Miaka elfu mbili iliyopita, wakati Bwana Yesu alipotokea na kufanya kazi, Mafarisayo walikwamia sheria na kukashifu kazi Yake, wakisema kuwa kazi Yake ilienda zaidi ya Maandiko.Ili kulinda hali zao na maisha yao, walijitahidi kwa nguvu zao zote ili kuwazuia watu kutafuta kazi ya Bwana Yesu, na kujiunga na serikali ya Kirumi kumsulubisha msalabani.
Maneno Husika ya Mungu:
Maana ya kupata mwili ni kwamba Mungu Anajionyesha katika mwili, na Anakuja kufanya kazi miongoni mwa wanadamu wa uumbaji Wake katika umbo la mwili. Hivyo, ili Mungu kuwa mwili, ni lazima kwanza Apate umbo la mwili, mwili wenye ubinadamu wa kawaida; hili ndilo hitaji la kimsingi zaidi. Kwa kweli, maana ya kupata mwili kwa Mungu ni kwamba Mungu Anaishi na kufanya kazi katika mwili, Mungu katika kiini Chake Anakuwa mwili, Anakuwa mwanadamu. Maisha Yake ya kimwili na kazi vinaweza kugawanywa katika hatua mbili. Kwanza ni maisha Anayoishi kabla ya kuanza kutekeleza huduma Yake.