6/30/2018

Nyimbo za Sifa | Moyo Wangu Hautatamani Chochote Zaidi

🎼🎼     → → πŸŽ™️πŸŽ™️  ↓↓    πŸ˜ŠπŸ˜Š       
~~~~~~~~~~~~🌺🌺🌺    **********     πŸ’“πŸ’“πŸ’“~~~~~~~~~~~~
πŸ˜‡πŸ˜‡
πŸ˜‡πŸ˜‡
Mungu amelipa gharama yote ya binadamu, akamwaga uhai Wake wote juu yetu.
Nahisi huzuni na kumwaga machozi ya majuto. Bila kujua nilimfanya Mungu ateseke sana.
Ni nini kilichopo ambacho siwezi kuachilia ili kuutosheleza moyo wa Mungu?

Umeme wa Mashariki | Ubia wa Kweli

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Ushuhuda

Umeme wa Mashariki | Ubia wa Kweli

Fang Li    Jiji la Anyang, Mkoa wa Henan
Hivi karibuni nilidhani nilikuwa nimeingia katika ubia wenye kuridhisha. Mshirika wangu na mimi tuliweza kujadili kitu chochote, wakati mwingine hata nikamwomba aonyeshe dosari zangu, na hatukupigana kamwe, hivyo nilidhani tulikuwa tumefanikisha ubia wenye kuridhisha. Lakini kama ukweli ulivyofichua, ubia wenye kuridhisha kwa kweli haukuwa kama kitu chochote nilichosadiki.

6/29/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kazi na Kuingia (9)

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kazi na Kuingia (9)

Tamaduni za asili na mitazamo ya kiakili madhubuti vimeweka kivuli katika roho safi na ya kitoto ya mwanadamu, vimeshambulia roho ya mwanadamu bila ubinadamu hata kidogo kana kwamba anaondolewa hisia na hali yoyote ya nafsi. Mbinu za mashetani hawa ni za kikatili kupita kiasi, na ni kana kwamba "elimu" na "malezi" vimekuwa ni njia za kitamaduni ambazo kwazo mfalme wa mashetani anamchinja mwanadamu;

"Mji Utaangushwa" (3) - Ni Nini Kiini cha Upinzani wa Mafarisayo kwa Mungu?


Kwa miaka elfu mbili, ingawa waumini wote wamejua ukweli kwamba Mafarisayo walimwasi Bwana Yesu, hakuna mtu katika ulimwengu mzima wa dini anayejua hasa mzizi wa chanzo na kiini cha uasi wa Mafarisayo kwa Mungu ni nini. Ni katika kuja kwa Mwenyezi Mungu tu katika siku za mwisho ndiyo ukweli wa swali hili unaweza kufichuliwa. Mwenyezi Mungu asema, "Mafarisayo hawa kwa dutu walikuwa wakaidi, wenye kiburi na hawakutii ukweli.

6/28/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Sura ya 13

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Sura ya 13

      Mwenyezi Mungu alisema, Mungu anachukia urithi wote wa joka kubwa jekundu, na Hulichukia joka kubwa jekundu hata zaidi. Huu ni mzizi wa ghadhabu iliyo ndani ya moyo wa Mungu. Inaonekana kwamba Mungu anataka kutupa vitu vyote ambavyo ni mali ya joka kubwa jekundu ndani ya ziwa la moto wa jahanamu kuviteketeza kabisa. Kuna nyakati ambazo hata inaonekana kwamba Mungu anataka kuunyosha mkono Wake kuliangamiza binafsi—hilo tu ndilo lingeweza kufuta chuki iliyo ndani ya moyo Wake.

Kuhusu Mungu Kumtumia Mwanadamu

Mwenyezi Mungu alisema, Hakuna mtu anayeweza kuishi kwa kujitegemea isipokuwa wale ambao wanapewa uelekeo maalumu na mwongozo na Roho Mtakatifu, kwani wanahitaji huduma na uchungaji wa wale wanaotumiwa na Mungu. Hivyo, katika kila enzi Mungu huwainua watu tofauti ambao hujishughulisha na kuchunga makanisa kwa ajili ya kazi Yake. Ambalo ni kusema, kazi ya Mungu lazima ifanywe kupitia wale ambao Huwaonyesha fadhili na kuwakubali;

6/27/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Sitapumbazwa Tena na "Nia Njema"

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, ushuhuda

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Sitapumbazwa Tena na "Nia Njema"

Meng Yu    Mji wa Pingdingshan, Mkoa wa Henan
Wakati mmoja nilipokuwa nikitimiza wajibu wangu, niliona kuwa ndugu fulani alikuwa akijaribu kuwafurahisha dada zake, maonyesho ya hali mbovu ya tabia yake machoni mwangu. Niliamua kutafuta fursa ya kumkumbusha haya mambo. Siku zilipita na nikaona utendaji wake wa wajibu ulikuwa wenye matokeo machache mazuri—ushahidi wa maoni yangu ya awali kumhusu.

Matamshi ya Mungu | Maisha Ya Kawaida ya Kiroho Huwaongoza Watu Kwenye Njia Sahihi

