7/31/2018

Unahitaji Kusadiki Vipi Mungu Ili Kuweza Kuokolewa na Kufanywa Kuwa Mtimilifu?

Sura ya 4 Ukweli wa Kazi ya Mungu ya Siku za Mwisho

5. Unahitaji Kusadiki Vipi Mungu Ili Kuweza Kuokolewa na Kufanywa Kuwa Mtimilifu?

Maneno Husika ya Mungu:
Kufanya muhtasari wa kuishika njia ya Petro katika kumwamini Mungu, ni kuishika njia ya kufuatilia ukweli, ambayo pia ni njia ya kujijua na kubadilisha tabia ya mtu. Ni kwa kuishika tu njia ya Petro ndio mtu atakuwa anashika njia ya kukamilishwa na Mungu. Mtu lazima aelewe hasa jinsi ya kuishika njia ya Petro na jinsi ya kuiweka katika vitendo. Kwanza, mtu lazima aweke kando madhumuni yake mwenyewe, shughuli zisizofaa, na hata familia yake na vitu vyote vya mwili wake. Lazima ajitolee kwa moyo wote, yaani, ajitolee kabisa kwa neno la Mungu, azingatie kula na kunywa neno la Mungu, azingatie kutafuta ukweli, utafutaji wa nia ya Mungu katika maneno Yake, na ajaribu kufahamu mapenzi ya Mungu katika kila kitu.

Hatimaye Naweza Kumpenda Mungu



Mungu, upendo Wako ni wa kweli na safi. Moyo Wako ni mwaminifu na mkarimu.
Ulitupa sisi kila kitu Chako ili kulipa gharama kwa ajili ya kutuokoa sisi.
Nakupenda na kukutegemea Wewe. Natetemeka katika uwepo Wako.
Nilipitia majaribu na Wewe. Sitaki uondoke upande wangu.

7/30/2018

"Wakati wa Mabadiliko" (1) - Wanawali Wenye Hekima Hunyakualiwaje?🎬👍


Kanisa la Mwenyezi Mungu | "Wakati wa Mabadiliko" (1) - Wanawali Wenye Hekima Hunyakualiwaje?

Watu wengine huongozwa na maneno ya Paulo katika suala la kumngoja Bwana ili kuinuliwa kwenda katika ufalme wa mbinguni: "Kwa ghafla, kufumba na kufumbua, wakati wa tarumbeta ya mwisho: kwa maana tarumbeta italia, na wafu watafufuliwa bila uovu, na tutabadilishwa" (1Kor 15:52). Wanaamini kwamba ingawa bado tunatenda dhambi siku zote bila kujinasua kutoka kwa pingu za asili ya dhambi, Bwana atazibadili taswira zetu mara moja na kutuleta katika ufalme wa mbinguni Atakapokuja.

Kuelewa Mapenzi ya Mungu Katikati ya Matatizo

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Wakristo
Xiao Rui    Mji wa Panzhihua, Mkoa wa Sichuan
Nilipokuwa nikihubiri injili nilikutana na viongozi wa madhehebu ambao walisema uongo ili kupinga na kuvuruga, na kuwaita polisi. Hili lilisababisha wale niliokuwa nikihubiria kutothubutu kuwasiliana nasi, na wale ambao walikuwa tu wameikubali injili kutoweza kuwa na imani katika kazi ya Mungu. Nilipofanya kazi kwa bidii sana lakini matokeo yalikuwa duni, nilifikiri: kazi ya Kiinjili ni ngumu sana kutekeleza.

Latest Swahili Gospel Movie "Kusubiri" | Bwana Yesu Kristo Ameonekana Kufanya Kazi Yake

Latest Swahili Gospel Movie "Kusubiri" | Bwana Yesu Kristo Ameonekana Kufanya Kazi Yake

Yang Hou'en ni mchungaji katika kanisa la nyumbani Uchina. Pamoja na babake Yang Shoudao, wamemngoja Bwana Yesu ashuke kutoka mawinguni na kuwachukua juu hadi katika ufalme wa mbinguni. Kwa ajili ya hili, walimfanyia Bwana kazi kwa bidii, walishikilia imara jina Lake, na kuamini kuwa yeyote ambaye sio Bwana Yesu ashukaye mawinguni ni Kristo wa uongo.

7/29/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ufafanuzi wa Tamko la Thelathini

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ufafanuzi wa Tamko la Thelathini


Mwenyezi Mungualisema, Watu wengine wanaweza kuwa na utambuzi kidogo katika maneno ya Mungu, lakini hakuna yeyote kati yao ambaye huamini hisia zake; wao huogopa sana kuingia katika ukanaji. Hivyo, wao kila mara wamegeuka kati ya furaha na huzuni. Ni haki kusema kwamba maisha ya watu wote yamejaa huzuni;

Neno la Mungu "Ngurumo Saba Zatoa Sauti - Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni"


Neno la Mungu "Ngurumo Saba Zatoa Sauti - Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni"

Mwenyezi Mungu alisema, "Wakati nuru ya Mashariki inapong’aa polepole tu ndipo giza kote duniani litaanza kugeuka na kuwa nuru, na hapo tu ndipo mwanadamu atatambua kwamba Nilishatoka Israeli zamani na Nimeanza kuchomoza upya Mashariki. Niliwahi kushuka Israeli na baadaye Niliondoka kutoka huko, Siwezi tena kuzaliwa Israeli kwa mara nyingine, kwa kuwa kazi Yangu inauongoza ulimwengu mzima na, zaidi ya hilo, umeme unamulika moja kwa moja kutoka Mashariki kwenda Magharibi.

