Mwenyezi Mungu alisema, Mpango Wangu mzima wa usimamizi, ambao una urefu wa miaka elfu sita, unashirikisha awamu tatu, au enzi tatu: Kwanza, Enzi ya Sheria; pili, Enzi ya Neema (ambayo pia ni enzi ya Ukombozi); na mwisho, Enzi ya Ufalme. Kazi Yangu katika enzi hizi tatu hutofautiana katika maudhui kulingana na asili ya kila enzi, lakini katika kila hatua huambatana na mahitaji ya mwanadamu—au, sahihi zaidi, inafanywa kulingana na ujanja ambao Shetani anatumia katika vita Vyangu dhidi yake. Madhumuni ya Kazi Yangu ni kumshinda Shetani, ili kutoa wazi hekima Yangu na kudura, kufichua ujanja wote wa Shetani na hivyo kuokoa wanadamu wote, wanaoishi chini ya miliki yake.
"Mungu anatekeleza hatua ya kazi kubwa kila wakati yeye hujifunua. Kazi hii ni tofauti na ile ya enzi mwingine yoyote. Haiwezi kufikiriwa na mtu, na haijawahi kujifunza na mwanadamu. Ni kazi ambayo huanza enzi mpya na huhitimisha enzi, na ni aina mpya ya kazi kwa ajili ya wokovu wa wanadamu; Zaidi ya hayo, ni kazi ya kuwaleta wanadamu katika wakati mpya. Hiyo ni umuhimu wa kuonekana kwa Mungu. kutoka kwa Neno Laonekana Katika Mwili"
11/20/2017
Video za Kikristo | Kuelezea Wazi Uhusiano Kati ya Biblia na Mungu | "Biblia na Mungu" (Swahili Subtitles)
Video za Kikristo | Kuelezea Wazi Uhusiano Kati ya Biblia na Mungu | "Biblia na Mungu" (Swahili Subtitles)
Liu Zhizhong ni mzee katika kanisa moja la mtaani la nyumba nchini China. Amekuwa muumini kwa zaidi ya miaka 30, na amesisitiza bila kukoma kwamba “Biblia ni ufunuo wa Mungu,” “Biblia inamwakilisha Mungu, kuamini katika Mungu ni kuamini katika Biblia, kuamini katika Biblia ni kuamini katika Mungu.” Moyoni mwake, Biblia ni kuu. Kwa sababu ya upendo na imani yake pofu katika Biblia, hajawahi kutafuta au kuitazama kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho. Hadi siku moja, alipowazuia waumini kusoma maneno ya Mwenyezi Mungu mtandaoni, akawa na fursa ya kukutana na wahubiri kutoka katika Kanisa la Mwenyezi Mungu.
11/19/2017
Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani
Umeme wa Mashariki | Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani |
Mwenyezi Mungu alisemai ,Nyinyi nyote mna furaha kupokea tuzo mbele ya Mungu na kutambuliwa na Mungu. Haya ni matakwa ya kila mtu baada ya yeye kuanza kuwa na imani kwa Mungu, kwani mwanadamu kwa moyo wake wote hutafuta mambo yaliyo juu na hakuna aliye tayari kubaki nyuma ya wengine. Hii ndiyo njia ya mwanadamu. Kwa sababu hii, wengi kati yenu wanajaribu daima kupata neema ya Mungu mbinguni, lakini kwa kweli, uaminifu wenu na uwazi kwa Mungu ni wa kiasi kidogo sana ukilinganishwa na uaminifu na uwazi wenu kwenu wenyewe.Mbona Nasema hivi? Kwa sababu Sikiri uaminifu wenu kwa Mungu kabisa, na zaidi Nakana kuwepo kwa Mungu ndani ya mioyo yenu.