Mwenyezi Mungu alisema, Mmetembea tu sehemu ndogo sana ya njia ya muumini katika Mungu, na bado hamjaingia kwenye njia sahihi, kwa hiyo bado mko mbali na kutimiza kiwango cha Mungu. Hivi sasa, kimo chenu hakitoshi kuyakidhi mahitaji Yake. Kwa sababu ya ubora wenu wa tabia na vilevile asili yenu ya maumbile ya upotovu, nyinyi daima huichukulia kazi ya Mungu kwa uzembe na hamuichukulii kwa uzito. Hii ni dosari yenu kubwa zaidi.

6/26/2018

Umeme wa Mashariki | Njia Yote Pamoja na Wewe

Umeme wa Mashariki |  Njia Yote Pamoja na Wewe

I
Nilikuwa kama mashua, ikielea baharini.
Ulinichagua,
na mahali pazuri Uliniongoza.
Sasa katika familia Yako,
nikipewa joto na upendo Wako,
nina amani kabisa.

Kama Tu Binadamu Watamwabudu Mungu wa Kweli Ndiyo Wataweza Kuwa na Jaala Nzuri

Mungu aliumba dunia hii. Aliumba binadamu.
Alikuwa mjenzi wa utamaduni wa zamani wa Ugiriki na ustaarabu wa binadamu.
Mungu tu ndiye Anayefariji, Anayefariji binadamu huyu.
Mungu pekee ndiye Anayejali kuhusu binadamu huyu mchana na usiku.

6/25/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Niko Tayari Kukubali Usimamizi wa Wote

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, ushuhuda

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Niko Tayari Kukubali Usimamizi wa Wote

Xianshang     Mji wa Jinzhong, Mkoa wa Shanxi
Muda mfupi uliopita, kila wakati niliposikia kwamba wahubiri wa wilaya walikuwa wakija kwa kanisa letu, ningehisi kutaharaki kiasi. Sikufichua hisia zangu kwa nje, lakini moyo wangu ulijaa upinzani wa siri. Nilidhani: "Ingekuwa bora kama nyinyi nyote hamkuja. Mkija, angalau msifanye kazi kanisani nami. Vinginevyo, nitakuwa nimewekewa mipaka na kutoweza kuwasiliana kwa karibu." Baadaye, hali hiyo ilikuwa mbaya sana kiasi kwamba kwa kweli nilichukia kuja kwao. Hata hivyo, sikufikiri kwamba kulikuwa na kitu kibaya nami na bila shaka sikujaribu kujijua katika mazingira ya hali hii.

"Mji Utaangushwa" (2) - Mbona Dhiki Imewafika Mafarisayo Wanafiki?



Imeandikwa katika Biblia kwamba Bwana Yesu aliwalaani Mafarisayo kwa dhiki saba. Siku hizi, njia inayotembelewa na wachungaji na wazee wa ulimwengu wa dini ni ile ya Mafarisayo na hali kadhalika wanapitia chuki ya Mungu na kukataliwa. Hivyo kwa nini Bwana Yesu aliwahukumu na kuwalaani Mafarisayo? Kimsingi ilikuwa kwa sababu walikuwa na kiini chenye unafiki ambacho kilimwasi Mungu, kwa sababu walitilia maanani kufanya matambiko ya dini na kufuata sheria tu, walieleza kanuni na mafundisho katika Biblia tu na hawakuweka maneno ya Mungu kwenye vitendo wala kufuata amri za Mungu kwa vyovyote, na hata waliacha amri za Mungu.

6/24/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kuvunja Pingu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, ushuhuda

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kuvunja Pingu


Zhenxi Jijini Zhenzhou, Mkoani Hena
Miaka kumi iliyopita, nikiendeshwa na asili yangu ya kiburi, sikuweza kamwe kutii kikamilifu mipangilio ya kanisa. Ningetii ikiwa ilinifaa, lakini iwapo haingenifaa ningechagua iwapo ningetii au la. Hili lilisababisha kukiuka sana mipangilio ya kazi wakati wa kutimiza wajibu wangu. Nilifanya jambo langu mwenyewe na kuichukiza tabia ya Mungu, na hivyo baada ya hapo nilitumwa nyumbani.

6/23/2018

Nyimbo ya Msifuni Mwenyezi Mungu | Maisha Yetu Sio Bure

Nyimbo ya Msifuni Mwenyezi Mungu  | Maisha Yetu Sio Bure

Maisha yetu sio bure.
Maisha yetu sio bure.

🎧🎧🎧🎧🎧🎧~~~~~🎼🎼🎼🎼🎼~~~~~~😍😍😍
I
Leo tunakutana na Mungu,
tunapitia kazi Yake.
Tumemjua Mungu katika mwili,
wa utendaji na wa hakika.

Mungu Aliilinda Familia Yetu Wakati wa Maafa

***********🌼🌼🌼❤️❤️❤️***********
~~~~~~~❤️❤️❤️🌻🌻🌻************🌻🌻🌻❤️❤️❤️~~~~~~
Wang Lan, Beijing
Agosti 6, Mwaka wa 2012
Mnamo Julai 21, mwaka wa 2012, mafuriko makubwa zaidi tangu miaka sitini yalipitia kijijini mwetu kwa nguvu mno. Maafa yalianguka kutoka mbinguni, maji ya mafuriko yalichanganya matope na mawe na kuharibu kijiji chote. Nyumba nyingi ziliharibiwa na maji na maporomoko ya matope.