7/28/2018

Mungu Kupata Mwili Ni Nini? Kiini cha Mungu Kupata Mwili Ni Nini?

Sura ya 5 Ukweli Kuhusu Mungu Kupata Mwili

1. Mungu Kupata Mwili Ni Nini? Kiini cha Mungu Kupata Mwili Ni Nini?

Maneno Husika ya Mungu:
Maana ya kupata mwili ni kwamba Mungu Anajionyesha katika mwili, na Anakuja kufanya kazi miongoni mwa wanadamu wa uumbaji Wake katika umbo la mwili. Hivyo, ili Mungu kuwa mwili, ni lazima kwanza Apate umbo la mwili, mwili wenye ubinadamu wa kawaida; hili ndilo hitaji la kimsingi zaidi. Kwa kweli, maana ya kupata mwili kwa Mungu ni kwamba Mungu Anaishi na kufanya kazi katika mwili, Mungu katika kiini Chake Anakuwa mwili, Anakuwa mwanadamu. Maisha Yake ya kimwili na kazi vinaweza kugawanywa katika hatua mbili. Kwanza ni maisha Anayoishi kabla ya kuanza kutekeleza huduma Yake.

Umuhimu wa Kazi ya Mungu ya Majaribio na Utakasaji

Sura ya 4 Ukweli wa Kazi ya Mungu ya Siku za Mwisho

4. Umuhimu wa Kazi ya Mungu ya Majaribio na Utakasaji

Maneno Husika ya Mungu:
Majaribu haya yanailenga hali gani ya ndani ya watu? Yanalenga tabia ya uasi ndani ya watu ambayo haiwezi kumridhisha Mungu. Kuna mengi ambayo ni machafu ndani ya watu, na mengi ambayo ni ya unafiki, na kwa hivyo Mungu anawatia katika majaribu ili kuwasafisha. ...
Ikiwa hujui tabia ya Mungu, bila shaka utaanguka wakati wa majaribu, kwa kuwa hufahamu jinsi Mungu anavyowafanya watu kuwa wakamilifu, na ni kwa njia gani Huwafanya wakamilifu, na majaribu ya Mungu yakikushukia na yasilingane na mawazo yako, utashindwa kusimama imara.

7/27/2018

"Ivunje Laana" (3) - Je, Neno la Mungu Lipo Isipokuwa Biblia?


Baadhi ya watu wa kidini huamini kuwa maneno na kazi zote za Mungu ziko katika Biblia, na kwamba hakuna maneno na kazi ya Mungu isipokuwa yale yaliyo katika Biblia. Je, aina hii ya mtazamo inaafikiana na ukweli? Biblia inasema, "Na kuna mambo mengi pia aliyoyafanya Yesu, ambayo, kama yakiandikwa kila moja, nadhani hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa" (Yohana 21:25). Mwenyezi Mungu alisema, "Kile Mungu alicho na anacho milele hakiishi wala hakina mipaka. Mungu ni chanzo cha uhai na vitu vyote. Mungu hawezi kueleweka na kiumbe yeyote aliyeumbwa.

Best Swahili Gospel Worship Song "Njoo Mbele Ya Mungu Mara kwa Mara" | Uso kwa uso na Mungu



💞@@@@🎼@@@@😇@@@@🎶@@@@🎤
🎻~~~~🎵~~~~💞~~~~💞~~~~💓~~~~💕
Chukua fursa unapokuwa na wakati, keti kimya mbele ya Mungu.
Soma neno Lake, jua ukweli Wake, rekebisha makosa yaliyo ndani yako.
Majaribu huja, yakabili; ijue nia ya Mungu na utakuwa na nguvu.
Mwambie ni vitu gani unavyokosa, shiriki ukweli Wake kila mara.
Roho yako ina furaha unapomwabudu Yeye.
Njoo mara kwa mara mbele ya Mungu, usipinge tena.

7/26/2018

Umuhimu wa Kazi ya Mungu ya Hukumu na Kuadibu

Sura ya 4 Ukweli wa Kazi ya Mungu ya Siku za Mwisho

3. Umuhimu wa Kazi ya Mungu ya Hukumu na Kuadibu

Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ya siku za mwisho ni kutenganisha vitu vyote kulingana na jinsi yavyo, kuhitimisha mpango wa usimamizi wa Mungu, kwa maana muda u karibu na siku ya Mungu imewadia. Mungu huwaleta wote ambao wameingia katika ufalme Wake, yaani, wale wote ambao wamekuwa waaminifu Kwake mpaka mwisho, katika enzi ya Mungu Mwenyewe. Hata hivyo, kabla ya kuja kwa enzi ya Mungu Mwenyewe, kazi Atakayofanya Mungu si kutazama matendo ya mwanadamu wala kuchunguza maisha ya wanadamu, ila ni kuhukumu uasi wake, kwa maana Mungu atawatakasa wale wote wanaokuja mbele ya kiti Chake cha enzi.