Kujadili Maisha ya Kanisa na Maisha Halisi
Umeme wa Mashariki | Kujadili Maisha ya Kanisa na Maisha Halisi |
Mwenyezi Mungu alisema, Watu huhisi kuwa wao wanaweza tu kubadilika katika maisha yao ya kanisani, na kuwa iwapo hawaishi ndani ya kanisa, mbadiliko hauwezekani, kuwa hawawezi kutimiza mbadiliko katika maisha yao halisi. Mwaweza kutambua suala hili ni lipi? Nimeongea juu ya kumleta Mungu katika maisha halisi, na hii ndiyo njia kwa wale wanaomwamini Mungu kuingia katika uhalisi wa maneno ya Mungu. Kwa kweli, maisha ya kanisa ni njia ndogo tu ya kuwakamilisha watu. Mazingira ya msingi ya kuwakamilisha wanadamu bado ni maisha halisi. Hiki ndicho kitendo halisi na mafunzo halisi Niliyozungumzia, yanayowaruhusu wanadamu kutimiza maisha ya ubinadamu wa kawaida na kuishi kwa kudhihirisha mfano wa mtu wa kweli katika maisha ya kila siku. Kipengele kimoja ni kwamba mtu lazima aelimike ili kuinua kiwango chake mwenyewe cha elimu, aweze kuelewa maneno ya Mungu, na kutimiza uwezo wa kuelewa.
11/18/2017
Tofauti Muhimu Kati ya Mungu Aliyepata Mwili na Wanadamu Wanaotumiwa na Mungu
Kwa miaka mingi Roho wa Mungu Amekuwa Akifanya kazi kwa kutafuta duniani. Kwa enzi nyingi Mungu Ametumia wanadamu wengi kufanya kazi Yake. Hata hivyo Roho wa Mungu bado hana mahali pazuri pa kupumzika. Kwa hivyo Mungu hupitia wanadamu mbalimbali kufanya kazi Yake na kwa kiasi kikubwa hutumia wanadamu kufanya hivyo. Yaani, katika miaka hii yote mingi, kazi ya Mungu haijawahi kusimama. Inaendelezwa mbele kupitia mwanadamu, bila kikomo mpaka siku ya leo. Ingawa Mungu Amesema na Ametenda mengi, mwanadamu bado hamjui Mungu, hii ni kwa sababu Mungu hajawahi kuonekana na mwanadamu na Yeye Hana umbo.
11/17/2017
Umeme wa Mashariki | Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea
Matamshi ya Mwenyezi Mungu - "Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea" |
Matamshi ya Mwenyezi Mungu - "Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea"
Watu wengi wanamwamini Mungu kwa ajili ya hatima yao ya baadaye au kwa ajili ya starehe ya muda mfupi. Kwa wale ambao hawajapitia ushughulikiaji wowote, imani kwa Mungu ni kwa ajili ya kuingia mbinguni, ili kupata tuzo. Sio ili kufanywa wawe na ukamilifu, au kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu. Ambayo ni kusema kwamba watu wengi hawamwamini Mungu ili watimize majukumu yao, au kukamilisha wajibu wao. Mara chache watu humwamini Mungu ili waishi maisha ya maana, wala hamna wale ambao wanaamini kwamba kwa kuwa mwanadamu yu hai, anapaswa ampende Mungu kwa kuwa ni sheria ya Mbinguni na kanuni ya dunia kufanya hivyo, na ni wito wa asili wa mwanadamu.
标签:
Baraka,
Injili,
Kristo,
Kupata-Mwili,
Kupata-Tuzo,
Kupata-Upendo,
Mafanikio,
Makanisa,
Mapenzi-ya-Mungu,
Mungu,
Nyaraka-Kumi,
Paulo,
Petro,
Roho-Mtakatifu,
Ufunuo,
VITABU,
Yehova,
Yesu
11/15/2017
Wale wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watakubaliwa na Mungu
Mwenyezi Mungu alisema, Kazi ya Roho Mtakatifu inabadilika kutoka siku hadi siku, ikipanda juu kwa kila hatua; ufunuo wa kesho unakuwa hata juu kuliko wa leo, hatua kwa hatua ukikwea hata juu zaidi. Hii ndiyo kazi anayotumia Mungu kumkamilisha mwanadamu. Iwapo mwanadamu hawezi kwenda sambamba, basi anaweza kuachwa wakati wowote. Kama mwanadamu hana moyo wa kutii, basi hawezi kufuata hadi mwisho. Enzi ya kale imepita; sasa ni enzi mpya. Na katika enzi mpya, kazi mpya lazima ifanywe. Hasa katika enzi ya mwisho ambapo mwanadamu atakamilishwa, Mungu atafanya kazi mpya hata haraka zaidi.
