9/30/2019

2019 Swahili Gospel Worship song | "Toa Akili na Mwili ili Kutimiza Agizo la Mungu" (Lyrics Video)



2019 Swahili Gospel Worship song | "Toa Akili na Mwili ili Kutimiza Agizo la Mungu" (Lyrics Video)


I

Kama washiriki wa jamii ya wanadamu,
kama wafuasi wa Kristo wa dhati,
ni wajibu wetu, ni jukumu letu
kutoa akili zetu na miili yetu
kwa kutimiza agizo la Mungu.
Kwa maana asili yetu yote ilitoka kwa Mungu,
na twaishi, kwa ajili ya ukuu Wake.
Kwa maana asili yetu, ilitoka kwa Mungu,
na twaishi, kwa ajili ya ukuu Wake.

9/29/2019

Neno la Mungu | Sura ya 108

Neno la Mungu | Sura ya 108

Ndani Yangu, wote wanaweza kupata raha na wote wanaweza kuwa huru. Wale walio nje Yangu hawawezi kupata uhuru na furaha kwa sababu Roho Wangu hayuko pamoja na watu hawa. Watu hawa wanaitwa wafu wasio na roho. Nami Nawaita wale walio ndani Yangu watu walio hai wenye roho. Wao ni Wangu, na watarudi kwenye kiti Changu cha enzi. Wale ambao hutoa huduma na wale ambao ni wa ibilisi ni wafu wasio na roho, nao wanapaswa kuangamizwa hadi wawe katika hali ya kutokuwepo.

9/28/2019

3. Ni lazima mtu atambue tofauti kati ya njia ya toba katika Enzi ya Neema na njia ya uzima wa milele katika siku za mwisho

VII. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Kwamba ni Kile tu Ambacho Kristo wa Siku za Mwisho Analeta Kilicho Njia ya Uzima wa Milele


3. Ni lazima mtu atambue tofauti kati ya njia ya toba katika Enzi ya Neema na njia ya uzima wa milele katika siku za mwisho


Aya za Biblia za Kurejelea:

“Na iwapo mtu yeyote atayasikia maneno yangu, na asiyaamini, Mimi sitamhukumu: kwa kuwa mimi sikuja ili niihukumu dunia, bali kuiokoa dunia. Yeye ambaye ananikataa mimi, na hayakubali maneno yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho” (Yohana 12:47-48).

9/27/2019

“Kumbukumbu Chungu” – Ni Vigezo Vipi vya Kuingia Kwenye Ufalme wa Mbinguni? | Filamu za Kikristo (Movie Clip 2/5)



“Kumbukumbu Chungu” – Ni Vigezo Vipi vya Kuingia Kwenye Ufalme wa Mbinguni? | Filamu za Kikristo (Movie Clip 2/5)


Kuhusiana na ni mtu aina gani anayeweza kuingia kwenye ufalme wa mbinguni, Bwana Yesu alisema, "ila yule atendaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni" (Mathayo 7:21). Kwa hivyo ni mtu aina gani hasa anayefanya mapenzi ya Baba wa mbinguni? Watu wengi husadiki kwamba wale wanaofuata mfano wa Paulo na kufanya kazi kwa uangalifu na bidii nyingi kwa ajili ya Bwana ndio wanaofanya mapenzi ya Baba wa mbinguni. Kisha kunao wale wanaosadiki kwamba wale ambao wanampenda Mungu pekee kwa moyo wao wote, akili na nafsi, ambao hawatendi dhambi tena na wamefikia utakaso, ndio wanaofanya mapenzi ya Baba wa mbinguni. Hivyo ni nani aliye sahihi na nani asiye sahihi kutokana na mitazamo hii miwili? Tafadhali tazama pande zote mbili zikishiriki katika majadiliano makali!

9/26/2019

“Wimbo wa Ushindi” – Jinsi ya Kugundua Mafarisayo wa Kisasa | Swahili Gospel Movie Clip 2/7



Wakati Bwana Yesu alikuja kufanya kazi Yake, mkuu wa ulimwengu wa dini alimshutumu na kumhukumu, na hatimaye wakaungana na serikali ya Kirumi kumsulubisha. Siku hizi mwenendo wa dhambi wa wale walio katika ulimwengu wa kidini ambao humpinga Mwenyezi Mungu ni sawa na maneno na matendo ya kutisha ya Wayahudi waliompinga Bwana Yesu wakati huo. Kwa nini hili liko hivi? Unajua sababu ya msingi ya kwa nini wanampinga Mungu? Je, unataka kuelewa kiini chao? Basi tazama video hii!