Nitalipa Upendo Wa Mungu

Nahisi furaha sana kumfuata Mungu wa matendo.
Sikufikiria kamwe kuuona uso wa Mungu.
Ni neema kubwa sana kupokea hukumu ya Mungu.
Lazima tuujali moyo Wake.
Katika uzoefu wa kazi ya Mungu, nimefurahia upendo Wake.
Kumwona Mungu akiteseka sana kwa ajili yetu,
nagundua kuwa mwanadamu amepotoshwa sana na Shetani.

7/25/2018

Trela ya Filamu "Yule Anayeshikilia Ukuu Juu ya Kila Kitu" | Kuchunguza Mafumbo ya Maisha🎬👏🎉


👀👀👀~~~~~~~~~~~👍👍👍👍&&&&&&&&&&🎉🎉🎉🎉🎉
 💞💞💞💞@@@@@@@@@@💓💓💓💓

Mtu Atarudi Kule Alikotoka.
Hakuna yeyote anayeweza kushinda ugonjwa na kifo. 
Hakuna yeyote anayeweza kubadilisha sheria za uzee na udhaifu wa mwili au akili.
………………………………

"Kwa nini tunaishi? Na kwa nini inatulazimu kufa? Nani anayeitawala dunia hii?"

Wimbo | Njia Yote Pamoja na Wewe

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Msifuni Mwenyezi Mungu


I
Nilikuwa kama mashua, ikielea baharini. Ulinichagua, na mahali pazuri Uliniongoza. Sasa katika familia Yako, nikipewa joto na upendo Wako, nina amani kabisa. Unanibariki, Unatoa maneno Yako ya hukumu. Bado sijui jinsi ninavyokosa kuithamini neema Yako. Kila mara nikiasi, kwa namna fulani nikiuumiza moyo Wako. Na bado Hunitendei kulingana na dhambi zangu lakini Unafanya kazi kwa ajili ya wokovu wangu. Ninapokuwa mbali, Unaniita nirudi kutoka hatarini.

7/24/2018

Umeme wa Mashariki | Ufafanuzi wa Tamko la Thelathini na Tatu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Umeme wa Mashariki | Ufafanuzi wa Tamko la Thelathini na Tatu 

Mwenyezi Mungu alisema, Kwa ukweli, kutegemea kile ambacho Mungu amefanya ndani ya watu, na kuwapa, na vilevile kile ambacho watu wanacho, inaweza kusemwa kwamba matakwa Yake kwa watu sio makubwa mno, kwamba hataki mengi kutoka kwao. Wangekosaje basi, kujaribu kumridhisha Mungu? Mungu humpa mwanadamu asilimia mia moja, lakini Huhitaji tu sehemu ndogo ya asilimia kutoka kwa watu—hii ni kuhitaji mengi sana?

Ni kwa Kupitia Usafishaji tu Ndiyo Mwanadamu Anaweza Kumpenda Mungu kwa Kweli

Mwenyezi Mungu alisema, Je, ni jinsi gani mwanadamu anafaa kumpenda Mungu wakati wa usafishaji? Baada ya kupitia usafishaji, wakati wa usafishaji watu wanaweza kumsifu Mungu kwa kweli na kuona jinsi wanavyokosa kwa kiasi kikubwa. Kadiri usafishaji wako ulivyo mkubwa, ndivyo unaweza zaidi kukana mwili; kadiri usafishaji wao ulivyo mkubwa, ndivyo zaidi ulivyo upendo wa watu kwa Mungu, Hili ndilo mnapaswa kuelewa.

7/23/2018

Ee Mungu, Siwezi kuwa bila Wewe

Ni Wewe unayenileta mbele Yako.
Ni maneno Yako matamu, ni upendo Wako wa upole,
Upendo Wako unaofurahisha sana, ndio unashikilia moyo wangu sana,
ambao unafanya moyo wangu kukupenda Wewe kutoka siku hii na kuendelea.
Ee … Moyo wangu unakufikiria kukuhusu Wewe kila wakati.

Umeme wa Mashariki | Ufafanuzi wa Tamko la Arubaini na Mbili

Umeme wa Mashariki | Ufafanuzi wa Tamko la Arubaini na Mbili 

Mwenyezi Mungu alisema, Sijui kama watu wameona mabadiliko yoyote katika tamko la leo. Huenda watu wengine wameona kidogo, lakini hawathubutu kusema kwa kweli. Labda wengine hawajatambua chochote. Mbona kuna tofauti kubwa sana hivyo kati ya siku ya kumi na mbili na ya kumi na tano ya mwezi? Umetafakari hili? Maoni yako ni gani? Umeelewa chochote kutokana na matamko yote ya Mungu? Ni kazi gani kuu iliyofanywa kati ya tarehe mbili Aprili na tarehe kumi na tano Mei?

7/22/2018

Ni Nani Anayejua Moyo wa Kutunza wa Mungu?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, upendo wa Mungu
Qingxin    Mji wa Zhengzhou, Mkoa wa Henan
Kuhusu kipengele cha ukweli cha "Mungu ni mwenye haki ", siku zote nilikuwa na ufahamu wa upuuzi kwa kiasi fulani. Nilidhani kuwa almradi mtu fulani hufichua upotovu katika kazi yake au hufanya makosa ambayo huiharibu kazi ya kanisa, mtu huyo atakabiliwa na rada, au kupoteza kazi yake au aathiriwe na adhabu. Hiyo ni haki ya Mungu.