6/22/2018

C. Jinsi Ambavyo Shetani Anatumia Desturi ya Kitamaduni Kumpotosha Mwanadamu | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Je, kuna mambo mengi yanayochukuliwa kuwa sehemu ya desturi ya kitamaduni? (Ndiyo.) Hii desturi ya kitamaduni inamaanisha nini? (Inapitishwa kutoka kwa mababu.) Inapitishwa kutoka kwa mababu, hiki ni kipengele kimoja. Familia, vikundi vya makabila, na hata jamii ya binadamu imepitisha njia yao ya maisha kutoka mwanzo, ama imepitisha mila, misemo, na kanuni, ambazo zimeingizwa kwa fikira za watu.

6/21/2018

Hekima Kubwa Mno ni Kumwinua Mungu na Kumtegemea Yeye

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, maombi

❤️❤️❤️❤️❤️πŸ˜‡πŸ˜‡πŸ˜‡πŸ˜‡πŸ˜‡
↓↓↓↓↓↓
πŸ’ͺπŸ’ͺπŸ’ͺπŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘
⇩⇩⇩⇩
πŸ‘πŸ‘πŸ‘
Lingxin    Mji wa Shijiazhuang, Mkoa wa Hebei
Siku chache zilizopita, nilisoma kifungu kutoka "Njia ya Kuingia Katika Uhalisi" katika Ushirika na Kuhubiri Kuhusu Kuingia Katika Maisha (IV): "Kwa mfano, sasa kuna mtu ambaye amechukua mzunguko mbaya. Kutumia hili kama hoja ya kuzungumza ili kuwasiliana ukweli, ungefanyaje hivyo? ... Kwanza, unapaswa kushuhudia kazi ya Mungu, kushuhudia jinsi Mungu huwaokoa wanadamu. Kisha, unaweza kuzungumza juu ya kama barabara anayotumia inaongoza kwa wokovu wa Mungu, kama anaweza kupata kazi ya Roho Mtakatifu, na kama hii ni barabara ambayo Mungu huikubali. Hivyo, kwanza unashuhudia kazi ya Mungu, na kisha ushuhudie barabara ambayo Mungu anatuongozea, yaani, barabara ya wokovu.

"Mji Utaangushwa" (1) - Ulimwengu wa Dini Umepotoka na kuwa Mji wa Babeli


Viongozi wa ulimwengu wa dini wanapotea toka kwenye njia ya Bwana na kufuata mitindo ya kidunia, pia wao hushirikiana na uasi mkali wa mamlaka ya utawala na shutuma ya Umeme wa Mashariki, na tayari wameanza kutembea kwenye njia ya upinzani kwa Mungu. Ulimwengu wa dini umepotoka na kuwa mji wa Babeli. Biblia inasema, "Na Yesu akaingia katika hekalu la Mungu, na akawafukuza wote waliokuwa wakiuza na kununua katika hekalu, na akazipindua meza za wabadilishaji wa fedha, na viti vya wale waliokuwa wakiuza njiwa, Na akawaambia, imeandikwa, nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala;

6/20/2018

Umeme wa Mashariki | Tamko la Thelathini na Tatu

Umeme wa Mashariki | Tamko la Thelathini na Tatu


Mwenyezi Mungu alisema, Katika nyumba Yangu, kulikuwapo wakati mmoja wale waliolisifu jina Langu takatifu, ambao walifanya kazi bila kuchoka ili utukufu Wangu duniani ungejaza anga. Kwa sababu ya hili, Nilifurahi sana, moyo Wangu ulijawa na furaha—lakini nani angeweza kufanya kazi badala Yangu, akiacha usingizi usiku na mchana? Azimio la mwanadamu mbele Yangu hunipa raha, lakini uasi wake huchochea hasira Yangu, na hivyo, kwa sababu mwanadamu hawezi kamwe kuzingatia wajibu wake, huzuni Yangu kwa ajili yake inakua kubwa zaidi.

Matokeo ya Mwisho Ambayo Kazi ya Mungu Inalenga Kufanikisha

Katika nyingi ya kazi ya Mungu,
mtu yeyote aliye na uzoefu wa kweli anahisi uchaji na heshima Kwake,
ambayo ni zaidi ya sifa.
Hukumu Yake na kuadibu
vinawafanya watu waone tabia Yake,
na kumcha katika mioyo yao.

6/19/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko la Thelathini

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko la Thelathini

Kati ya binadamu, wakati mmoja Nilifanya muhtasari wa ukaidi na udhaifu wa mwanadamu, na hivyo Nilielewa udhaifu wa binadamu na Nikafahamu vema ukaidi wake. Kabla ya kuwasili kati ya binadamu, Nilikuwa nimekuja kuelewa kitambo furaha na huzuni kati ya binadamu—na kwa sababu ya hili, Ninaweza kufanya kile ambacho binadamu hawezi, na kusema kile ambacho binadamu hawezi, na Mimi hufanya hivyo kwa urahisi sana. Je, hii siyo tofauti kati ya Mimi na binadamu?

6/18/2018

Mwenyezi Mungu Amenipa Fursa ya Pili Katika Maisha


Ndugu wawili wa kawaida, Beijing 
                                                        
                                                                     Agosti 15, 2012
Julai 21, mwaka wa 2012 ilikuwa siku isiyosahaulika sana kwangu, pamoja na kuwa siku muhimu zaidi ya maisha yangu.
Siku hiyo, mvua kubwa ilikuwa ikinyesha katika Wilaya ya Fangshan jijini Beijing—ilikuwa kubwa kuliko yoyote iliyowahi kuonekana pale katika miaka sitini na mmoja. Muda mfupi baada ya saa 4 jioni, nilitoka nje mtaani ili kuangalia na nikaona kuwa maji yalikuwa kila mahali. Gari la familia yetu lilikuwa tayari limeelea, na sababu ya pekee gari hilo kutosombwa na mkondo wa maji ilikuwa kwamba lilizuiwa na kitu mbele yake kilicholizuia kusonga.

Chochote Mungu Asemacho Ndiyo Hukumu Hasa ya Mwanadamu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kanisa
Xunqiu    Mji wa Nanyang, Mkoa wa Henan
Nilikuwa nikidhani kwamba Mungu alimhukumu na kumuadibu mwanadamu wakati tu Alipoufichua upotovu wa asili wa mwanadamu au alipoeleza maneno mkali ambayo yaliuhukumu mwisho wa mwanadamu. Ilikuwa ni baadaye kabisa tu ambapo tukio moja liliponiongoza kutambua kwamba hata maneno mapole ya Mungu pia yalikuwa ni hukumu na kuadibu Kwake. Niligundua kuwa kila neno Alilolisema Mungu ni hukumu Yake kwa mwanadamu.