Sehemu Vita vya kiroho ni mkusanyiko wa ushuhuda wa Wakristo ambao walishindwa Shetani katika vita vya kiroho chini ya uongozi wa maneno ya Mungu baada ya kukubali wokovu wa Mungu wa siku za mwisho.

9/25/2019

“Wimbo wa Ushindi” – Je, Bwana Atatokeaje na Kufanya Kazi Yake Wakati Atakaporudi? | Swahili Gospel Movie Clip 1/7



“Wimbo wa Ushindi” – Je, Bwana Atatokeaje na Kufanya Kazi Yake Wakati Atakaporudi? | Swahili Gospel Movie Clip 1/7


Ishara ya maafa makubwa wakati wa siku za mwisho- miezi minne ya damu imetokea na nyota za angani zimechukua kuonekana kwa ajabu; maafa makubwa yanakaribia, na wengi wa wale walio na imani katika Bwana wamepata hisia ya kurudi Kwake kwa pili au kwamba tayari Amewasili. Wakati wote wanasubiri kuja kwa mara ya pili kwa Bwana kwa hamu kubwa, labda tumefikiria juu ya maswali yafuatayo: Je, Bwana ataonekanaje kwa mwanadamu Atakaporudi katika siku za mwisho? Je, ni kazi gani ambayo Bwana atafanya wakati Atakapokuja tena? Je, unabii wa hukumu ya kiti kikuu cheupe cha enzi kutoka Kitabu cha Ufunuo utatimizwaje hasa? Video hii fupi itafunua majibu kwako!

9/24/2019

Neno la Mungu | Sura ya 12

Ikiwa una tabia ambayo si thabiti, nyepesi kuhamaki kama upepo au mvua, kama huwezi kuendelea kusonga mbele, basi fimbo Yangu haitakuwa mbali na wewe. Unaposhughulikiwa, kadiri hali ilivyo mbaya zaidi, na kadiri unavyoteswa zaidi, ndivyo upendo wako kwa Mungu unavyoongezeka, na unaacha kushikilia dunia. Bila njia nyingine, unakuja Kwangu, na unapata tena nguvu na imani yako. Ilhali, katika hali rahisi, ungeboronga. Ni lazima uingie ndani kwa mtazamo chanya, uwe mwenye vitendo na si baridi.

9/23/2019

Wale Ambao Mungu Atawaokoa ni wa Kwanza Kabisa Moyoni Mwake

Wale Ambao Mungu Atawaokoa ni wa Kwanza Kabisa Moyoni Mwake

I
Kazi ya Mungu ya kuokoa ni muhimu vipi,
muhimu zaidi kuliko vitu vingine vyote Kwake.
Kwa mipango na mapenzi yaliyokusudiwa, sio mawazo na maneno tu,
Anafanya kila kitu kwa wanadamu wote.
Oh ni muhimu kiasi gani, kazi ya Mungu ya kuokoa, kwa ajili ya mwanadamu na Yeye Mwenyewe.
Jinsi gani Mungu anajishughulisha, ni juhudi gani Anayofanya.
Anasimamia kazi Yake, anatawala vyote, watu wote.
Hajawahi kuonekana kabla, kwa gharama kubwa sana.

9/22/2019

2. Kuna tofauti ipi kati ya jinsi ambavyo Bwana Yesu alifanya kazi katika Enzi ya Neema na jinsi Mwenyezi Mungu anavyofanya katika Enzi ya Ufalme?

V. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Tofauti Kati ya Kazi ya Mungu ya Hukumu Katika Siku za Mwisho na Kazi Yake ya Ukombozi Katika Enzi ya Neema

2. Kuna tofauti ipi kati ya jinsi ambavyo Bwana Yesu alifanya kazi katika Enzi ya Neema na jinsi Mwenyezi Mungu anavyofanya katika Enzi ya Ufalme?

Maneno Husika ya Mungu:
Wakati wa kupata mwili Kwake mara ya kwanza, ilikuwa muhimu kwa Mungu kuponya wagonjwa na kufukuza mapepo kwa sababu kazi Yake ilikuwa ni kukomboa. Ili kulikomboa kabila lote la mwanadamu, Alipaswa kuwa mwenye upendo na mwenye kusamehe. Kazi Aliyoifanya kabla ya kusulubiwa ilikuwa kuponya watu na kufukuza mapepo, ambayo iliashiria wokovu Wake wa mwanadamu kutoka katika dhambi na uchafu.