Kupima kwa Sura Ni Upuuzi Tu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Ushuhuda
Yifan    Jiji la Shangqiu, Mkoa wa Henan
Katika siku za nyuma, mimi mara nyingi niliwapima watu kwa sura zao, nikiwachukua watu wachangamfu, wajuzi na wambuji hasa kwa heshima sana. Niliamini kwamba watu kama hao walikuwa wa busara, hodari kwa kuwaelewa wengine na kwa ujumla wema na wakarimu. Ni juzi juzi tu, kama ambavyo uhalisi umejifichua, nimekuja kurekebisha njia hii ya upuuzi ya kufikiri.

7/21/2018

Kwa Nini Yasemekana Kwamba Kuzijua Awamu Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kujua Mungu?

Sura ya 3 Ukweli Kuhusu Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

5. Kwa Nini Yasemekana Kwamba Kuzijua Awamu Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kujua Mungu?

(Fungu Lililochaguliwa la Neno la Mungu)
Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu
Kazi ya kumsimamia mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu, na ina maana kuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu. Hatua hizi tatu hazihusishi kazi ya kuuumba ulimwengu, ila ni hatua tatu za kazi ya Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Kazi ya kuiumba dunia ilikuwa kazi ya kusababisha uwepo wa wanadamu wote. Haikuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu, na haina uhusiano na kazi ya kumwokoa mwanadamu, kwa kuwa dunia ilipoumbwa mwanadamu hakuwa amepotoshwa na Shetani, na hivyo hakukuwa na haja ya kutekeleza kazi ya kumwokoa mwanadamu.

Latest Swahili Christian Movie "Imani katika Mungu" | Hufunua Fumbo la Imani Katika Mungu



Yu Congguang huhubiri injili kwa niaba ya Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wakati wa kuhubiri injili, aliandamwa na serikali ya Kikomunisti ya China. Alikimbia milimani, ambapo alipokea msaada kutoka kwa Zheng Xun, mfanyakazi mwenza wa kanisa la nyumba la mahali pale. Walipokutana mara ya kwanza, walihisi kama tayari walikuwa wamejuana kwa muda mrefu. Zheng Xun alimpeleka Yu Congguang kwenye kibanda cha makuti ambapo yeye na wafanyakazi wenzake walikusanyika.

Jitiishe Mwenyewe ili Kufundisha Wengine Nidhamu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Ushuhuda
Xiaoyan    Jiji la Xinyang, Mkoa wa Henan
Nilikuwa na ubia wa kazi wa karibu na dada mmoja mzee katika masuala ya jumla. Baada ya kufanya kazi naye kwa muda fulani, nikamwona kuwa mzembe katika kazi yake na kwamba hakukubali ukweli. Kikwelikweli, nilikata kauli kumhusu. Hatua kwa hatua, uhusiano wa kawaida kati yetu ulipotea, hatukuweza kupatana vizuri, na hatukuweza kuwa mbia katika kazi.

7/20/2018

Nilijifunza Kufanya Kazi na Wengine

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Wakristo
Liu Heng    Mkoa wa Jiangxi
Kupitia neema na kuinuliwa kwa Mungu, nilichukua jukumu la kuwa kiongozi wa kanisa. Wakati huo, nilikuwa na shauku mno na niliweka azimio mbele ya Mungu: Bila kujali kinachonikabili, sitayatelekeza majukumu yangu. Nitafanya kazi vizuri na yule dada mwingine na nitakuwa mtu anayetafuta ukweli. Lakini nilikuwa nimeamua tu, na sikujua jinsi ya kuingia katika uhalisi wa uhusiano wa kufanya kazi kwa mpangilio wa kuridhisha.

Hakuna Anayeweza Kufanya Kazi Badala Yake

Kazi ya Mungu hufanywa na Mungu Mwenyewe.
Ni Yeye ndiye Anayeianzisha kazi Yake, na ni Yeye anayeikamilisha.
Ni Yeye anayeipanga kazi.
Ni yeye ndiye anayeisimamia, na zaidi kuifanikisha kazi hiyo.
Ni kama ilivyosemwa katika Biblia,
Mungu ndiye Mwanzo na Mwisho;
Mungu ndiye Mpanzi na tena Mvunaji.”

7/19/2018

Umuhimu wa Kazi ya Mungu ya Maneno

Sura ya 4 Ukweli wa Kazi ya Mungu ya Siku za Mwisho

1. Umuhimu wa Kazi ya Mungu ya Maneno

Maneno Husika ya Mungu:
Katika Enzi ya Ufalme, Mungu anatumia neno ili kukaribisha enzi mpya, ili kubadilisha mbinu za kazi Yake, na kuweza kufanya kazi katika enzi nzima. Hii ndiyo kanuni ambayo kwayo Mungu hufanya kazi katika Enzi ya Neno. Alikuwa mwili ili kuweza kuzungumza kutoka mitazamo tofauti, kumwezesha binadamu kumwona Mungu kwa kweli, ambaye ni Neno linaloonekana katika mwili, na hekima Yake na maajabu. Kazi kama hiyo inafanywa ili kwa njia bora zaidi kutimiza shabaha za kumshinda binadamu, kumkamilisha binadamu, na kumwondoa binadamu.

Filosofia ya Shetani Inanasa na Kuharibu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, kanisa
Wu You    Mji wa Hechi, Mkoa wa Guangxi
Wakati fulani uliopita, kanisa lilinipangia kuishi na familia mwenyeji kwa sababu za kazi. Wakati nilipofanya ushirika kwanza na ndugu wa kiume na wa kike wa familia hii mwenyeji, walisema, "Tunaogopa sana kuomba katika ushirika. Tunajua cha kusema tunaposali peke yetu, lakini linapokuja suala la kuomba wakati wa ushirika, hatujui hasa cha kusema."

