwokoa Mwanadamu Kutoka kwa Ushawishi wa Shetani | Filamu za Injili (Movie Clip 5/7)



“Kupita Katika Mtego” – Jinsi Mungu Anavyomwokoa Mwanadamu Kutoka kwa Ushawishi wa Shetani | Filamu za Injili (Movie Clip 5/7)


Biblia inasema, "Kwa maana muda umekuja ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu..." (1 Petro 4:17). Katika siku za mwisho, Mwenyezi Mungu anaonyesha ukweli wote unaomtakasa na kumwokoa mwanadamu na Anatuonyesha tabia Yake yenye haki, uadhama na isiyokosewa. Kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho imefanywa kumwokoa mwanadamu ili aweze kujinasua kutoka kwa ushawishi wa Shetani na kurudi kwa Mungu. 

8/24/2019

“Kupita Katika Mtego” – Kwa nini Chama cha Kikomunisti cha China Kinalitesa Kanisa la Mwenyezi Mungu | Filamu za Injili (Movie Clip 6/7)



“Kupita Katika Mtego” – Kwa nini Chama cha Kikomunisti cha China Kinalitesa Kanisa la Mwenyezi Mungu | Filamu za Injili (Movie Clip 6/7)


Chama cha Kikomunisti cha China ni serikali ya kishetani ambayo huchukia ukweli na Mungu. Kinajua kwamba Mwenyezi Mungu peke Yake katika ulimwengu ndiye Anayeweza kuonyesha ukweli. Mwenyezi Mungu yuko katika mchakato wa kufanya kazi ya wokovu wa siku za mwisho. Neno la Mwenyezi Mungu likienezwa kati ya watu, wale wote wanaopenda ukweli watarejea kwa Mwenyezi Mungu. Uso wa kishetani wa Chama cha Kikomunisti cha China, uso wake wa kweli, ambao huchukia ukweli na kumpinga Mungu utafunuliwa.

8/23/2019

Maisha ya Kikristo: Huenda Nisiwe Tajiri, lakini Nina Bahati Sana

Maisha ya Kikristo: Huenda Nisiwe Tajiri, lakini Nina Bahati Sana

Na Bong, Philippines
Nataka Kuwa Tajiri
“Mwalimu mkuu, tafadhali mpe mwanangu fursa na kumruhusu afanye mtihani!” Macho ya mama yangu yalimsihi mwalimu mkuu alipokuwa akizungumza kwa sauti ya kutetemeka kidogo.
Bila kuonyesha hisia, mwalimu mkuu akasema, “Hapana, shule ina kanuni. Mtoto anaweza kufanya mtihani tu wakati ada ya mtihani imelipwa!”

8/22/2019

Video za Kikristo | "Kaa Mbali na Shughuli Zangu" | Christ Is My Lord and My God



Video za Kikristo | "Kaa Mbali na Shughuli Zangu" | Christ Is My Lord and My God


Li Qingxin ni mhubiri katika kanisa la nyumba nchini Uchina ambaye amekuwa mwaminifu kwa Bwana kwa miaka mingi. Siku zote kwa shauku kubwa anaifanya kazi ya Bwana ya kuieneza injili, akisubiri kwa uangalifu kuja kwa Bwana ili amlete hadi kwenye ufalme wa mbinguni. Katika miaka ya hivi majuzi, Li Qingxin amegundua kwamba vikundi na makanisa mbalimbali yamekuwa na ukiwa zaidi. Umeme wa Mashariki, hata hivyo, limekuwa la kusisimua zaidi, licha ya shutuma na mateso mengi yenye mhemko kutoka kwa serikali ya Kikomunisti ya Uchina na jamii ya dini. Kondoo wazuri zaidi na zaidi na kondoo viongozi wa madhehebu na vikundi mbalimbali wamekubali Umeme wa Mashariki. 

8/21/2019

2018 Gospel Music "Mungu Kuutawala Mwanzo na Mustakabali wa Wanadamu" (Swahili Subtitles)


2018 Gospel Music "Mungu Kuutawala Mwanzo na Mustakabali wa Wanadamu" (Swahili Subtitles)


Kutoka wakati tunapoingia ulimwenguni tukilia kwa huzuni, sisi huanza kutekeleza majukumu tofauti katika maisha. Sisi husogea kutoka kuzaliwa hadi ugonjwa hadi uzee hadi kifo; sisi huenda kati ya furaha na huzuni…. Wnadamu hasa hutoka wapi, na kwa kweli tutaenda wapi? Ni nani aliyeudhibiti mwanzo wa mwanadamu, na ni nani huamuru mustakabali wake? Leo, yote yatafichuliwa …

Tazama Video: Mungu Amekuja Mungu Ametawala | "Kwaya ya Injili ya Kichina Onyesho la 18"

8/20/2019

Matamshi ya Mungu | Sura ya 83

Hujui kwamba Mimi ni Mwenyezi Mungu; hujui kwamba mambo yote na vitu vyote viko chini ya udhibiti Wangu! Maana ya kila kitu huumbwa na kukamilishwa na Mimi ni nini? Baraka au misiba ya kila mtu hutegemea utimilifu Wangu, matendo Yangu. Mwanadamu anaweza kufanya nini? Mwanadamu anaweza kufanikisha nini kwa kufikiri? Katika enzi hii ya mwisho, katika enzi hii potovu, katika dunia hii ya giza ambayo Shetani ameipotosha sana, ni kina nani wachache ambao wako jinsi Nipendavyo? Ikiwa ni leo, jana, au katika siku zijazo zisizo mbali, maisha ya kila mtu huamuliwa na Mimi. 

8/19/2019

Wimbo wa Kuabudu "Niko Tayari Kutekeleza Wajibu Wangu kwa Uaminifu" | God Is My Salvation


Wimbo wa Kuabudu "Niko Tayari Kutekeleza Wajibu Wangu kwa Uaminifu" | God Is My Salvation


Mpendwa Mwenyezi Mungu, ni Wewe ndiye Unayenipenda,
uliniinua kutoka kwa rundo la kinyesi hadi kwa mazoezi ya ufalme.
Maneno Yako yamenitakasa,
yakanifanya nianze kuishi maisha ya furaha.
Moyoni mwangu nahisi, kwa kweli, ni upendo Wako mkuu.
Aa … aa … aa … aa … Mpendwa Mwenyezi Mungu!
Maneno Yako yote ni ukweli.
Unastahili upendo wa binadamu.
Ee Mungu! Ukipuuza uasi wangu wa zamani,
Unanijali na kufanya kazi kuniokoa.
Unaniongoza katika njia ya kweli,
Ukitazama kila wakati katika upande wangu,
natarajia tu nitakua na kuwa mtu mpya.