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Si Rahisi Kuwa Mtu Mwaminifu

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Si Rahisi Kuwa Mtu Mwaminifu
Zixin    Jiji la Wuhan, Mkoa wa Hubei
Kupitia kula na kunywa neno la Mungu na kusikiliza mahubiri, nilikuja kuelewa umuhimu wa kuwa mtu mwaminifu na hivyo nikaanza kufanya mazoezi kuwa mtu mwaminifu. Baada ya muda, niliona kuwa nilipata kuingia kiasi katika kuwa mtu mwaminifu. Kwa mfano: Wakati wa kuomba au kuzungumza na mtu, ningeweza kuongea ukweli na kutoka kwa moyo; niliweza pia kuchukulia kutekeleza wajibu wangu kwa uzito, na wakati nilipofichua upotovu niliweza kujiweka wazi kwa watu wengine.

6/17/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Ufafanuzi wa Tamko la Arubaini

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Ufafanuzi wa Tamko la Arubaini

Kwa Mungu, mwanadamu ni kama mtu anayechezewa katika mshiko Wake, kama nudo inyoshwayo kwa mkono katika mikono Yake—inayoweza kufanywa nyembamba au nzito kama apendavyo Mungu, kuifanyia Apendavyo. Ni haki kusema kwamba mwanadamu kwa kweli ni mtu anayechezewa mikononi mwa Mungu, kama paka wa Uajemi ambaye bibi amemnunua kutoka sokoni. Bila shaka, yeye ni mtu anayechezewa mikononi mwa Mungu—na kwa hiyo hakukuwa na chochote cha uongo kuhusu ufahamu wa Petro.

Meupe na Safi ni Maji yaliyo Kando ya Kiti cha Enzi cha Mungu

Maji yaliyo kando ya kiti cha enzi cha Mungu, safi na meupe, yanatulisha sisi.
Neno la Mungu, maji ya uzima, mtiririko unaostawisha mioyo yetu.
Mwenyezi Mungu, tunakusifu Wewe. Shukrani ziwe Kwako na mwanga Wako!
Kutoka kwa upotovu Ulituokoa, hivyo sasa tunaishi katika mwanga Wako!
Sasa tunaishi katika mwanga Wako!

6/16/2018

Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Unampenda Mungu kiasi gani hasa leo? Na unajua kiasi gani hasa kuhusu yote ambayo Mungu amefanya ndani yako? Haya ni mambo unayopaswa kujifunza. Mungu anapowasili duniani, yote ambayo Amefanya ndani ya mwanadamu na kumkubalia mwanadamu kuona ni ili mwanadamu atampenda na kumjua Yeye kweli. Kwamba mwanadamu anaweza kuteseka kwa ajili ya Mungu na ameweza kufikia umbali huu ni, kuhusiana na jambo moja, kwa sababu ya upendo wa Mungu, na kuhusiana na jambo lingine, ni kwa sababu ya wokovu wa Mungu;

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Wivu, Ugonjwa Sugu Wa Kiroho

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, upendo wa Mungu


Kanisa la Mwenyezi Mungu | Wivu, Ugonjwa Sugu Wa Kiroho



He Jiejing    Jiji la Hezhou, Mkoa wa Guangxi
Dada mmoja na mimi tuliunganishwa ili tusahihishe makala pamoja. Tulipokuwa tukikutana, nilitambua kuwa haikujalisha kama ilikuwa ni kuimba, kucheza ngoma, kupokea neno la Mungu, au kuwasiliana ukweli, huyu dada alikuwa bora kuniliko katika kila kipengele. Ndugu wa kiume na wa kike wa familia mwenyeji wote walimpenda na wangezungumza naye. Kwa sababu ya hili, moyo wangu ulikuwa na wasiwasi sana na nilihisi kama nilikosa kuthaminiwa—hata kufikia kiasi kwamba nilifikiri kuwa mradi alikuwa huko, hakukuwa na nafasi yangu.

6/15/2018

Ni Nini Ambacho Kimeidanganya Roho Yangu?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kanisa
Xu Lei     Mji wa Zaozhuang, Mkoa wa Shandong
Siku moja nilipokea taarifa juu ya mkutano. Kwa kawaida hili ni tukio la kufurahisha, lakini mara tu nilipofikiria jinsi kazi yangu hivi karibuni ilikuwa machafuko kabisa, sikuweza kujizuia kuhisi wasiwasi. Kama mkuu wangu angejua jinsi sikuwa nimemaliza kazi yoyote yangu, bila shaka angehitaji kunishughulikia, na huenda hata kunibadilisha na mwingine kaziniNingefanya nini basi? Siku iliyofuata nilikwenda kwa mkutano na moyo mzito. Nilipofika huko, nikaona kwamba mkuu wangu alikuwa bado hajafika, lakini baadhi ya wafanyakazi wenzangu walikuwa hapo tayari. 

Kila Neno la Mungu ni Maonyesho ya Tabia Yake

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, kanisa
Hu Ke    Mji wa Dezhou, Mkoa wa Shandong
Wakati wowote nilipoona maneno haya yaliyosemwa na Mungu, nilihisi kuwa na wasiwasi: “Kila sentensi Niliyoizungumza inaendeleza tabia ya Mungu. Mngefanya vizuri zaidi endapo mngetafakari kuhusu maneno Yangu kwa umakini, na kwa kweli mtafaidi pakubwa kutoka katika maneno haya.” Nilihisi kuwa na wasiwasi kwa sababu kuelewa tabia ya Mungu ni muhimu sana yote kwa ufahamu wa mwanadamu wa Mungu na kutafuta kumpenda na kumridhisha Yeye.

6/14/2018

Sura ya 9. Kutafuta Mapenzi ya Mungu na Kuuweka Ukweli Katika Vitendo Kwa Kiasi Kikubwa Zaidi Iwezekanavyo

Mwenyezi Mungu alisema, Punde tu watu wanapokuwa na haraka wakati wakiutumiza wajibu wao, hawajui jinsi ya kuuzoea; punde tu wanaposhughulika na mambo, hali yao ya kiroho inakuwa na matatizo; hawawezi kudumisha hali yao ya kawaida. Inawezekanaje kuwa hivi? Unapoombwa kufanya kazi kidogo, haufuati ukawaida, unakosa mipaka, husogei karibu na Mungu na unajitenga mbali na Mungu. Hili linadhibitisha kwamba watu hawajui jinsi ya kuwa na uzoefu. Haidhuru nini ufanyacho, unapaswa kwanza kuelewa halisi kwa nini unalifanya hili na asili ya jambo hili ni lipi.