7/18/2018

Sifu Mungu | Wewe Tu Unaweza Kuniokoa Mimi🎼🎙️😇😇

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Nyimbo


Sifu Mungu | Wewe Tu Unaweza Kuniokoa Mimi

 I 
Mnyenyekevu na Uliyejificha, Waambatana na watu katika matatizo yao, Ukiwapa njia ya uzima wa milele. Unawapenda binadamu kama mwili Wako mwenyewe. Na Wastahili upendo wao. Afadhali Uteseke Mwenyewe, ili Umwezeshe mwanadamu apate faida. Na Wanyesha uzima juu yao. Moyo Wako unapendeza kweli, Wewe ni mwenye haki sana na Wastahili sifa ya mwanadamu. Maneno Yako yanitwaa. Hukumu Yako yanitakasa. Wewe pekee Waweza niokoa.

Umuhimu wa Kazi ya Mungu ya Kushinda

Sura ya 4 Ukweli wa Kazi ya Mungu ya Siku za Mwisho

2. Umuhimu wa Kazi ya Mungu ya Kushinda

Maneno Husika ya Mungu:
Wanadamu kwa ajili ya kupotoshwa sana na Shetani, hawajui kuwa kuna Mungu na wameacha kumwabudu Mungu. Adamu na Hawa walipoumbwa mwanzoni, utukufu wa Yehova na Ushuhuda wa Yehova daima vilikuwepo. Lakini baada ya kupotoshwa, mwanadamu alipoteza utukufu na ushuhuda kwa sababu kila mtu alimwasi Mungu na kuacha kumtukuza kabisa. Kazi ya sasa ya kushinda ni kuupata ushuhuda na utukufu wote, na kuwafanya wanadamu wote wamwabudu Mungu, ili kuwepo na ushuhuda miongoni mwa viumbe wote. Hili ndilo linapaswa kufanywa katika hatua hii ya kazi.

7/17/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko la Arubaini na Mbili

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko la Arubaini na Mbili

Punde tu kazi mpya inapoanza, watu wote wanakuwa na kuingia kupya, na wanasonga mbele nami bega kwa bega, tunatembea pamoja kwenye barabara kubwa ya ufalme, na kuna urafiki mkubwa kati ya mwanadamu na Mimi. Ili kuonyesha hisia Zangu, ili kudhihirisha mtazamo Wangu kwa mwanadamu, Nimemzungumzia mwanadamu kila mara.

Trela ya Filamu "Yule Anayeshikilia Ukuu Juu ya Kila Kitu" | Kuuchunguza Ulimwengu🎬🎉🎼


Katika anga kubwa mno ya ulimwengu iliyojaa nyota, sayari zinagongana, na mfululizo wa michakato migumu huzaa sayari mpya.… Sayari zisizo na idadi za mbingu ulimwenguni zote hufanya kazi kwa ulinganifu—ni nani huzielekeza? Filamu ya Kikristo ya muziki—Yule Anayeshikilia Ukuu Juu ya Kila Kitu—hivi karibuni itafichua ukweli wa kweli!

7/16/2018

Uhusiano Kati ya Kila Mojawapo ya Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

Sura ya 3 Ukweli Kuhusu Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

4. Uhusiano Kati ya Kila Mojawapo ya Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

Maneno Husika ya Mungu:
Kutoka kwa kazi ya Yehova mpaka ile ya Yesu, na kutoka kwa kazi ya Yesu hadi kwa kazi iliyoko kwa awamu hii ya sasa, awamu hizi tatu zinajumlisha upana wote wa usimamizi wa Mungu, na zote ni kazi za Roho mmoja. Kutoka Alipoumba ulimwengu, Mungu Amekuwa Akisimamia wanadamu. Yeye ndiye Mwanzo na ndiye Mwisho; Yeye ndiye wa Kwanza na wa Mwisho, na Yeye ndiye mwanzilishi wa enzi na Yeye ndiye huleta enzi kwenye kikomo. Awamu tatu za kazi, katika enzi tofauti na maeneo mbalimbali, hakika yanafanywa na Roho mmoja. Wote ambao wanatenganisha awamu hizi tatu wanampinga Mungu.

Wimbo wa Maneno ya Mungu | Watu Wote Wanaishi Katika Mwanga wa Mungu🎼🎉👏

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Nyimbo za kanisa

I
Sasa kwa kushangilia sana,
utakatifu wa Mungu na haki
vinakua ulimwenguni kote,
ikitukuka sana kati ya wanadamu wote.
Miji ya mbinguni inacheka,
falme za dunia zinacheza.
Ni nani asiyesherehekea?
Ni nani asiyetoa machozi?
Wanadamu hawagombani wala kupigana makonde;

7/15/2018

Trela ya Filamu ya Kikristo "Yule Anayeshikilia Ukuu Juu ya Kila Kitu" | Kutoa Sheria🎬👏



🎉🎉🎉🎉🎉🎉**********🎊🎊🎊🎊→→*******👏👏👏


Amri na sheria ambazo Yehova Mungu aliwapa Waisraeli hazijakuwa na athari kubwa sana kwa sheria ya binadamu tu, lakini pia zimetekeleza jukumu muhimu katika kuanzishwa na utengenezwaji wa ustaarabu wa kimaadili na taasisi za kidemokrasia katika jamii za binadamu. Filamu ya Kikristo ya muziki—Yule Anayeshikilia Ukuu Juu ya Kila Kitu—hivi karibuni itaonyesha ukweli wa kihistoria!