11/14/2017
Kuzishika Amri na Kuutenda Ukweli
Umeme wa Mashariki | Kuzishika Amri na Kuutenda Ukweli |
Matamshi ya Mwenyezi Mungu - Kuzishika Amri na Kuutenda Ukweli
Katika matendo, amri zapaswa kuunganishwa na matendo ya ukweli. Wakati unapozishika amri, mtu anapaswa kutenda ukweli. Wakati anapotenda ukweli, mtu hapaswi kukiuka kanuni za amri au kwenda kinyume na amri. Fanya yale ambayo Mungu anahitaji uyafanye. Kuzishika amri na kuutenda ukweli vinahusiana, bali havikinzani. Zaidi unavyotenda ukweli, ndivyo unavyoweza kutilia maanani zaidi kiini cha amri. Zaidi unavyotenda ukweli, ndivyo utakavyoweza kulielewa zaidi neno la Mungu kama ilivyoonyeshwa katika amri. Kutenda ukweli na kuzishika amri sio vitendo vinavyopingana, lakini badala yake vinahusiana. Mwanzoni, ni kwa kuzishika tu amri ndipo mwanadamu anaweza kuutenda ukweli na kufikia kuipata nuru kutoka kwa Roho Mtakatifu. Lakini hii sio nia ya awali ya Mungu.
Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake
Umeme wa Mashariki | Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake |
Kwanza, hebu na tuuimbe wimbo wa kumsifu Mungu: Wimbo wa Ufalme (I) Ufalme Umeshuka katika Ulimwengu
Kisaidizi ala cha muziki: Watu wanashangilia Mungu kwa furaha, watu wanamsifu Yeye, sauti zisizohesabika zinaongea kuhusu Mungu mmoja wa kweli, ufalme umeshuka ulimwenguni.
1. Watu wanashangilia Mungu kwa furaha, watu wanamsifu Yeye, sauti zisizohesabika zinaongea kuhusu Mungu mmoja wa kweli, watu wasiohesabika wanaangalia matendo Yake. Ufalme umeshuka ulimwenguni, na mtu wa Mungu yu tajiri na mwenye ukarimu, tajiri na mwenye ukarimu.
Ni nani asiyeshangilia kwa haya (ni nani asiyeshangilia kwa haya)? Ni nani asiyecheza kwa haya (ni nani asiyecheza kwa haya)? Zayuni (Zayuni), Zayuni (Zayuni), inua bango lako la ushindi ili kusherehekea Mungu!
Kisaidizi ala cha muziki: Watu wanashangilia Mungu kwa furaha, watu wanamsifu Yeye, sauti zisizohesabika zinaongea kuhusu Mungu mmoja wa kweli, ufalme umeshuka ulimwenguni.
1. Watu wanashangilia Mungu kwa furaha, watu wanamsifu Yeye, sauti zisizohesabika zinaongea kuhusu Mungu mmoja wa kweli, watu wasiohesabika wanaangalia matendo Yake. Ufalme umeshuka ulimwenguni, na mtu wa Mungu yu tajiri na mwenye ukarimu, tajiri na mwenye ukarimu.
Ni nani asiyeshangilia kwa haya (ni nani asiyeshangilia kwa haya)? Ni nani asiyecheza kwa haya (ni nani asiyecheza kwa haya)? Zayuni (Zayuni), Zayuni (Zayuni), inua bango lako la ushindi ili kusherehekea Mungu!