Kutumia Neno la Mungu Kama Kioo

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kanisa
Wu Xia    Mji wa Linyi , Mkoa wa Shandong
Baada ya kuikubali kazi hii na kula na kunywa neno la Mungu, ilikuwa dhahiri kwangu kwamba ni muhimu sana kwamba mimi nijifahamu. Kwa hiyo, nilipokuwa nikila na kunywa neno la Mungu, nilihakikisha nimejithibitisha tena dhidi ya neno ambalo Mungu humfichua mwanadamu. Katika hali nyingi, niliweza kutambua kasoro zangu na upungufu. Nilihisi kwamba ningekuja kujifahamu kweli. Hata hivyo, ilikuwa ni kwa njia ya ufunuo kutoka kwa Mungu tu nilipoweza kuona kwamba kwa hakika sikujifahamu kulingana na neno la Mungu.

6/13/2018

Ahadi ya Mungu kwa Waisraeli

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, injili
Katika mwaka wa Bwana wetu, mtoto wa kiume alizaliwa katika hori kwa nyumba ya wageni katika Bethlehemu ya Uyahudi. Wanaume watatu wenye busara kutoka mashariki, wakiongozwa na nyota ambayo haikuwahi kuonekana kabla, walifika mahali pa kuzaliwa kwa mtoto.Wakamsujudia kwa ibada. Mtoto huyu Ndiye aliyeahidiwa na Mungu, ambaye angewaongoza na kuwakomboa Waisraeli kutoka kwa sheria.
Soma Zaidi:Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Mwenyezi Mungu alisema, Wakati Yesu Alikuja kufanya kazi yake, ilikuwa ni kwa uongozi wa Roho Mtakatifu;

Maangamizo ya Mungu ya Dunia kwa Mafuriko

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, injili
“Mwisho wa kila mwenye mwili umekuja mbele zangu; kwa sababu dunia imejawa na dhuluma kupitia kwao; na, tazama, nitawaharibu pamoja na dunia” (Mwanzo 6:13).
Yaliyopendekezwa: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Tazama Video: ~~~~~~~~~~****************~~~~~~~~~~~

Safina ya Siku za Mwisho | “Siku za Nuhu Zimekuja” Swahili Gospel Video


6/12/2018

Mwenyezi Mungu, Sasa Niko na Wewe

Mwenyezi Mungu, sasa kwa sababu tuko na Wewe, masumbuko yanabadilika kuwa furaha.
Kula, kunywa, kufurahia maneno Yako, tuko na Wewe kila siku.
Maji Yako ya uzima yanatustawisha, tuna ukarimu kwa vyote.
Jua ukweli, ingia katika ukweli, yote yanakutegemea Wewe.
Ndugu, acha tule, tunywe maneno ya Mungu.
Shirikini na ukweli Wake, mkifurahia neema Yake, ishini katika ufalme Wake kila wakati.
Dada, pendaneni kila mmoja.

New Swahili Gospel Movie "Mji Utaangushwa" | Hukumu katika Siku za Mwisho


Cheng Huize ni mfanyakazi mwenzi katika kanisa la nyumba huko China. Ameamini katika Bwana kwa miaka mingi, na amefanya kazi kwa ajili ya Bwana kwa shauku thabiti. Yeye hujitwisha majukumu mengi kwa ajili ya kanisa, na ana huruma kwa ndugu zake. Kanisa lake lilipokua na ukiwa zaidi na zaidi kila siku, uovu katika kanisa lake ulionekana mara kwa mara zaidi na zaidi. Mchungaji alipendekeza kwa juhudi kwamba kanisa lilipaswa kuanzisha kiwanda, na akawaongoza wafuasi kwenye njia ya utajiri, na pia kuwashawishi wao kujiunga na Kanisa la Nafsi Tatu ili kwamba wangeweza kutegemea msaada toka kwa serikali ya kikomunisti ya China. Hii ilisababisha mjadala mkali kujitokeza.

6/11/2018

Umeme wa Mashariki | "Kuona Ni Kuamini" Haipaswi Kuaminiwa

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, ushuhuda

Umeme wa Mashariki | "Kuona Ni Kuamini" Haipaswi Kuaminiwa


Xiaowen   Mji wa Zhengzhou, Mkoa wa Henan
Awali, nilipokuwa nikisikia watu wakitoa maoni juu ya kitu fulani, mara nyingi wangesema "kuona ni kuamini." Muda ulivyoendelea kupita, pia nilichukua huu kama msingi wa kuangalia mambo, na ilikuwa vivyo hivyo kuhusu maneno ya Mungu. Matokeo yake ni kwamba niliishia kutoweza kuamini maneno mengi ya Mungu ambayo hayakuwa yametimizwa. Kama wakati wangu uliotumiwa kumwamini Mungu ulipoongezeka, niliona maneno ya Mungu kwa viwango tofauti vya kutimizwa , nikaona ukweli wa mafanikio ya maneno ya Mungu na sikuwa tena na shaka juu ya chochote ambacho Mungu alisema.

Matamshi ya Mungu | Kile Ambacho Mchungaji wa Kutosha Anapaswa Kujiandaa Nacho

Mwenyezi Mungu alisema, Lazima uwe na ufahamu wa hali nyingi ambazo watu watakuwa ndani wakati Roho Mtakatifu anafanya kazi juu yao. Hasa, wale wanaofanya kazi kwa namna sawa kumtumikia Mungu lazima wawe na ufahamu bora zaidi wa hali nyingi zinazoletwa na kazi ambayo Roho Mtakatifu hutekeleza kwa wanadamu. Ikiwa unasema tu kuhusu uzoefu mwingi na njia nyingi za kuingia ndani, inaonyesha kwamba uzoefu wa watu unaegemea upande mmoja sana. Bila kufahamu hali nyingi kwa kweli, huwezi kufikia mbadiliko katika tabia yako.