Sikiliza zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu, Chanzo cha Mafanikio ya Umeme wa Mashariki 

Mungu Mmoja Wa Kweli Ameonekana katika Mwili

Radi inanguruma, ikitingiza mbingu. Mungu mmoja wa kweli ameonekana!
Ni sauti ya Roho Mtakatifu mwenyewe na ushuhuda Wake,
kama sauti ya radi kutoka mbingu. Amina! Amina!
Tunathibitisha Mungu ameonekana katika mwili.
Mwokozi amerejea, juu ya wingu jeupe.

7/14/2018

Tendeni Ukweli Mara Mnapouelewa

Kazi na neno la Mungu vina maana ya kuleta mabadiliko katika tabia zenu; lengo Lake si kuwafanya tu kulielewa au kulitambua na kufanya hilo kuwa mwisho wa jambo hilo. Kama mmoja wa uwezo wa kupokea, hampaswi kuwa na ugumu katika kuelewa neno la Mungu, kwa kuwa wingi wa neno la Mungu limeandikwa kwa lugha ya kibinadamu ambayo ni rahisi sana tu kuelewa. Kwa mfano, mnaweza kujua ni nini Mungu anataka muelewe na kutenda;

Nyimbo za Mungu | Nitakubali Uishi Moyoni Mwangu Wakati Wote🎼🎹

Unaandamana nami katika misimu minne.
Nikitazama uso Wako wenye upweke, mawimbi ya huzuni yanajaa moyoni mwangu.
Sijawahi kubembeleza huzuni Wako na sikujali kamwe kuhusu upweke Wako;
nikikumbana na maneno Yako ya bidii tena na tena, mimi ni mkaidi sana.

7/13/2018

Kazi ya Mungu ni Ya Hekima Sana!

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Wakristo
Shiji    Jiji la Ma’anshan , Mkoa wa Anhui
Wakati wa kufanya kazi kwangu kama kiongozi katika kanisa, kiongozi wangu mara nyingi angeshirikiana mifano ya kushindwa kwa wengine ili kutumikia kama somo kwetu. Kwa mfano: Viongozi wengine walizungumza tu kuhusu elimu na mafundisho lakini walikosa kutaja upotovu wao au kuwasiliana kwa karibu kuhusiana na ufahamu wao wa jinsi ukweli unavyotumika kwa ukweli.

Ambua Barakoa, na Uanze Maisha Upya

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Ushuhuda

Chen Dan    Mkoa wa Hunan
Mwishoni mwa mwaka jana, kwa sababu sikuweza kuzindua kazi ya injili katika eneo langu, familia ya Mungu ilimhamisha ndugu mmoja wa kiume kutoka eneo jingine ili kuchukua kazi yangu. Kabla ya haya sikuwa nimearifiwa, bali nilisikia kwa njia isiyo ya moja kwa moja kutoka kwa dada mmoja niliyekuwa mbia naye. Nilifadhaika sana. Nilishuku kwamba mtu aliyekuwa madarakani hakuwa ameniarifu kwa kuhofia kwamba singekubali kuiacha nafasi yangu na ningeshindana.

7/12/2018

Kusudio na Umuhimu wa Kila Mojawapo ya Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

Sura ya 3 Ukweli Kuhusu Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

3. Kusudio na Umuhimu wa Kila Mojawapo ya Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ambayo Yehova alifanya kwa Waisraeli ilianzisha mahali pa Mungu pa asili miongoni mwa binadamu, ambapo pia palikuwa pahali patakatifu ambapo Alikuwapo. Aliwekea kazi Yake mipaka kwa watu wa Israeli. Mwanzoni, Hakufanya kazi nje ya Israeli; badala yake, Aliwachagua watu Aliowaona kuwa wa kufaa ili kuzuia eneo la kazi Yake. Israeli ni mahali ambapo Mungu aliwaumba Adamu na Hawa, na kutoka katika mavumbi ya mahali hapo Yehova alimuumba mwanadamu; mahali hapa pakawa kituo cha kazi Yake duniani. Waisraeli, ambao walikuwa wa ukoo wa Nuhu na pia wa ukoo wa Adamu, walikuwa msingi wa kibinadamu wa kazi ya Yehova duniani.

Njoo Mbele Ya Mungu Mara kwa Mara

Chukua fursa unapokuwa na wakati, keti kimya mbele ya Mungu.
Soma neno Lake, jua ukweli Wake, rekebisha makosa na dhambi ndani yako.
Majaribu huja, yakabili; ijue nia ya Mungu na utakuwa na nguvu.
Mwambie ni vitu gani unavyokosa, shiriki ukweli Wake kila mara.
Roho yako ina furaha unapomwabudu Yeye.
Njoo mara kwa mara mbele ya Mungu, usipinge tena.
Kujali kwako mwili, kunamuumiza Yeye sana.

