maandiko ya Biblia,neno la mungu |
Umeme wa Mashariki | Kuhusu Biblia (4)
Biblia inaandika masuala ya Israeli na matendo ya watu wake wateule wakati huo. Kwa maneno mengine, ni maelezo ya masuala ya Yehova, ambayo kwayo Roho Mtakatifu hatoi lawama. Ingawa kulikuwa na uteuzi wa sehemu za kujumuisha au kuondolewa, ingawa Roho Mtakatifu hathibitishi, bado Hatoi lawama. Biblia si kitu chochote zaidi ya historia ya Israeli na kazi ya Mungu. Watu, masuala, na mambo inayoyarekodi yote yalikuwa ya kweli, na hakuna kitu kuhusu hayo kilikuwa ni ishara ya maisha ya baadaye—mbali na unabii wa Isaya na Danieli, au kitabu cha Yohana cha maono. Watu wa awali wa Israeli walikuwa wenye maarifa na watu wenye utamaduni wa hali ya juu, na maarifa yao ya kale na utamaduni ulikuwa wa kiwango cha juu, na hivyo kile walichoandika kilikuwa cha kiwango cha juu kuliko watu wa leo.