Umeme wa Mashariki | Siri Niliyoishikilia kwa Kina Ndani ya Moyo Wangu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, hukumu

Umeme wa Mashariki | Siri Niliyoishikilia kwa Kina Ndani ya Moyo Wangu

Wuzhi    Mji wa Linyi, Mkoa wa Shandong
Katika majira ya kuchipua ya mwaka wa 2006, nilinyang'anywa cheo changu kama kiongozi na nikarudishwa nilikotoka kwa sababu nilifikiriwa kuwa "bwana ndiyo" sana. Niliporejea mara ya kwanza, nilitumbukia ndani ya kikalibu cha mateso na maumivu makubwa. Sikuwahi kufikiri kwamba baada ya miaka mingi ya uongozi mambo yangeharibika kwa sababu ya kuwa "bwana ndiyo." Huu ulikuwa ndio mwisho kwangu, nilidhani, kila mtu aliyenijua angejua juu ya kushindwa kwangu na ningefanywa kama mfano mbaya katika kanisa.

6/10/2018

Umeme wa Mashariki | Tafakuri kuhusu Kubadilishwa

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Wakristo

Umeme wa Mashariki | Tafakuri kuhusu Kubadilishwa

Yi Ran    Mji wa Laiwu , Mkoa wa Shandong
Wakati fulani awali, kwa sababu yangu kutoelewa kanuni iliyotumiwa na kanisa ya masahihisho ya wafanyakazi wa kanisa, wakati kanisa lilibadilisha kiongozi, dhana iliibuka ndani yangu. Kutoka kwa kile nilichoweza kuona, dada aliyebadilishwa alikuwa mzuri sana kwa kupokea na kushirikiana ukweli, na aliweza kuwa wazi juu ya maonyesho yake ya upotovu. Kwa hiyo sikuweza kujua asilani jinsi mtu fulani aliyetafuta ukweli sana angeweza kubadilishwa.

6/09/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kujijua Mwenyewe Hasa Ni Kujua Asili ya Binadamu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kujijua Mwenyewe Hasa Ni Kujua Asili ya Binadamu 

La muhimu katika kufikia badiliko la tabia ni kujua asili ya mtu mwenyewe, na hili ni lazima litoke kwa ufunuo na Mungu. Ni katika neno la Mungu tu ambapo mtu anaweza kujua asili yake ya kutia kinyaa, afahamu katika asili yake mwenyewe sumu mbalimbali za Shetani, atambue kuwa yeye ni mjinga na mpumbavu, na atambue dalili dhaifu na hasi katika asili yake mwenyewe. Mara haya yanapojulikana kikamilifu, na unaweza kwa hakika kunyima mwili, daima kutekeleza neno la Mungu, na kuwa na mapenzi ya kujiwasilisha kikamilifu kwa Roho Mtakatifu na kwa neno la Mungu, basi umeianza njia ya Petro.

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Vigezo vya Mtu Mwema Kwa Dhati

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kanisa

Kanisa la Mwenyezi Mungu | 28. Vigezo vya Mtu Mwema Kwa Dhati

Moran   Mji wa Linyi, Mkoa wa Shandong
Tangu nilipokuwa mtoto, siku zote nilishikiza umuhimu mkubwa kwa jinsi watu wengine walivyoniona na ukadiriaji wao kwangu. Ili niweze kupata sifa kutoka kwa wengine kwa kila kitu nilichokifanya, sikubishana na yeyote asilani wakati wowote kitu chochote kilichoibuka, ili kuepuka kuharibu picha nzuri watu wengine walikuwa nayo kwangu. Baada ya kuikubali kazi ya Mungu katika siku za mwisho, niliendelea kwa njia hii, nikizingatia kwa kila njia iwezekanayo picha nzuri ambayo ndugu zangu wa kiume na wa kike walikuwa nayo kwangu.

6/08/2018

Kutatua Asili na Kutenda Ukweli

1. Uhusiano Kati ya Ubinadamu na Uwezo wa Kutenda Ukweli
Mwenyezi Mungu alisemaWatu husema kuwa kutenda ukweli ni vigumu kabisa. Basi mbona watu wengine wanaweza kutenda ukweli? Watu wengine husema ni kwa sababu kwa asili wanaipokea kazi ya Roho Mtakatifu ikifanya kazi juu yao, na pia kwa sababu ni wazuri kiasili. Hoja hii ina kiwango fulani cha mantiki. Watu wengine ni wazuri kiasili; wana uwezo wa kutenda ukweli. Ubinadamu wa watu wengine ni mnyonge, hivyo ni vigumu kwao kutenda ukweli; hii inamaanisha kuwa watakumbana na matatizo fulani.

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Sura ya 9

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Sura ya 9

Mwenyezi mungu alisema, Katika mawazo ya watu, Mungu ni Mungu, na mwanadamu ni mwanadamu. Mungu haneni lugha ya mwanadamu, wala mwanadamu hawezi kunena lugha ya Mungu, na kwa Mungu, madai ya mwanadamu Kwake ni rahisi, ilhali matakwa ya Mungu kwa mwanadamu hayafikiki na hayafikiriki kwa mwanadamu. Ukweli, hata hivyo, ni kinyume kabisa: Mungu anataka tu "asilimia 0.1" ya mwanadamu. Hili si la kushangaza tu kwa kila mtu, lakini pia huwafanya wahisi kukanganyikiwa sana, kama kwamba wote wamechanganyikiwa.