7/11/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko la Thelathini na Nane


Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko la Thelathini na Nane 


Kotekote katika uzoefu wa wanadamu umbo Langu halijakuwepo, wala kuwepo kwa uongozi wa maneno Yangu, na kwa hiyo Nimemuepuka mwanadamu kwa umbali kila mara na kisha Nikaondoka kwake. Nadharau uasi wa wanadamu. Sijui kwa nini. Inaonekana Nimemchukia mwanadamu tangu mwanzo, na bado Nahisi huruma kubwa kwake. Na kwa hiyo mwanadamu ananiangalia na mioyo miwili, kwani Nampenda mwanadamu, na pia Namchukia mwanadamu.

2018 Best African Worship Song "Miaka Elfu Mbili ya Kungoja" | Karibu Kurudi kwa Bwana Yesu



Kwamba Mungu amekuwa mwili 
hutikisa ulimwengu wa kidini,
inavuruga utaratibu wa kidini,
na inakoroga roho za wale 
wanaongoja kuonekana kwa Mungu.
Nani asiyeshangazwa na haya?
Ni nani asiye na hamu ya kumwona Mungu?
Mungu ameishi kwa miaka mingi kati ya binadamu, 
lakini binadamu hafahamu.

7/10/2018

Ninaona Ukweli wa Upotovu wa Watu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kanisa
Li Heng    Jiji la Suqian, Mkoa wa Jiangsu
Miongoni mwa maneno ambayo kwayo Mungu humfichua mwanadamu nilipata kifungu hiki, “Ilisemwa hapo awali kwamba watu hawa ni uzao wa joka kubwa jekundu. Kwa kweli, ili kuwa wazi, wao ni mfano halisi wa joka kubwa jekundu” (“Ufafanuzi wa Tamko la Thelathini na Sita” katika Neno Laonekana katika Mwili). Nilidhani hili halikunihusu. Ilionekana kwangu kwamba Mungu alifichua maneno haya kwa wale wanaomiliki mamlaka, kwa sababu wao ni joka kubwa jekundu lililobadilishwa;

Nia ya Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

Sura ya 3 Ukweli Kuhusu Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

2. Nia ya Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

Maneno Husika ya Mungu:
Mpango Wangu mzima wa usimamizi, mpango ambao una urefu wa miaka elfu sita, unashirikisha hatua tatu, au enzi tatu: Enzi ya Sheria mwanzoni; Enzi ya Neema (ambayo pia ni Enzi ya Ukombozi); na katika siku za mwisho, Enzi ya Ufalme. Kazi Yangu katika enzi hizi tatu hutofautiana katika maudhui kulingana na asili ya kila enzi, lakini katika kila hatua huambatana na mahitaji ya mwanadamu—au, kwa usahihi zaidi, inafanywa kulingana na ujanja ambao Shetani hutumia katika vita Vyangu dhidi yake. Madhumuni ya Kazi Yangu ni kumshinda Shetani, ili kudhihirisha hekima Yangu na kudura, kufichua ujanja wote wa Shetani na hivyo kuokoa wanadamu wote, wanaoishi chini ya miliki yake.

7/09/2018

Kazi ya Kusimamia Mwanadamu ni Gani?

Sura ya 3 Ukweli Kuhusu Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

1. Kazi ya Kusimamia Mwanadamu ni Gani?

Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ya kumsimamia mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu, na ina maana kuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu. Hatua hizi tatu hazihusishi kazi ya kuuumba ulimwengu, ila ni hatua tatu za kazi ya Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Kazi ya kuiumba dunia ilikuwa kazi ya kusababisha uwepo wa wanadamu wote. Haikuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu, na haina uhusiano na kazi ya kumwokoa mwanadamu, kwa kuwa dunia ilipoumbwa mwanadamu hakuwa amepotoshwa na Shetani, na hivyo hakukuwa na haja ya kutekeleza kazi ya kumwokoa mwanadamu.

Zawadi ya Kupendeza Zaidi Ambayo Mungu Amenipa

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kanisa
Yixin    Jiji la Shijiazhuang, Mkoa wa Hebei
Kabla, ningewasikia mara kwa mara ndugu zangu wa kiume na wa kike wakisema, "Kila kitu ambacho Mungu hufanya ni kwa ajili ya matokeo mazuri; ndiyo yote wanayohitaji watu." Nilikubali hili na kukubaliana nalo, lakini sikuwa na ufahamu wowote kupitia uzoefu wangu mwenyewe. Baadaye nilipata ufahamu kiasi kwa njia ya mazingira ambayo Mungu aliniumbia.

7/08/2018

"Mji Utaangushwa" (5) - Mji mkuu wa dini wa Babeli Umekusudiwa Kuangamia Chini ya Ghadhabu ya Mungu!


Ulimwengu wa dini humkaidi na kumlaani Mwenyezi Mungu, ukitenda matendo maovu yasiyohesabika, na wamekuwa kambi ya Shetani ambayo humpinga Mungu vikali. Mji mkuu wa dini wa Babeli umekusudiwa kuangamia chini ya ghadhabu ya Mungu! Ufunuo unatabiri, "Ole, ole ule mji mkuu Babeli, ule mji ulio na uwezo! kwani hukumu yako imekuja katika saa moja" (Ufunuo 18:10). Mwenyezi Mungu asema, "Tunaamini hakuna nchi ama nguvu inayoweza kuzuia yale anayotaka kutimiza Mungu.

Kwa Nini Mungu Anaitwa kwa Majina Tofauti katika Enzi Tofauti?