9/21/2019

“Kumbukumbu Chungu” – Uhusiano Kati ya Hukumu katika Siku za Mwisho na Kuingia kwenye Ufalme wa Mbinguni? | Filamu za Kikristo (Movie Clip 5/5)



“Kumbukumbu Chungu” – Uhusiano Kati ya Hukumu katika Siku za Mwisho na Kuingia kwenye Ufalme wa Mbinguni? | Filamu za Kikristo (Movie Clip 5/5)


Katika ulimwengu wa kidini, kunao wengi wanaosadiki kwamba mradi tu wanahifadhi jina la Bwana, kusadiki kabisa katika ahadi ya Bwana na kufanya kazi kwa uangalifu na bidii nyingi kwa ajili ya Bwana, wakati Atarudi wanaweza kunyakuliwa na kuingia kwenye ufalme wa mbinguni. Je, yeyote anaweza kuingia kwenye ufalme wa mbinguni kwa kumsadiki Bwana kwa njia hii? Ni nini kitatufanyikia kama tusipoikubali kazi ya hukumu ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho?

9/20/2019

"Mazungumzo" – Upingaji wa Ajabu wa Mkristo wa Mawazo ya Mchungaji wa Utatu | Swahili Christian Video Clip 5/6


"Mazungumzo" – Upingaji wa Ajabu wa Mkristo wa Mawazo ya Mchungaji wa Utatu | Swahili Christian Video Clip 5/6


CCP kinamkaribisha mchungaji na Kanisa la Utatu kujaribu kumtia kasumba na kumbadilisha Mkristo mmoja. Huyu Mkristo na mchungaji wanafungua mjadala mzuri katika kukabiliana na dhana zilizotolewa na mchungaji wa Utatu. Je, Mkristo huyu atampingaje huyu mchungaji? Kwa nini jaribio hili la CCP katika kutia kasumba na ubadilishaji utaishia kushindwa?

Zaidi: 1. Ni jinsi gani mtu anafaa kuitambua sauti ya Mungu? Je, mtu anawezaje kuthibitisha kwamba Mwenyezi Mungu kweli ni Bwana Yesu aliyerudi?

9/19/2019

"Mazungumzo" – Kuitii Serikali Inayotawala Sio Sawa na Kumtii Mungu | Swahili Christian Video Clip 4/6




"Mazungumzo" – Kuitii Serikali Inayotawala Sio Sawa na Kumtii Mungu | Swahili Christian Video Clip 4/6


Ili kumdanganya na kumjaribu Mkristo mmoja kumtelekeza Mungu, CCP kilimwita mchungaji mmoja wa Kanisa la Utatu kumtia kasumba, na Mkristo huyu na mchungaji wakazua mjadala mzuri juu ya maneno ya Paulo: "Acha kila nafsi itii mamlaka ya juu zaidi. Kwani hakuna mamlaka isipokuwa ya Mungu: mamlaka yaliyoko yameamriwa na Mungu" (Warumi 13:1). Fasiri zao tofauti ni zipi za maneno haya? Mchungaji wa Utatu yuko chini ya CCP na huchukua njia ya Kanisa la Utatu—kwa kweli ni kusudi gani la siri liko hapo? Mkristo atakanaje hoja hii ya mchungaji "kuwa chini ya mamlaka ya juu"?


Iliyotazamwa Mara Nyingi: Filamu za Kikristo | "Mazungumzo" | Christian Testimony of Overcoming Satan

9/18/2019

2. Ni lazima mtu aelewe kwamba ukweli wote ulioonyeshwa na Mungu katika siku za mwisho ndio njia ya uzima wa milele

VII. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Kwamba ni Kile tu Ambacho Kristo wa Siku za Mwisho Analeta Kilicho Njia ya Uzima wa Milele

2. Ni lazima mtu aelewe kwamba ukweli wote ulioonyeshwa na Mungu katika siku za mwisho ndio njia ya uzima wa milele

Aya za Biblia za Kurejelea:
Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana hatazungumza juu yake mwenyewe; bali chochote atakachosikia, atakinena: na atawaonyesha mambo yajayo” (Yohana 16:12-13).