6/07/2018

Umeme wa Mashariki | Ufafanuzi wa Tamko la Thelathini na Sita

Umeme wa Mashariki | Ufafanuzi wa Tamko la Thelathini na Sita

Mwenyezi Mungu alisema, Inasemekana kwamba Mungu ameanza sasa kuwaadibu watu, lakini hakuna yeyote anayeweza kusema kwa hakika, hakuna yeyote anayeweza kutoa jibu dhahiri iwapo kusudi la asili la kuadibu huku limewafika wanadamu. Kwani Mungu asema, "Mwanadamu hajawahi kugundua chochote katika kuadibu Kwangu, kwani hafanyi chochote ila kushika nira inayozunguka shingo kwa mikono miwili, macho yake mawili yakiwa yamekodolewa Kwangu, kana kwamba anamwangalia adui kwa makini—na wakati huu tu ndio Nahisi vile amedhoofishwa.

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko la Arubaini

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko la Arubaini

Watu hukodolea macho kila mwendo Wangu, kana kwamba Nakaribia kuleta mbingu chini, na wao kila mara hukanganyikiwa na shughuli Zangu, kana kwamba matendo Yangu ni yasiyoeleweka kabisa kwao. Hivyo, wao hufuata nyayo Zangu kwa yote watendayo, wakiogopa sana kwamba watakosea Mbinguni na kutupwa katika "ulimwengu wa wenye kufa." Sijaribu kuwashikilia watu, bali Huufanya upungufu wao lengo la kazi Yangu.

6/06/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 92. Njia ya Utendaji katika Kusuluhisha Ukaidi

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 92. Njia ya Utendaji katika Kusuluhisha Ukaidi


Ni vyema kupitia mazingira ya aina tofauti. Mungu hakupangii mazingira haya bila sababu. Yeye hakuongozi popote pale bila makusudi, bali Yeye huandaa mazingira fulani spesheli kwa kila mmoja—mazingira ya kifamilia, mazingira ya kimaisha, mazingira uliyokulia, na mazingira unatekeleza majukumu yako punde utakapo mwamini. Yeye hutayarisha hali au mazingira fulani spesheli kwako wewe kuzipitia.

Umeme wa Mashariki | Huduma ya Aina Hii Kwa Hakika Ni Ya Kudharauliwa

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kanisa

Umeme wa Mashariki | Huduma ya Aina Hii Kwa Hakika Ni Ya Kudharauliwa

Ding Ning Mji wa Heze, Mkoa wa Shandong
Katika siku chache zilizopita, kanisa limepanga mabadiliko katika kazi yangu. Nilipopokea wajibu huu mpya, niliwaza, "Ninahitaji kuchukua fursa hii ya mwisho kuita mkutano na ndugu zangu wa kiume na wa kike, niongee nao wazi juu ya mambo, na niwaache na picha nzuri." Kwa hiyo, nilikutana na mashemasi kadhaa, na kufikia mwisho wa wakati wetu pamoja, nikasema, "Nimeulizwa kuondoka hapa na kuenda kwa kazi tofauti. Natumaini mtamkubali kiongozi ambaye anakuja kuchukua nafasi yangu na kufanya kazi pamoja naye kwa moyo mmoja na wazo moja."

6/05/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ufalme Takatifu Umeonekana

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ufalme Takatifu Umeonekana

Jua la haki hung’aa juu ya nchi zote, linarejesha viumbe vyote vilivyo hai.
Watu wa Mungu wanakusanyika kwa furaha, ili kusifu mafanikio Yake makubwa.
Nchi zote wanacheza, wanaimba, wanashangilia. Kila kitu chenye pumzi kinakuja kusifu,
sifa kwa ushindi na kuja kwa siku ya Mungu.

Ee Mwenyezi Mungu, Mpendwa Wangu Mzuri

Mwenyezi Mungu, mpendwa wangu mzuri, Una moyo wangu.
Unapitia magumu, Unavumilia aibu, yote kwa ajili ya kutuokoa.
Unatoa maisha Yako kwangu, naona jinsi Ulivyo mzuri.
Unakuja duniani kutoka mbinguni, ukiwa mwenye mwili.
Uko hapa Ukiishi na sisi, lakini hakuna anayejua Wewe ni nani.
Sikuota kamwe kuwa Muumba Mwenyewe angekuja ulimwenguni.
Aa … mpendwa wangu! Aa … mpendwa wangu!

"Siri ya Utauwa: Mfuatano" (2) - Namna ya Kumfahamu Mungu Mwenye Mwili


Katika siku za mwisho, Mungu amepata mwili kufanya kazi ili kumwokoa mwanadamu. Lakini kwa sababu hatufahamu ukweli wa kupata mwili, tunamchukulia Mungu mwenye mwili kuwa sawa na mwanadamu wa kawaida, hatuwezi kuitambua sauti ya Mungu na tunajua hata kidogo zaidi jinsi ya kumkaribisha Bwana—kufikia kiwango ambacho hata tunaweza kufuata ulimwengu wa dini na nguvu zinazotawala kumkana na kumshutumu Mungu—hali haiwi tofauti na wakati ambapo Mungu alipata mwili kama Bwana Yesu kufanya kazi Yake ya Enzi ya Neema. 

6/04/2018

Umeme wa Mashariki | Jinsi ya kuelewa Umoja wa Mwili na Roho

Umema wa mashariki | Jinsi ya kuelewa Umoja wa Mwili na Roho

Mwenyezi Mungu alisema, Baadhi ya watu huuliza, “Mungu huangalia kwa makini moyo wa binadamu, na mwili na Roho wa Mungu ni moja. Mungu hujua kila kitu ambacho watu husema, kwa hivyo Mungu anajua kwamba sasa ninamwamini?” Kujibu hili swali huhusisha jinsi ya kuelewa Mungu mwenye mwili na uhusiano kati ya Roho Wake na mwili. Baadhi husema, “Mungu ni halisi kwa njia thabiti.” Wengine husema, “Yeye ni halisi kwa njia thabiti. Lakini mwili Wake na Roho Yake ni moja, kwa hivyo Yeye anapaswa kujua hilo!”