Sura ya 2 Ukweli wa Majina ya Mungu

2. Kwa Nini Mungu Anaitwa kwa Majina Tofauti katika Enzi Tofauti?

Maneno Husika ya Mungu:
Katika kila enzi, Mungu Anafanya kazi mpya na huitwa kwa jina jipya; Je, anawezaje kufanya kazi sawa katika enzi tofauti? Itakuwaje Yeye kugandamana na yale ya zamani? Jina la Yesu lilichukuliwa kuwa la kazi ya ukombozi, hivyo bado Yeye Anaweza kuitwa kwa jina moja wakati Atarudi katika siku za mwisho? Je, bado Yeye Atafanya kazi ya ukombozi? Ni kwa nini Yehova na Yesu ni kitu kimoja, ilhali wanaitwa kwa majina tofauti katika enzi hizi tofauti? Je, si kwa sababu enzi za kazi Yao ni tofauti? Jina moja linawezaje kumwakilisha Mungu kwa ukamilifu wake?

7/07/2018

Kuukaribisha Uso Wako Unaotabasamu Unapoonekana Mbele Yangu

Uliniinua kutoka kwa vumbi hadi ndani ya kumbatio Lako.
Uliamsha moyo wangu kutoka kwa usingizi wa usiku mrefu wa giza.
Nikitazama ndani ya ukungu wangu, naona uso Wako unaotabasamu.
Inauita moyo wangu na upendo wangu.
Sikufikiria kamwe ningeuona uso Wako.
Baraka iliyoje imenipata bila kutarajia.

Nilipitia Wokovu wa Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, wakristo
Cheng Hao    Mji wa Yongzhou, Mkoa wa Hunan
Kwa neema ya Mungu, mimi na mke wangu tulipandishwa vyeo hadi kwa timu ya injili ya pili ili kutimiza wajibu wetu. Muda mfupi uliopita, mke wangu alipandishwa cheo kuwa mkurugenzi wa timu, huku mimi, kutokana na kiburi changu mwenyewe na utukutu wangu, nilipoteza kazi ya Roho Mtakatifu na kupelekwa nyumbani kutafakari juu ya matendo yangu.

7/06/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Siri Zilizofichwa Nyuma ya Ukimbizaji

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Ushuhuda

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Siri Zilizofichwa Nyuma ya Ukimbizaji

📖📖~~~*******~~~🌻🌻🌻~~~******~~~😘😘
Li Li     Mji wa Dezhou, Mkoa wa Shandong
Sio muda mrefu uliopita, nilitiwa moyo na Mungu na kupandiswa cheo kuwa mfanyakazi wa eneo. Siku moja, nilipokuwa nimekusanyika na wafanyakazi wenzangu, sikuweza kujizuia kufikiria mwenyewe: ni lazima nifanye vyema. Ningetimiza wajibu wangu vibaya, viongozi wangu na wafanyakazi wenzangu wangenionaje? Matokeo yake yalikuwa, tulipozungumzia mada fulani pamoja, almradi nilikuwa na ufahamu kidogo wa mada hiyo, basi ningejaribu kuwa wa kwanza kusema kitu, hata hivyo wakati sikuwa na ufahamu wa mada iliyojadiliwa na sikuweza kusema chochote, nilijipata nikiwa na wasiwasi.

“Mji Utaangushwa” (4) - Je, Kufafanua Biblia ni Sawa na Kutukuza na Kutoa Ushuhuda kwa Mungu?


Watu wengi katika ulimwengu nzima wa dini huamini kwamba wale ambao wanaweza zaidi kueleza Biblia ni watu wanaomjua Mungu, na kwamba kama wao pia wanaweza kufafanua siri za Biblia na kueleza unabii, basi wao ni watu ambao hufuata mapenzi ya Mungu, na wanatukuza na kutoa ushuhuda kwa Mungu. Watu wengi, kwa hiyo, wana imani ya ujinga kwa mtu wa aina hii na humuabudu. Hivyo maelezo ya Biblia ya wachungaji na wazee wa kanisa kweli humtukuza na kutoa ushuhuda kwa Mungu? Mwenyezi Mungu asema, "Wale wanaosoma Biblia kwa makanisa makubwa hukariri Biblia kila siku, lakini hakuna yeyote anayeelewa madhumuni ya kazi ya Mungu.

7/05/2018

Kwa Nini Mungu Hutajwa Majina, na Jina Moja Linaweza Kuwakilisha Uzima wa Mungu?

Sura ya 2 Ukweli wa Majina ya Mungu

1. Kwa Nini Mungu Hutajwa Majina, na Jina Moja Linaweza Kuwakilisha Uzima wa Mungu?

Maneno Husika ya Mungu:
Je, Jina la Yesu “Mungu pamoja nasi,” linaweza kuwakilisha tabia ya Mungu kwa ukamilifu wake? Je, linaweza kueleza Mungu kwa ukamilifu? Kama mwanadamu atasema ya kwamba Mungu Ataitwa tu Yesu, na hawezi kuwa na jina lingine kwa sababu Mungu hawezi kubadilisha tabia yake, basi maneno hayo ni kufuru! Je, unaamini kwamba jina la Yesu, Mungu pamoja nasi, linaweza kumwakilisha Mungu kikamilifu? Mungu Anaweza kuitwa majina mengi, lakini baina ya majina haya mengi, hamna moja ambalo linaweza kujumlisha yote ambayo Mungu Anamiliki, na hamna jina moja ambalo linaweza kumwakilisha Mungu kikamilifu.