Mwenyezi Mungu alisema, Kuwa na ujuzi wa utendaji na kuwa na uwezo wa kuona wazi kazi ya Mungu—yote haya yanaonekana katika maneno Yake. Ni kwa maneno ya Mungu tu ndimo unaweza kupata nuru, hivyo unapaswa kujitayarisha na maneno Yake zaidi. Gawa ufahamu wako kutoka kwa maneno ya Mungu katika ushirika, na kupitia katika ushirika wako wengine wanaweza kupata nuru na unaweza kuwaongoza watu kwenye njia—njia hii ni ya utendaji.
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Mateso na Maafa Yalinisaidia Kukua
Baituo Mji wa Dezhou, Mkoa wa Shandong
Kabla, nilijua tu kwamba hekima ya Mungu ilitumiwa kwa msingi wa njama za Shetani, kwamba Mungu ni Mungu mwenye hekima na kwamba Shetani milele atakuwa adui mshinde wa Mungu katika nadharia, lakini sikuwa na ufahamu au maarifa ya jambo hili kutegemeza uzoefu halisi. Baadaye, ni ndani tu ya mazingira yaliyopangwa na Mungu nilipopata uzoefu halisi wa kipengele hiki cha kweli.