Kutoka kwa Mateso Kunatoka Harufu Nzuri ya Upendo

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Wakristo
Xiaokai, Mkoa wa Jiangxi
Mimi ni mwanamke wa kawaida wa mashambani, na, kwa sababu ya dhana ya kikabaila ya kuthamini tu watoto wa kiume, sikuweza kuinua kichwa changu mbele ya wengine kwa ajili ya aibu ya kutozaa mtoto wa kiume. Wakati tu nilikuwa nikiteseka zaidi kabisa, nilichaguliwa na Bwana Yesu na, miaka miwili baadaye, nilikubali wokovu wa Mwenyezi Mungu. Aidha, nilielewa ukweli mwingi kutoka kwa ndani ya maneno ya Mwenyezi Mungu na moyo wangu ulipata ufunguliaji wa kweli.

6/03/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Arubaini na Tano

Mwenyezi Mungu alisema, Wakati mmoja Nilichagua bidhaa nzuri kubaki ndani ya nyumba Yangu, ili ndani yake kungekuwa na utajiri usio na kifani, na ingepambwa hivyo, Nilipata raha kutokana na hilo. Lakini kwa sababu ya mtazamo wa mwanadamu Kwangu, na kwa sababu ya motisha za watu, Sikuwa na budi ila kuiweka kazi hii kando na kufanya kazi nyingine. Nitatumia motisha za mwanadamu kufanikisha kazi Yangu, Nitashawishi vitu vyote vinihudumie, na kusababisha nyumba Yangu kutokuwa ya kusononeka na ya ukiwa tena kama matokeo.

Tabia ya Mungu ni Haki na, Hata Zaidi, Upendo

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kanisa
Fang Xin, Beijing
Agosti 15, mwaka wa 2012
Tangu mwaka wa 2007, nilipoikubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, ingawa nimeonekana juu juu kuwa na kazi nyingi sana kutekeleza majukumu yangu, sijaupa moyo wangu kwa Mungu, na mara nyingi nimehisi kufungwa kiasi cha msongo wa pumzi na masuala madogo ya familia. Kila wakati ninapowaza kuhusu ukweli kwamba binti yangu tayari ana umri wa miaka thelathini, na angali bado hajapata mwenzi wa kufaa, mimi hulalamika kwa Mungu;

6/02/2018

Usitafute Mbinu Mpya Unapomtumikia Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Wakristo
Heyi   Mji wa Zhuanghe, Mkoa wa Liaoning
Nilikuwa nimepandishwa cheo tu kuchukua jukumu la kiongozi wa kanisa. Lakini baada ya kipindi cha kazi ngumu, sio tu kuwa kazi ya kiinjili ilikuwa bila uhai kiasi, lakini ndugu zangu wa kiume na wa kike katika timu ya kiinjili walikuwa pia wakiishi katika hali hasi na ya udhaifu. Nikiwa nimekabiliwa na hali hii, sikuweza tena kudhibiti hisia zangu. Ni vipi tena ningeweza kuiamsha kazi ya kiinjili?

4. Bila Ya Wokovu wa Mungu, Singeweza Kuwa Hapa Leo

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, upendo wa Mungu
Zhang Jin, Beijing
Agosti 16, 2012
Mimi ni dada mzee mwenye miguu miwili yenye kasoro. Hata wakati hali ya hewa ni nzuri nje, nina shida kutembea, lakini wakati maji ya mafuriko yalipokuwa karibu kunimeza, Mungu aliniruhusu kutoroka hatari kimiujiza.
Ilikuwa Julai 21, mwaka wa 2012. Siku hiyo mvua ya mfoko ilinyesha, na nilikuwa tu nje nikitimiza wajibu wangu. Baada ya saa 10:00 mchana, mvua ilikuwa bado haijaisha.

6/01/2018

Umeme wa Mashariki | "Siri ya Utauwa: Mfuatano" (1) - Ni Jinsi Gani Bwana Ataonekana kwa Mwanadamu Atakaporudi Tena


Katika karne zote tangu Bwana Yesu alipofufuka na Akapaa mbinguni, sisi waumini tumetamani sana kwa hamu kurudi kwa Yesu Mwokozi. Watu wengi wanaamini kwamba utakuwa mwili wa kiroho wa Yesu aliyefufuka ambao utaonekana kwetu wakati Bwana atarudi. Lakini kwa nini Mungu ameonekana kwa mwanadamu akiwa mwili kama Mwana wa Adamu katika siku za mwisho? Mwenyezi Mungu asema, "Mungu Asipokuwa mwili, Atabaki kama Roho bila kuonekana au kuguswa na mwanadamu. Mwanadamu ni kiumbe wa mwili, na mwanadamu na Mungu ni wa dunia mbili tofauti na ni tofauti kwa asili.

Umeme wa Mashariki | 33. Mazungumzo Mafupi Kuhusu Chanzo cha Giza na Uovu wa Dunia na Uovu

Umeme wa Mashariki | 33. Mazungumzo Mafupi Kuhusu Chanzo cha Giza na Uovu wa Dunia na Uovu

Yang Le    Mji wa Wuhai, Eneo Huru la Mongolia la Ndani
Nilipokuwa bado shuleni, baba yangu alikuwa mgonjwa na akafa. Baada ya kufa, wajomba wa pande zote mbili za familia ambao mara nyingi walisaidiwa na baba yangu hawakukosa kututunza tu—mama yangu ambaye hakuwa na chanzo cha mapato, dada zangu wawili na mimi—lakini, kwa kinyume, walifanya kila kitu walichoweza kutengeneza faida kutoka kwetu, hata kupigana nasi kwa ajili ya urithi mdogo ambao baba yangu alikuwa ameacha.