11/12/2017
Kumwamini Mungu Lazima Kulenge Uhalisi, Si Tamaduni za Kidini
Umeme wa Mashariki | Kumwamini Mungu Lazima Kulenge Uhalisi, Si Tamaduni za Kidini |
Mwenyezi Mungu alisema , Je, ni desturi ngapi za kidini unazozizingatia? Ni mara ngapi wewe umeasi dhidi ya neno la Mungu na kwenda kwa njia yako mwenyewe? Ni mara ngapi wewe umetia katika vitendo neno la Mungu kwa sababu wewe kwa kweli unajali mizigo Aliyobeba na unatafuta kutimiza mapenzi Yake? Lielewe neno la Mungu na uliweke katika vitendo. Kuwa mwenye maadili katika vitendo na matendo yako; huku si kutii sheria au kufanya hivyo shingo upande kwa ajili ya kujionyesha. Badala yake, haya ni kutenda ukweli na kuishi kulingana na neno la Mungu. Kutenda kama huku pekee ndiko hutosheleza Mungu. Desturi yoyote inayompendeza Mungu si kanuni bali ni kutenda ukweli.
11/11/2017
Upendo Halisi kwa Mungu ni wa Hiari
Umeme wa Mashariki | Upendo Halisi kwa Mungu ni wa Hiari |
Umeme wa Mashariki | Upendo Halisi kwa Mungu ni wa Hiari
Watu wote wamepitia usafishaji kwa sababu ya maneno ya Mungu. Kama sio Mungu mwenye mwili wanadamu bila shaka hawangebarikiwa kuteseka hivyo. Inaweza pia kusemwa hivi—wale wanaoweza kukubali majaribio ya maneno ya Mungu ni watu waliobarikiwa. Kulingana na ubora wa akili wa watu wa asili, mwenendo wao, mitazamo yao kwa Mungu, hawastahili kupokea aina hii ya usafishaji. Ni kwa sababu wameinuliwa na Mungu ndio wamefurahia baraka hii. Watu walikuwa wakisema kwamba hawakustahili kuuona uso wa Mungu au kusikia maneno Yake. Leo ni kwa sababu tu ya kutiwa moyo na Mungu na fadhili Zake ndio watu wamepokea usafishaji wa maneno Yake.
11/10/2017
Umeme wa Mashariki | Tabia Yako Ni Duni Sana!
Umeme wa Mashariki | Tabia Yako Ni Duni Sana! |
Mwenyezi Mungu alisema, Ninyi nyote mmeketi katika viti vya kifahari, mkiwafundisha wale wa vizazi vijana ambao ni wa aina yenu, ukiwafanya waketi nawe. Je, mngekosaje kujua kwamba wale "watoto" wenu walikuwa tayari hawana pumzi, na kwamba hawakuwa na kazi Yangu zamani? Utukufu Wangu huangaza kutoka nchi ya Mashariki hadi nchi ya Magharibi, lakini wakati utukufu Wangu huenea mpaka mwisho wa dunia na wakati unapoanza kuinuka na kuangaza, Nitaondoa utukufu wa Mashariki na kuuletea Magharibi ili kwamba hawa watu wa giza katika Mashariki ambao wameniacha Mimi watakuwa bila mwanga unaong'aa kuanzia hapo kwendelea.
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Fumbo la Kupata Mwili (2)
Fumbo la Kupata Mwili (2)
Mwenyezi Mungu alisema, Katika wakati ambapo Yesu Alifanya kazi Uyahudi, Aliifanya wazi, lakini sasa, Nazungumza na Kufanya kazi kati yenu kwa siri. Wasioamini hawana ufahamu wowote. Kazi Yangu kati yenu imetengwa kutoka kwa nyingine. Maneno haya, kuadibu huku na hukumu hii, vinajulikana tu kwako na sio mwingine. Kazi hii yote inatendeka kati yenu na kuonekana tu kwenu; hakuna yeyote asiyeamini anayefahamu haya, kwani muda haujafika. Wanadamu hao wako karibu kufanywa wakamilifu baada ya kuvumilia adibu, lakini wale walio nje hawajui lolote juu yake. Kazi hii imefichwa sana! Kwao, Mungu mwenye mwili ni siri, lakini kwa wale walio katika mkondo, Anaweza kuchukuliwa kuwa wazi.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)